Na wamekwisha chemsha. Handling ya vidhibiti ilikuwa ya hovyo. Finger prints zingethibitisha kama mshitakiwa aliwahi kuishika na hata hizo kete alizifunga au alizihesabu! Sio rahisi sana kukuta muuza madawa ya kulevya sio mtumiaji pia, je kun maabara imethibitisha kuwa yale ni madawa ya kulevya? Inashangaza kila shahidi aliyekuwa kwenye upekuzi anasema “kete za madawa ya kulevya” walipaswa angalau kusema “kete zinazodhaniwa ni madawa ya kulevya”. Hawajui wakihojiwa kama kuna ripoti ya maabara na ikawa haipo basi hakuna uthibitisho ni madawa ya kulevya!? Polisi wanachukua risasi tatu kama kidhibiti lakini wanaleta moja eti mbili wamezitumia. Vipi kama mtuhumiwa angedaiwa kuwa na bastola tu - wapimaji wangeshindwa kuthibitisha kama ni nzima au la?? Polisi na kitengo chao wanakosaje risasi za 9mm kwa ajili ya majaribio??!! Ugaidi gani ww kulipua vituo vya mafuta mikoa minne kwa risasi 3 na bastola??
Bahati mbaya Polisi wameshathibitisha finger prints hazikuchukuliwa. Ukiweka na huu mkanganganyiko wa Luvern, Luger na CZ 100 na mwenzake A50… unakuta jaji anapata shida!!
Shahidi anailizwa kama ana record za sauti za mratibu anasema hapana. Alitoa taarifa za uhalifu uliopangwa kwa walengwa, usalama wa taifa, kamati za ulinzi husika? Hapana!!
Kama sio uzembe basi walikuwa wanajua kabisa jambo zima halipo na hili ni rahisi kuonesha kuliko eti kulikuwa na uhalifu unaenda kutendeka!!