Kesi ya Mbowe: Kibatala na Mallya wameiondolea Mahakama uwezo wa kumfunga Mbowe hata ikishinikizwa

Kesi ya Mbowe: Kibatala na Mallya wameiondolea Mahakama uwezo wa kumfunga Mbowe hata ikishinikizwa

Amedanganywa nini mzee? kwamba wewe unajua mambo yote yanayotendeka hapa nchini? una tiss? una polisi? una vyombo vya uchunguzi?

Utasemaje waongo wakati wewe mwenyewe hapo ulipo upo kiganjani mwa vyombo hivyo vinavyojua unaishije na unatakiwa kuishije kila siku? usilolijua ni kama usiku wa giza.
Huu ni ujinga na upotoshaji,Rais kadanganywa maana Mbowe hana record yoyote ya uhalifu wala hajawahi kukutwa na hatia na mahakama yoyote Tanzania,hauhitaji Tiss kujua hili..ni akili tu.

Maisha ya mtu na kila kitu chake Mungu ndie anashikilia...Kama wewe maisha yako yapo mikononi kwa TISS na vyombo vya usalama,una matatizo kichwani...kifo cha Magu akijakufunza bado!
 
Wakati mwingine nikisikia watu wasio wanasheria wanavyojadili mambo ya kisheria huwa nawaonea huruma sana kwasababu it will take them 100 years to know the truth. hapo hakuna wanasheria, tafuteni wengine, fuateni ushauri huu mtakuja kunishukuru.

Hao sio criminal lawyers, kuna mawakili wa jinai wazuri na wanajua techniques kuliko hao, wao faida yao ni kwamba wanajipublicise na kupata wateja na kujulikana zaidi nchini ila sio kuwasaidia kwenye hiyo kesi.
Acha kuwaonea wivu Kina Kibatala.
Wako vizuri kushinda Mawakili wengi sana ndani ya Tanzania
 
Jana tumesikia polisi akitoa ushahidi wake kwenye kesi ya Mbowe. Tumesikia na siyo mara ya kwanza wakijitetea kwamba maelezo waliyoandika wamejisahau wakakosea yaani "typographical error".

Je, sheria na mahakama zinasema kuhusu hiki kinachoitwa "typographical error"?

Ukweli ni kwamba mtu unaweza kukosea kuandika kitu tofauti na ulivyotarajia. Ila wakati wa kusahihisha "typographical error"? jaji hajaanza kusikiliza kesi.

Bahati nzuri kesi hii imeenda hivyo upande wa akina Mbowe. Kama mnakumbuka wiki mbili zilizopita akina Kibatala, Mallya na wenzao waliomba kuwe na kesi ndogo yaani "trial within trial".

Msingi wa kesi ile ndogo ilikuwa maandishi au maelezo ya mtuhumiwa mmoja yasipokelewe kama ushahidi. Sasa hivi kidogokidogo tutaanza kuona akina Kibatala, Mallya walitumia akili ya ziada ambayo wote hatukuiona.

Pamoja na polisi kuendeshwa sana kwenye ile kesi ndogo hadi nchi nzima tukajua PGO polisi hawajui PGO bado ilikuwa ni vigumu kina Kibatala kushinda. Naamini hata akina Kibatala walijua wasingeshinda lakini kuna kitu walikuwa wanakiweka

Kwa nini hawakushinda na walijua hawatashinda? Hoja pale si polisi kuijua au kutoijuaPGO . Hoja kubwa pale ilikuwa kwamba kama mtuhumiwa aliandika maelezo kwa hiari yake au aliteswa ndipo akalazimishwa kuyaandika baada ya mateso.

Maadam mtuhumiwa alikiri kwamba ameandika lakini kwa mateso jaji hakuwa na namna ila kuitupilia mbali kesi ile. Ni vigumu kwa jaji au mtu yeyote kuthibitisha kwamba mtuhumiwa aliteswa ndipo akaandika maelezo.

Hapa msingi ni uleule kwamba huwezi kuandika maelezo halafu mbele ya jaji uyaruke kwa kisingizo cha "typographical error" au cha kuteswa kabla ya kuyaandika.

Hivyo, polisi, serikali na mahakama hawakujua wanachokitaka akina Kibatala na kimsingi walitaka ile hukumu ije vilevile kama ilivyokuja, yaani washindwe. Na akina Kibatalla walishindwa kama walivyotaka.

Sasa kushindwa kwa akina Kibatala kuna msaada gani kwako?

Ukiangalia kesi inavyokwenda sasa ndiyo utajua kwa nini walitaka washindwe kesi.

Hebu angalia wanachokifanya sasa hivi. Huwasikii tena wakiuliza maswali ya PGO. Wanajikita sana kushambulia ushahidi wa polisi unaoletwa mahakamani.

Wanasoma maelezo ya shahidi wa serikali aliyoyaandika kisha wanalinganisha na anachosema mahakamani. Kwa kufanya hivyo wamefaulu kukuta ujinga mwingi kwenye ushahidi wa polisi na mashahidi wote wanaoletwa na serikali

Mwisho wa siku ni kwamba kila polisi (shahidi) mmesikia akisema "hapo nilikosea kiandika" au wakisema hilo kosa ni "typographical error" kama alivyosema wa jana.

Hii maana yake akina Kibatala, Mallya na wenzao wameshafaulu kuiweka mahakamani katika kitanzi. Maana yake ushahidi wote wa maandishi jaji sasa hana mamalaka ya kuukataa. Hana mamlaka ya kuona kwamba hiyo ni "typographical error".

Mahakama hiyohiyo ilikataa mtuhumiwa kubadili ushahidi wake kwa kisingizo cha kuteswa hivyo ushahidi huo utaingia mahakamani.

Sasa polisi nao ushahidi wao hautaruhusiwa kubadilishwa. Alichoandika mtuhumiwa kitahesabika kama ushahidi na alichoandika polisi kitatumika kwenye hukumu. Hapa akina Kibatala wamecheza kama Pele na ilikuwa vigumu kugundua.

Kimsingi kama mahakama ilinuia kumfunga Mbowe kwa mbinu hii ya kina Kibatala imewashinda na inawezekana serikali inaweza isilete mshahidi wengi kama tulivyodhani

Vilevile mojawapo ya kesi muhimu kwa kesi hii ni ile ya Mahakama ya Rufani ya "Harish Ambaram Jina (By His Attorney Ajar Patel) v. Abdulrazak Jussa Suleiman".

Katika kesi hii mahakama iligundua tatizo kwenye malezo ya Patel yeye akajitetea kwamba alikosea kuandika yaani "typographical error".

Mahakama ya Rufani ikakataa utetezi huo ikamwambia "kama ulikosea kuandika "typographical error" basi ulitakiwa kurekebisha kabla ya siku ya kusikilizwa kesi". Kipindi cha jaji kusikiliza kesi siyo cha kurekebisha document.

Hivyo, akina KIbatala, Mallya naamini kesi hii wanaijua lakini kama hawaikumbuki basi iko kwenye ukurasa wa 134 wa ripoti za kesi Tanzania za mwaka 2004 yaani [2004] T.L.R. 134.

Wasalaam
Huku kujilisha upepo hamjaaacha tu? Hivi kwa nini mnadhani wote waliomo humu ni wapuuzi kama ninyi? Acheni hizo bwana. Kesho na keshokutwa mtakuja tena hapa kuanza lalamika kuwa haki haikatendekea sababu ya mambo haya ha kipuuzi.
 
Hujui na hufuatilii kinachondelea mahakamani, je neno terrorist na terrorism yalianzia hapo mahakamani au kwenye ripoti ya polisi. Kama ni kwenye ripoti. Je yalitakiwa yawepo au, kumbuka umesema ripoti ilikuwa ya kiswahili, lengo la mawakili ni kulinganisha kama Shahidi ndiye aliandika ripoti hiyo kutokana na maelezo ya mdomo
uyu jamaa atakua kasoma kajisehemu tuu ka hii kesi, then akakimbilia ku comment..

Yani kabisa shahidi anasema imeandikwa Kingereza, yeye anatwambia ni kiswahili.
 
Hayo hapo juu yanaathiri nini ushahidi wa prosecution hasa ikizingatiwa shahidi hajui kiingereza, ameulizwa kwa kiswahili, maelezo yaliandikwa kwa kiswahili, na wapo mashahidi wengine wanatarajiwa kuitwa pengine kana kwamba ushahidi wa mtu mmoja tu huyo hata ukiwekwa pembeni utaangaliwa ushahidi wa wengine?

Kujua kiswahili cha terrorist/terrorism au kutojua kunafifisha charge aliyosomewa? wakati pengine ameshaeleza maelezo ya nini maana ya ugaidi?.....je? wamejua nini lengo la prosecution kumwita shahidi huyo?

Kwamba walimwita kuja kuthibitisha nini among others kwasababu kuna wakati prosecution wanaweza kuita shahidi kuja kuthibitisha kitu kimoja tu miongoni mwa vingi na vingine vitathibitishwa na mashahidi wengine na akishathibitisha kile wanachokitaka tu wanakuacha tu wewe uulize maana za terrorism na matakataka yako yoote na kesi yao inabaki imesimama.

Ndio maigizo wanayoyafanya hao mawakili wenu. kwa bahati nzuri nilishawahi kuwa prosecutor na ninawaonea huruma chadema kwasababu kwa wanachokifanya mawakili wenu mtakuja kulia

Kwanza ile kesi sio ya CHADEMA ni ya mbowe na wenzake. Hivyo usiwasikitikie CHADEMA msikitie mbowe. Pili, kazi ya cross examination ni kushake credibility ya shahidi, je shahidi anafahamu anachokisema au la. Sasa shahidi ameulizwa maswali mengi tu ameshindwa kujibu, Hilo limedicredit.
 
Wakati mwingine nikisikia watu wasio wanasheria wanavyojadili mambo ya kisheria huwa nawaonea huruma sana kwasababu it will take them 100 years to know the truth. hapo hakuna wanasheria, tafuteni wengine, fuateni ushauri huu mtakuja kunishukuru.

Hao sio criminal lawyers, kuna mawakili wa jinai wazuri na wanajua techniques kuliko hao, wao faida yao ni kwamba wanajipublicise na kupata wateja na kujulikana zaidi nchini ila sio kuwasaidia kwenye hiyo kesi.
Sheria ni kwa ajili ya watu ndiyo maana ikiwezekana tunaendesha kesi zetu pro se.
 
Huku kujilisha upepo hamjaaacha tu? Hivi kwa nini mnadhani wote waliomo humu ni wapuuzi kama ninyi? Acheni hizo bwana. Kesho na keshokutwa mtakuja tena hapa kuanza lalamika kuwa haki haikatendekea sababu ya mambo haya ha kipuuzi.
Sio kosa kulalamika haki isiopotendeka. Maana mahakama na haki kwa Tanzania ni vitu viwili tofauti. Rejea kesi ya Lema Arusha alikaa miezi sita rumande mpaka mahakama kuu ilovyobatilisha maamuzi akapewa dhamana. Mahakama zisipotenda haki ziambiwe.
 
Inaathiri nini kwenye ushahidi wa prosecution, si umebaki umesimama? shauri yenu.
Shauri yako Kama hujui Nini kimeadhirika. Wewe ni mtaalamu wa silaha hujui maana ya terrorism na umeandika mwenyewe kwenye fomu. Sasa Kama Neno la kwenye fomu uliyojaza mwenyewe hujui, je yale unayosema tuna uhakika gani unaajua.
 
Hawatakuewa hapa,wewe wape muda tu watarudi tena hapa kupiga mayowe mwisho wa kesi.Kwa sasa kila mtu hapa anajiona ni nguli wa kuchambua kinachoendelea Mahakamani,

Kwamba ushindi kwao ni kutoa update hapa mitandaoni,umewashauri vizuri sana swala la kutafuta Wanasheria nguli wa kesi za jinai,lakini hawatakuelewa,wao kwao Kibatala ndiyo kila kitu,wanamuona mbobezi kwenye nyanja zote za kisheria.
Tatizo mnadharau watanzania wenzenu kisa sio wa chama chenu. Kuna wanasheria gani nguli wa jinai??. Mawakili wanachofanya ni cross examination ili kushake credibility ya ushahidi na wanafanya kazi yao vizuri. Maana mwenye mzigo was kudhibitisha ukweli was mashtaka ni jamhuri kupitia mawakili wake. Sio kina kibatala
 
Wakati mwingine nikisikia watu wasio wanasheria wanavyojadili mambo ya kisheria huwa nawaonea huruma sana kwasababu it will take them 100 years to know the truth. hapo hakuna wanasheria, tafuteni wengine, fuateni ushauri huu mtakuja kunishukuru.

Hao sio criminal lawyers, kuna mawakili wa jinai wazuri na wanajua techniques kuliko hao, wao faida yao ni kwamba wanajipublicise na kupata wateja na kujulikana zaidi nchini ila sio kuwasaidia kwenye hiyo kesi.

Fala kweli wewe kuna fact za kisheria hata engineer anaelewa
 
Hayo ni maneno ya Div. IV ya 32 Simon Zero!

Watu na akili zao hawawezi kuamini binadamu mwenzao kuwa malaika, labda watu kama Kabudi aliyeamini dikteta Magufuli kuwa ni mungu!
Ila Mbowe alitaga yaani alikula DIV 0 Ihungo🤣
 
Najua sababu za kuachiwa na mahakama kuu ni kwamba hawakusomewa preliminary hearing kwenye kesi ya awali yani Trial. Ndio ujue mahakama zetu siyo conclusive.
 
Hayo hapo juu yanaathiri nini ushahidi wa prosecution hasa ikizingatiwa shahidi hajui kiingereza, ameulizwa kwa kiswahili, maelezo yaliandikwa kwa kiswahili, na wapo mashahidi wengine wanatarajiwa kuitwa pengine kana kwamba ushahidi wa mtu mmoja tu huyo hata ukiwekwa pembeni utaangaliwa ushahidi wa wengine?

Kujua kiswahili cha terrorist/terrorism au kutojua kunafifisha charge aliyosomewa? wakati pengine ameshaeleza maelezo ya nini maana ya ugaidi?.....je? wamejua nini lengo la prosecution kumwita shahidi huyo?

Kwamba walimwita kuja kuthibitisha nini among others kwasababu kuna wakati prosecution wanaweza kuita shahidi kuja kuthibitisha kitu kimoja tu miongoni mwa vingi na vingine vitathibitishwa na mashahidi wengine na akishathibitisha kile wanachokitaka tu wanakuacha tu wewe uulize maana za terrorism na matakataka yako yoote na kesi yao inabaki imesimama.

Ndio maigizo wanayoyafanya hao mawakili wenu. kwa bahati nzuri nilishawahi kuwa prosecutor na ninawaonea huruma chadema kwasababu kwa wanachokifanya mawakili wenu mtakuja kulia.
kama wewe ndio uliwahi kuwa prosecutor..God help us!
 
Mkuu 'Kisanduku', umejizungushazungusha sana bure tu!

Sioni uhusiano juu ya 'kesi ndogo', na haya ya 'typo' yaliyomo kwenye kesi yenyewe. Umejitahidi sana kuonyesha uwepo wa mfanano, lakini ni kama mfanano huo unaulazimisha tu uwepo.

Hukumu ya kesi ndogo, unaeleza kwamba akina Kibatala walishindwa! Kwa utaalam wako, kweli unaona kwamba kesi ile walishindwa? Maelezo ya Jaji uliyasikia na ukaridhika na sheria alizotumia kuamua hiyo kesi?

Inaonekana kama wewe ni msomi wa sheria, lakini ulivyoiweka hii mada, inashusha hadhi ya elimu uliyo nayo kwenye taaluma hiyo. Au pengine bado ni mwanafunzi?
 
Back
Top Bottom