KESI YA MAUAJI: Utetezi wa Elizabeth Michael (Lulu) ndani ya mahakama kuu

KESI YA MAUAJI: Utetezi wa Elizabeth Michael (Lulu) ndani ya mahakama kuu

Nakupata mkuu.

Ila nadhani kwenye hili hakimu hakua nje ya mipaka ili kuweka kesi sawa sawa maana umri wa Lulu ulikua na mashaka kipindi kile cha kifo cha Kanumba.

Nadhani pia hata kwenye utetezi wake Lulu kuna sehemu atakua kazungumzia umri wake kipindi hicho au kwenye maelezo ya awali kutakua na sehemu ya umri wake wakati kitendo hicho kinatokea.

Niliona jana mahala pia kua alieleza kua alienda kwa Kanumba na gari, hivyo unaona ni mambo yanayohusiana na tukio. Maana lazima uulizwe ulifikaje kwa jamaa, akasema alienda akiwa anaendesha gari, hapo akazua jambo lingine.

Ndio maana hakimu ametaka kuweka kumbukumbu sawa, kama lienda na gari anaendesha, je alikua na leseni, je aliipataje kama alikua chini ya miaka 18, alidanganya polisi, kama alidanganya atakua kadanganya mangapi?

Lulu akikutana na mwanasheria mzuri wa cross examination hachomoki, aombe wamuwekee wanasheria mazwazwa.
Mwanasheria wa utetezi kama anajua utetezi anaweza kukubali kwamba Lulu aliendesha bila leseni au alikuw ana leseni ya mazabe (kama kweli ilikuwa hivyo) kwa sababu ni bora kuwa na kesi ya kuendesha bila leseni kuliko kesi ya mauaji.
 
Hawezi kufungwa huyo, atahukumiwa kwenda jela miaka kadhaa au kutoa fidia ya hela kiasi flani, kesi inaishia hapo........
Ikitokea ni kifungo au faini, i guess atatoka kwasababu majjizo ana hela mingi, hvy atamlipia.
 
Sioni uhusiano wa Lulu kujichanganya kuhusu leseni ya kuendesha gari na kifo cha Kanumba.

Sioni ni kivipi kujichanganya huko kuhusu leseni kutaathiri matokeo ya hiyo kesi.
Mkuu, lazima waestablish mazingira kabla ya tukio. Hivyo lazima aulizwe mazingira ya awali kabla ya tukio, kama kuonana na marehemu, milonana wapi, mlikutana vipi, ilikua sehemu gani nk nk.

Hivyo katika maelezo hayo Lulu atakua amesema labda aliitwa na marehemu au alipugiwa simu na marehemu aende kwake. Ataulizwa, aliendaje, kwa miguu au boda boda au taxi au daladala, akisema taxi, ataulizwa anamkumbuka dereva aliempeleka au hamkumbuki, je huyo dereva alimfaham kabla au alimuona siku hiyo.

Sasa yeye alisema alienda na gari yake akiwa anaendesha, hapo akazua jambo jipya, je alikua na leseni, je leseni aliiapata kiuhalali, alipataje leseni huku alikua na umri wa chini ya miaka 17 au alidanganya polisi ili apewe leseni, kudanganya polisi ni kosa kisheria.

Hayo maswali na mengine mengi yanahusiana kabosa na kesi hiyo ya Lulu.
 
Hilo swali sioni umuhimu wala uhusiano wake na kesi.

Kwanza sidhani kama ni swali sahihi kwa jaji kuuliza. Labda kama lingeulizwa na upande wa mashitaka.

Ni swali lililo prejudicial!
 
Mwanasheria wa utetezi kama anajuautetezianaweza kukubali kwamba Lulu aliendesha bila leseniaualikuw ana leseni ya mazabe (kama kweli ilikuwa hivyo) kwa sababu ni bora kuwa na kesi ya kuendesha bila leseni kuliko kesi ya mauaji.
Hahaaaa, kweli, bora kesi ya kuendesha gari bila leseni kuliko ga mauaji.

Hii kesi ili itamgharimu sana Lulu, lazima apate wanasheria wazuri na wenye uzoefu ili wamchomoe, hao wanahitaji mpunga mrefu sana.
 
japo wananchi wenzangu mnashangilia huyu binti kufungwa, me niko against na nyie, ingawa hata sio fan wake,lakini namhurumia sana,jela sio sehemu nzuri kabisa,mimi niliwahi kukaa lock up masaa kadhaa tu,mpaka leo nina adabu zote...tuombe Mungu tu mahakama ionyeshe huruma zake tuendelee kuwa nae uraiani..maana kesi yenyewe imemkalia vibaya,halafu marafiki zake nao ni kama wamemtenga vile..dah!namhurumia sana kiukweli
 
alivaa taulo huenda alotoka bafuni miguu majimaji na ile kikimbiza ili hali ulo na nyege aisee utapiga mweleka na kuamkia ahera soku ya kiama kama alivyofanya marehemu bado anaserereka huko ahera akisubiri parapanda!
Umenichekesha sana mkuu...
 
Binti hana makosa,itakuwa kanumba pombe ilikuwa inamshinda na ndo ilimfanya ale mweleka mkali bila hata kupata akili ya kuokoa kichwa kisigote sakafu wakati anadondoka
 
Hapana, hakimu anaweza kumuuliza mtu swali lolote na wakati wowote, hakimu anaweza kukataa swali au akamodify swali wakati wowote.

Mambo ya kisheria ya ajabu sana mkuu. Hapo hakimu hajatenda kosa lolote, sema ndio hivyo ameuliza swali litakalowapa waendesha mashitaka red light ili wao nao wapuge hapo hapo kummaliza kabisa.

Ukijichanganya tu kwenye cross examination, maelezo yako yote uliyotoa yanaweza kua discredited na ukajikuta kwenye matatizo hasa kama wewe ndie mwenye kesi, ikiwa ni shahidi basi ushahidi wake unatupiliwa mbali kabisa.

Natamani hata nikapate ka certificate ka sheria aisee. Sheria tam sana.
Mkuu njoo,mi napiga llb open mwaka wa pili
 
Seth anatakiwa akamatwe kwa kuacha uovu wa kanumba kutembea na under 18..!
 
Aiseee Mungu amsaidie, yaaan mi niliumia tuuu niliposikia Kanumba mbaba mzima anatembea na hako katoto
 
Nakupata mkuu.

Ila nadhani kwenye hili hakimu hakua nje ya mipaka ili kuweka kesi sawa sawa maana umri wa Lulu ulikua na mashaka kipindi kile cha kifo cha Kanumba.

Nadhani pia hata kwenye utetezi wake Lulu kuna sehemu atakua kazungumzia umri wake kipindi hicho au kwenye maelezo ya awali kutakua na sehemu ya umri wake wakati kitendo hicho kinatokea.

Niliona jana mahala pia kua alieleza kua alienda kwa Kanumba na gari, hivyo unaona ni mambo yanayohusiana na tukio. Maana lazima uulizwe ulifikaje kwa jamaa, akasema alienda akiwa anaendesha gari, hapo akazua jambo lingine.

Ndio maana hakimu ametaka kuweka kumbukumbu sawa, kama lienda na gari anaendesha, je alikua na leseni, je aliipataje kama alikua chini ya miaka 18, alidanganya polisi, kama alidanganya atakua kadanganya mangapi?

Lulu akikutana na mwanasheria mzuri wa cross examination hachomoki, aombe wamuwekee wanasheria mazwazwa.
Learned brodas n sisters hakuna zwazwa mkuu
 
Back
Top Bottom