Kesi inayoendelea ya Mbowe hairipotiwi na chombo chochote Cha habari nchini na hakuna updates zinatolewa na vyombo vikubwa vya habari isipokuwa akaunti moja ya tweer inayoripoti na vyombo vingine kuchukua taarifa hapo nakuweka kwenye akaunti zao. Katika tasnia ya habari na kwa kuzingatia demokrasia hii Ni ishara ya wazi kwamba vyombo vyetu vya habari havina meno na Wala uongozi wao haupo kwa ajili yakuvisaidia.
Majirani zetu Kenya kesi zote hata zinqzomkabili Rais zinarushwa live ikiwemo TV ya Taifa, watu wanasikia na kuelewa kutoka kwenye midomo ya watuhumiwa,utetezi, serikali na Mahakama na hivyo kuweka usawa- na kuonyesha misingi ya haki.
Tanzania Kama mahakama imezuia waandishi wa habari wakati huo wanataka kuendesha kesi kigitali unajiuliza wanaficha Nini? Kwanini Bunge liruhusu vyombo vya habari, serikali iruhusu lakini chombo Cha haki Kama mahakama kizuie Uhuru wakupata habari? Kama mahakama imeshindwa kuheshimu Uhuru wa kupata habari wanawezaje kusimamia utendaji haki? Kama mahakama inapingana na vifungu vya sheria inawezaje kusimamia mfumo wa utoaji haki?
Hii nifedhea ambayo sijui inalenga Nini? Uwezi kuona vyombo vya habari vimezuiwa vya Nini Wakati watu binafsi wanarekodi na kuandika Kisha kurusha kwa jamii kile kinachoendelea mahakamani?