- Thread starter
- #161
Hii ni forum ya maelezo, toa maelezo.
Mkuu 'Kisanduku', umejizungushazungusha sana bure tu!
Sioni uhusiano juu ya 'kesi ndogo', na haya ya 'typo' yaliyomo kwenye kesi yenyewe. Umejitahidi sana kuonyesha uwepo wa mfanano, lakini ni kama mfanano huo unaulazimisha tu uwepo.
Hukumu ya kesi ndogo, unaeleza kwamba akina Kibatala walishindwa! Kwa utaalam wako, kweli unaona kwamba kesi ile walishindwa? Maelezo ya Jaji uliyasikia na ukaridhika na sheria alizotumia kuamua hiyo kesi?
Inaonekana kama wewe ni msomi wa sheria, lakini ulivyoiweka hii mada, inashusha hadhi ya elimu uliyo nayo kwenye taaluma hiyo. Au pengine bado ni mwanafunzi?