Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi Jumatatu, Agosti 17, 2026, baada ya upande wa Jamhuri kuomba muda zaidi kutokana na changamoto za kiafya alizopata shahidi wa 18 aliyepaswa kuanza kutoa ushahidi leo Ijumaa.
Jana, shahidi wa 17 wa upande wa Jamhuri, ambaye utambulisho wake ulihifadhiwa na kutajwa kama ‘P’, alimaliza kutoa ushahidi wake. Miongoni mwa mambo aliyoyaeleza ni namna alivyoshiriki kama mwandishi wa habari katika kuripoti mkutano wa CHADEMA uliofanyika Aprili 3, 2025.
Upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama kuwa shahidi wa 18 amepata changamoto za kiafya, hivyo kuomba kesi hiyo iahirishwe.
Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, imekubali ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Jumatatu, Agosti 17, 2026.
Upande wa Jamhuri umeahidi kwamba Jumatatu utawaleta mashahidi wote waliobaki ili kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.