Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Kesi ya Liyumba, Utata na Maendeleo yake

Status
Not open for further replies.
Wamejaribu kumtafuta kwenye nyumba zake zote? au Hakimu katishishiwa kibarua chake ndo maana akatoa kibali cha kukamatwa
 
Wamtafute pia kwenye Hotel ambazo warembo wanapenda kutembelea na kukaa humo inawezekana kwa kuwa amekaa sana sero alimisi sana na hivyo anajaribu kufanya Compensation .....
 
Mimi nahisi hata wakienda kuhakiki thamani ya nyumba aliyoiweka kama dhamana watagundua kuwa haifiki Mil 800 kama ilivyo kwenye hati. Liyumba sio mtoto mdogo na pia ni msomi. Alijua itafika siku atatakiwa mahakamani, labda hakuamini kuwa walio nae wangeachia hali hiyo iwe hivyo. Maana hata baadhi ya washitakiwa wa EPA waliwahi kuhakikishiwa kuwa mambo yasingefika Mahakamani, hadi walipojikuta wanasomewa mashitaka.

Naamini atakuwa alinunua nyumba (yenye thamani ndogo), akaitengeneza vizuri tu na kuiandaa kwa ajili ya udhamini utakapohitajika. Kama aliweza kuweka dhamana ya kuku na mbuzi, atashindwa vipi kujiandaa kwa hilo?
 
Yaani huyu hakimu ni mpumbavu wa kutupwa. Kulikuwa hakuna sababu zozote za liumba kutoka mahabusu, zaidi kulikuwa na sababu nyingi sana huyu bwana kuendelea kusota rumande

KWANZA KABISA mali alizowasilisha zilikuwa hazieleki kabisa, tena unaambiwa mpaka kuku walikuwa sehemu ya mali, kitu ambacho kingezidi kumtia wasiwasi huyu hakimu kama sio upofu wake uliosababishwa na nguvu ya hongo.

sasa angalia mazingaombwe kwenye passpot, mda wake ulikuwa unaisha february 2007, kitu kinachoonyesha kwamba, hakupeleka passport yake kabisa, kwa sababu passopt sasa hivi zinaisha 2015 kwani zile za mwanzo tulibadilisha 2005 kama mtakumbuka.

kwa hiyo huyu hakimu kwa kweli, labda kama alishinikizwa na jk au ni upofu wake uliotokana na rushwa, vinginevyo kichwa cheke hakikuwa kizuri kabisa.

hakuna valid passpot inayoisha kabla ya 2015 baada ya kubadilishwa mwaka 2005.
 
duh! kweli nchi hii ni kiboko. it looks like you can buy your way out of any shit that you get yourself into...
 
Hakimu khadija kama itathibitishwa aliruhusu Liumba kutoka selo bila kutimiza masharti ya dhamana ni lazima aadabishwe. Kusema kwamba labda alikuwa ameshinikizwa na mabosi isiwe sababu ya kuonewa huruma. Huyu Hakimu aliapa wakati anaajiriwa kwamba ataweka maslahi ya taifa mbele. Kama aliona kuna msukomo kutoka juu ili apindishe mambo basi ingefaa aachie ngazi au ajitoe kwenye hiyo kesi.

Tanzania tumefika hapa tulipo kutokana na uwoga wetu. Watu wako BoT wanaona mambo ya ajabu yanayopelekea hili taifa kusambaratika wananyamaza, kimya! Wanaogopa. Watu wanaogopa mabosi wao kama vile ni wala watu. Mtu akiwa na pesa tunamwogopa tunamtetemekea. Anafanya anachotaka tunanyamaza kimya. Kila mtu analinda ka-mkate chake anaogopa akipiga kelele kanaweza kakachafuliwa. Inafika mahali tuige mfano wa dk Slaa. Mbona yeye amepiga kelele na amewapigia kelele wale tuliokuwa tunasema ni untouchables lakini anadunda mpaka leo. Believe it hao wanamtandao tunaowaogopa ni waoga kuliko hata sisi. Ukionyesha jeuri ukapiga makelele hadharani wanapigwa butwa wanafyata wanakuwa wadogo.
 
Mahakimu wengi hawapendi kujisomea hata kuangalia hata movies za kisheria walau wapate cha kujifunza ktk maamuzi yao mahali pa kazi, huyu mama hana mume wala mtoto, hivyo hana hata wa kumshauri tu kiubinadamu. Kuna ka series fulani multchoice kanaitwa boston legal pale unawaona akina allen na dan crane wakitunishana misuli na majaji/mahakimu kimaigizo but kuna some practisable fact ktk mienendo ya kesi, pccb wame raise figure ile as ndio yote imeliwa na hakimu hajitumi kui study ili ajue kama washitaki wameshafanya homework yao vizuri yeye anakomalia 50bil kama dhamana, nadhani hii ilikuwa ni dhamana ghari kuliko yote ktk nchi yetu, hata kama sheria inaruhusu lakini mh.hakimu anapaswa atambue kuwa twin towers ziko pale tayari ni mali ya nchi na siyo liyumba hivyo alipaswa ku seek maelezo toka kwa pccb ktk exactly amount imekuwa swallowed na al, au asimamishe kusikiliza maombi ya dhamana na kuomba muongozo wa jambo hili kwa mkuu wake jaji wa kanda, huko wangeliangalia hilo kwa usaidizi wa dpp na pccb na charge sheet ingeletwa ikiwa ina sura inayofanana na ukweli, mh.hakimu alifurahia kuingia ktk rekodi mpya ya dhamana bila kutafakari gharama za rekodi hiyo in future, huo ni uzembe na kiburi cha ujuaji.

Upande wa pili ni mawakili prof. Mgongo fimbo na timu yake nao wamemfikisha ametus liyumba hapo un reasonably, hawakua act professionally kumsaidia mteja wao bali waling'ang'ania ubabe na kujulikana wakati walichohitaji ni hekima na tafakuri nzito ya kisheria pale mnapoingia ktk rekodi mpya bail kwa mteja.

Tuombe mungu jambo hili liende salama ila ninakiri kuwa alichosema mwanakijiji kina 50% ukweli, hakuwa na nia ya kutoroka bali kujidhuru na ndio maana kuna uwezekano mkubwa leo akaletwa tena mahakamani kama jaribio la jana waungwana waliweza kumtuliza na kumwelesha.

Bi hadija alipaswa ku seek technical advise toka jaji wake incharge baada ya kugundua makosa aliyoyafanya, hakufanya siku hiyohiyo, aliondoka zake na kuzima simu mpaka media ilipomuandama na mahakama kuu nayo kuliona hilo haraka, next day akatoa arrest warranty na ku detain wadhamini, tukiri tu kuwa amechemsha sana na wala wanasiasa wasiingizwe hapo.
 
Watanzania tunaingizwa tena mkenge. Haya mambo yanakuwa kama sinema itakuwaje apotee kiaina na pasipoti aliotoa imekwisha muda wake nk. Je hizi sio fix ili aachiliwe? Leo Ijumaa anatakiwa kuripoti Polisi hivyo wamsubiri huko kama atatokea. Jamaa alikuwa na nyumba ndogo kadhaa hapa mjini nahisi anakula vyake somewhere. Lets wait and see.
 
Watu mna wasiwasi sana. Liyumba haendi kokote na kizimbani atasimama si masaa mengi yajayo. Kumekuwepo na massive manhunt na vyanzo vya uhakika vinadokeza jamaa atakuwa amedakwa usiku huu kama mtego walioutega utafanikiwa kwani intel yote ilikuwa inaonesha jamaa yupo bado Dar! So.. subirini mahakamani leo... maana wakimkosa leo basi ndiyo watafute shimo kama la Sadam au waende kwenye mapango ya Tora Bora!


Nahofia maisha yake...Polisi wanatakiwa wamtafute, wakimpata wahakikishe usalama wake.
 
Bi hadija alipaswa ku seek technical advise toka jaji wake incharge baada ya kugundua makosa aliyoyafanya, hakufanya siku hiyohiyo, aliondoka zake na kuzima simu mpaka media ilipomuandama na mahakama kuu nayo kuliona hilo haraka, next day akatoa arrest warranty na ku detain wadhamini, tukiri tu kuwa amechemsha sana na wala wanasiasa wasiingizwe hapo.

Mkuu, Bi Khadija alishalamba chake, huo ushauri angeufanyia nini tena maskini ya Mungu!!!!!
 
Liumba ni core center ya saga zima la BoT, ukiweka ndani Liumba umewaacha uchi mafisadi wengi tuu. So, who knows labda Liumba katekwa in the form of Mafia style? Hahahahaha, haya ni mambo ya kawaida kabisa kwenye panzi scum....Yaani saga la BoT ni kama DeJa Vu, Balali alikwenda kutubiwa mara akafa mara mazishi private, tukaenda jeneza halikufunguliwa..... Ken Lay style baby.

Sasa kuhusu Liumba goodluck na kumsaka... Yaani hapo ndio utajua kwamba Legal system doesnt work all the time... Na system ya usalama ya Tanzania ilivyokuwa mbovu, Liumba anaweza kuwa kwa kimada wake hapo hapo Kigogo dar na msimkate.
 
Pamoja na kashfa ya wivi wa mamilioni, Liumba kuwa mtaani anazidi kueneza lile gonjwa maana dada zetu nao ni kama vipofu kwa wenye pesa. Akipatikana aishi rumande maisha yote........
 
Liumba ni core center ya saga zima la BoT, ukiweka ndani Liumba umewaacha uchi mafisadi wengi tuu. So, who knows labda Liumba katekwa in the form of Mafia style? Hahahahaha, haya ni mambo ya kawaida kabisa kwenye panzi scum....Yaani saga la BoT ni kama DeJa Vu, Balali alikwenda kutubiwa mara akafa mara mazishi private, tukaenda jeneza halikufunguliwa..... Ken Lay style baby.

Sasa kuhusu Liumba goodluck na kumsaka... Yaani hapo ndio utajua kwamba Legal system doesnt work all the time... Na system ya usalama ya Tanzania ilivyokuwa mbovu, Liumba anaweza kuwa kwa kimada wake hapo hapo Kigogo dar na msimkate.
l

issue ya kutekwa inawezekana, lakini tuangalie mchakato mzima wa kesi na mazingira ya dhamana, kwa hiyo ukichunguza sana kama ni umafia basi umeanzia mahakamani, kwa sababu Liyumba hakuwa na vigezo vya kupata dhamana
 
Jamaa kapeleka passport ya zamani ambayo ilishabadilishwa na kubaki new passport. Bi Khadija na wenzake hawakuliona hilo sababu ya rushwa iliyoshatembezwa wakawa vipofu
 
... Liumba kuwa mtaani anazidi kueneza lile gonjwa maana dada zetu nao ni kama vipofu kwa wenye pesa. Akipatikana aishi rumande maisha yote........

...upofu sawa, basi na uziwi pia? ...

Hivi kweli kuna watu humu mnaamini 'katoroka'?...

...Pheewww, no wonder kuna walioamini Mh.Chenge alikuwa
analichawia bunge, kama wale walioamini Mar.Wangwe aliuwawa
kabla ya ajali... au Mar.Daudi Balali aliji...
 
Wakuu..

What is up so far? AL ameshapatikana au la? Au hatafutwi altogether?!

Wenye latest please tubandikie...
 
Mi nahisi kuna kupika maneno hapa. Mara nyingi tunatia chumvi mno kabla jambo halijafahamika kwa undani. Jamaa kauliza source. mara nyingine misimamo yetu inatoa fursa ya watuhumiwa kujipanga na kuficha ushahidi na kutambua mashahidi pia. Tuache wahusika watoe taarifa ndio tutajua wapi pa kuanzia
 
kimtazamo ni hivyo,lkn kumbuka tayari ana kashfa nyingi mtaani zina muandama,hivyo sio jambo la kushangaza.ila watampata tuuu
 
hivyo ni sawa kabisa,unajuwa tatizi la watanzania tunapenda kujadili mambo yanayo zidi vichwa vyetu.tayari PCCB wapo kazi,na si dhani kama interpol watalala,huyu liyumba yupo humu hum tanzania
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom