Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 5,383
- 18,776
Dunia hii haina haki kabisa.Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu imeahirishwa mpaka Jumatatu Agosti 17, 2026 baada ya upande wa mashataka ambao ni jamhuri kuomba kesi ihairishwe kwa madai kuwa shahidi wa 18 ambaye alibidi aanze kuhojiwa leo amepata changamoto za kiafya.
Upande wa Jamhuri umeahidi kwamba Jumatatu wataleta mashahidi wao wote waliobaki.
Shahidi amekimbia moto🤣Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu imeahirishwa mpaka Jumatatu Agosti 17, 2026 baada ya upande wa mashataka ambao ni jamhuri kuomba kesi ihairishwe kwa madai kuwa shahidi wa 18 ambaye alibidi aanze kuhojiwa leo amepata changamoto za kiafya.
Upande wa Jamhuri umeahidi kwamba Jumatatu wataleta mashahidi wao wote waliobaki.
Na Hilo ni Jopo la majaji watatu, waliotumia Mimbali ya Mahakama Kutengeza kuwa wanaendelea na kesi mfululizo🤣huu ni upumbavu sasa, kama vipi mtuhumiwa awe anatokea nyumbani kwake basi......!!! wanafanya kama kamchezo hivi as if huko jera anakorudishwa ni dubai.
Mambo ya Nolle presqueHata j3 sidhan kama watakuja wote
Mimi ni shahidi wa 18 bado nakariri matango niliyolishwa pia nitawaomba majaji wamzuie Lissu asinifanyie dodoso.Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, imeahirishwa hadi Jumatatu, Agosti 17, 2026, baada ya upande wa Jamhuri kuomba muda zaidi kutokana na changamoto za kiafya alizopata shahidi wa 18 aliyepaswa kuanza kutoa ushahidi leo Ijumaa.
Jana, shahidi wa 17 wa upande wa Jamhuri, ambaye utambulisho wake ulihifadhiwa na kutajwa kama ‘P’, alimaliza kutoa ushahidi wake. Miongoni mwa mambo aliyoyaeleza ni namna alivyoshiriki kama mwandishi wa habari katika kuripoti mkutano wa CHADEMA uliofanyika Aprili 3, 2025.
Upande wa Jamhuri umeieleza Mahakama kuwa shahidi wa 18 amepata changamoto za kiafya, hivyo kuomba kesi hiyo iahirishwe.
Mahakama Kuu, Masjala Ndogo Dar es Salaam, imekubali ombi hilo na kuahirisha kesi hadi Jumatatu, Agosti 17, 2026.
Upande wa Jamhuri umeahidi kwamba Jumatatu utawaleta mashahidi wote waliobaki ili kuendelea na ushahidi wa upande wa mashtaka.