Kesi ya Mbowe: Kibatala na Mallya wameiondolea Mahakama uwezo wa kumfunga Mbowe hata ikishinikizwa

Huu ni ujinga na upotoshaji,Rais kadanganywa maana Mbowe hana record yoyote ya uhalifu wala hajawahi kukutwa na hatia na mahakama yoyote Tanzania,hauhitaji Tiss kujua hili..ni akili tu.

Maisha ya mtu na kila kitu chake Mungu ndie anashikilia...Kama wewe maisha yako yapo mikononi kwa TISS na vyombo vya usalama,una matatizo kichwani...kifo cha Magu akijakufunza bado!
 
Acha kuwaonea wivu Kina Kibatala.
Wako vizuri kushinda Mawakili wengi sana ndani ya Tanzania
 
Huku kujilisha upepo hamjaaacha tu? Hivi kwa nini mnadhani wote waliomo humu ni wapuuzi kama ninyi? Acheni hizo bwana. Kesho na keshokutwa mtakuja tena hapa kuanza lalamika kuwa haki haikatendekea sababu ya mambo haya ha kipuuzi.
 
uyu jamaa atakua kasoma kajisehemu tuu ka hii kesi, then akakimbilia ku comment..

Yani kabisa shahidi anasema imeandikwa Kingereza, yeye anatwambia ni kiswahili.
 

Kwanza ile kesi sio ya CHADEMA ni ya mbowe na wenzake. Hivyo usiwasikitikie CHADEMA msikitie mbowe. Pili, kazi ya cross examination ni kushake credibility ya shahidi, je shahidi anafahamu anachokisema au la. Sasa shahidi ameulizwa maswali mengi tu ameshindwa kujibu, Hilo limedicredit.
 
Sheria ni kwa ajili ya watu ndiyo maana ikiwezekana tunaendesha kesi zetu pro se.
 
Huku kujilisha upepo hamjaaacha tu? Hivi kwa nini mnadhani wote waliomo humu ni wapuuzi kama ninyi? Acheni hizo bwana. Kesho na keshokutwa mtakuja tena hapa kuanza lalamika kuwa haki haikatendekea sababu ya mambo haya ha kipuuzi.
Sio kosa kulalamika haki isiopotendeka. Maana mahakama na haki kwa Tanzania ni vitu viwili tofauti. Rejea kesi ya Lema Arusha alikaa miezi sita rumande mpaka mahakama kuu ilovyobatilisha maamuzi akapewa dhamana. Mahakama zisipotenda haki ziambiwe.
 
Inaathiri nini kwenye ushahidi wa prosecution, si umebaki umesimama? shauri yenu.
Shauri yako Kama hujui Nini kimeadhirika. Wewe ni mtaalamu wa silaha hujui maana ya terrorism na umeandika mwenyewe kwenye fomu. Sasa Kama Neno la kwenye fomu uliyojaza mwenyewe hujui, je yale unayosema tuna uhakika gani unaajua.
 
Tatizo mnadharau watanzania wenzenu kisa sio wa chama chenu. Kuna wanasheria gani nguli wa jinai??. Mawakili wanachofanya ni cross examination ili kushake credibility ya ushahidi na wanafanya kazi yao vizuri. Maana mwenye mzigo was kudhibitisha ukweli was mashtaka ni jamhuri kupitia mawakili wake. Sio kina kibatala
 
Sugu alishinda kwenye Rufaa akaachiwa huru. Mahakama ilitoa hukumu isiyo haki.
unajua sababu ya kuachiwa kwa sugu? na ni sababu ambayo hadi kesi inaisha kibatala hakuwa anajua hoja hiyo ya msingi?
 

Fala kweli wewe kuna fact za kisheria hata engineer anaelewa
 
Hayo ni maneno ya Div. IV ya 32 Simon Zero!

Watu na akili zao hawawezi kuamini binadamu mwenzao kuwa malaika, labda watu kama Kabudi aliyeamini dikteta Magufuli kuwa ni mungu!
Ila Mbowe alitaga yaani alikula DIV 0 Ihungo🤣
 
Najua sababu za kuachiwa na mahakama kuu ni kwamba hawakusomewa preliminary hearing kwenye kesi ya awali yani Trial. Ndio ujue mahakama zetu siyo conclusive.
 
kama wewe ndio uliwahi kuwa prosecutor..God help us!
 
Mkuu 'Kisanduku', umejizungushazungusha sana bure tu!

Sioni uhusiano juu ya 'kesi ndogo', na haya ya 'typo' yaliyomo kwenye kesi yenyewe. Umejitahidi sana kuonyesha uwepo wa mfanano, lakini ni kama mfanano huo unaulazimisha tu uwepo.

Hukumu ya kesi ndogo, unaeleza kwamba akina Kibatala walishindwa! Kwa utaalam wako, kweli unaona kwamba kesi ile walishindwa? Maelezo ya Jaji uliyasikia na ukaridhika na sheria alizotumia kuamua hiyo kesi?

Inaonekana kama wewe ni msomi wa sheria, lakini ulivyoiweka hii mada, inashusha hadhi ya elimu uliyo nayo kwenye taaluma hiyo. Au pengine bado ni mwanafunzi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…