Kesi ya Mbowe: Namba A5340 kwanini imekuwa issue kubwa?

Kesi ya Mbowe: Namba A5340 kwanini imekuwa issue kubwa?

Maana yake namba za usajili zilibadilishwa kukidhi nia ya kutenda uharifu bila ya kujulikana mmiliki halali ni yupi.

Serikali ndio msimamizi mkuu wa usajili wa silaha yoyote ya moto nchini Tanzania hivyo wanafahamu silaha ipi ilisajili lini wapi na mmilikishwaji ni nani kwahiyo hapo kuna mlengwa hatajwi tu kwa majina ila wanabishania utofauti wa namba kunusu au kusaidia ushahidi kumtia mtu mmowapo hatia kwamba aliruhusu silaha yake kutaka kutumika kinyume na sheria.
Kwenye hati ya mashitaka bunduki inasomeka kama Luvern.

Shahidi wa 3 yule wa Forensic alisema ni Luger. Ila kwenye statement yake alisema ni CZ100.

Shahidi Madembwe alisema ni Ruger.

Unaweza kuona huo mkanganyiko.
 
Ni kweli nami naamini jaji ameshaona jamhuri wamepeleka kitu cha hovyo mahakamani, lakini jaji huyo huyo ataamua kesi kwa kuwapa ushindi jamhuri huku akitabasamu, huyu tayari atakuwa ametimiza wajibu wake kwa mabosi wake na sio kwa taaluma yake kama kesi inavyotaka, wakati mwingine nawahurumia mawakili wa upande wa utetezi kwa akili kubwa wanayotumia kushindana na hawa wasanii na genge lao.
Wanaweza kufanya ktk kesi zingine, hii denooJ nasema na kukuhakikishia tena kuwa, Mbowe ni mtu huru, hakuna Jaji wa kumfunga kwa kesi isiyokuwa na facts...

Hata wao wako monitored. Yuko aliye mkuu, mwenye haki isiyotiliwa shaka aliye juu yao anawa - monitor step by step. HATA WAO WANAOGOPA KUFA broo...!!

Lenye possibility wa 50/50 ni hili.

Kuwa lengo kuu la hayawani hawa ni kumtesa na kumpotezea muda Mbowe. Kwa hiyo mkakati wao, ni kuhakikisha mahakama hii inamhukumu kifungo. Halafu mahakama ya rufani inakwenda kutengua hiyo hukumu..

Hili linawezekana. Lakini napo ni pagumu sana kwa kuzingatia mwenendo wa kesi hii yote hadi sasa...!
 
Kuna haja ya kuwa wanarekodi haya mahojiano aisee, kwanza teknolojia imekua sana na pia hii ingeondoa kabisa huu ubishi kwamba mimi nimesikia hivi wewe hujasikia..
Yako recorded yote ndugu kwa sauti na kwa maandishi pia...

Mahakamani hususani mahakama za juu, kumbukumbu ya kila hoja na matukio zinahifadhiwa kwa njia ya sauti (audio) na kwa njia ya maandishi (text) kama ilivyo bungeni ambako kila tendo na sauti ya kila mtu huhifadhiwa na ndiyo maana ya "Hansard"...
 
Hayo ni mambo ya technical sana kwenye sheria tulia mpira bado haujaisha,japokua hadi sasa naona upande wa serikikali umeelemewa upande wa kiungo na beki zimekatika.
hapo kuna sheria gani sasa?
 
Mkuu umebainisha mambo ya maana sana ambayo akina Kibatala wanarukaruka tu kama maharage ya wakimbizi kwenye sufuria jikoni
 
Yasemekana mshitakiwa #2 alikamatwa na bastola ambalo anakanusha.

Kwamba alikamatwa na bastola au hakukamatwa na bastola, hayo ni mambo mengine.

Kukamatwa na bunduki kinyume cha sheria mbona bado ni msala usio kuwa na kifani?

Kwanini upande wa mashtaka wameshupalia zaidi namba kuliko hata kuwa mshitakiwa anatuhumiwa kukutwa na silaha kinyume cha sheria?

Kwanini pia upande wa utetezi wanasikika kuongea CZ 100 kwenye bastola na kuwa si A5340, badala ya kukomaa tu kuwa Adamoo hakukutwa na bastola?

Kwanini kumekuwa na marumbano haya kuhusiana namba A5340?

Ni kitu gani mahsusi kinatafutwa kwenye namba hii pendwa?
Mkuu bado kuna point hapa ina miss. Kumbuka ukituhumiwa kuwa una bastola huwezi kukanusha kwa maneno kuwa mimi sikukutwa nayo. Mahakama ikaishia hapo.

Namna ya kuonesha kuwa hukukutwa nayo sio kwa kutamka tu kwamba mi sikuwa na siraha, bali ni kuwaonesha wanaokutuhumu kuwa siraha inayotajwa siyo yenyewe. Ili mshtaki akushinde lazima athibitishe beyond resonable doubt na sio kwa kusema tu tulimkuta na siraha ikatosha ushahidi. Siraha ilikuwa namba ngapi? aina gani? ikionekana kinachotajwa kuwa siraha kina idendification contradicting ndio huamuriwa kuwa anayekutuhumu amekusingizia na ni kesi ya Kusukwa.

Kinachofanywa na akina Kibatala sio kukaa mahakamani na kubishana kuwa Adamu kasekwa hakukutwa na siraha kwa maneno matupu. Aliyekukuta na siraha athibitishe ni siraha gani? Tayari mashahidi wameshapishana kwenye aina ya siraha. Trumped up cases🤣🤣🤣
 
Wanaweza kufanya ktk kesi zingine, hii denooJ nasema na kukuhakikishia tena kuwa, Mbowe ni mtu huru, hakuna Jaji wa kumfunga kwa kesi isiyokuwa na facts...

Hata wao wako monitored. Yuko aliye mkuu, mwenye haki isiyotiliwa shaka aliye juu yao anawa - monitor step by step. HATA WAO WANAOGOPA KUFA broo...!!

Lenye possibility wa 50/50 ni hili.

Kuwa lengo kuu la hayawani hawa ni kumtesa na kumpotezea muda Mbowe. Kwa hiyo mkakati wao, ni kuhakikisha mahakama hii inamhukumu kifungo. Halafu mahakama ya rufani inakwenda kutengua hiyo hukumu..

Hili linawezekana. Lakini napo ni pagumu sana kwa kuzingatia mwenendo wa kesi hii yote hadi sasa...!
Mbowe ni mtu huru kwa wapenda haki, lakini ni mfungwa kwa CCM, serikali yake, na taasisi zake mahakama ikiwa included.

Hapa Samia kaamua kutumia madaraka yake na kuikataa dhamira yake licha ya rangi za vilemba anavyobadilisha kichwani kila siku, bado naisubiri siku ya hukumu.
 
Hapa kwa hili inawezekana.
Chama changu ccm hili litatuangusha kwani ukweli utabaki kuwa ukweli na uongo hautaweza kutuweka huru tutarudi ktk zile zama za KUZOMEWA TENA.
Chama kiingilie mapema ndo maana tunamwona Ndugai, Mpina,Msukuma,Polepole wameshaona chama kama chama upepo ushaanza kubadilika.
Upinzani bungeni haupo lakini ndani ya chama na bungeni upo wazi ndo maana gazeti letu la UHURU lilipewa likizo ya kuwa KIGAZETI.
Hii kesi haitatuweka pazuri kisiasa labda tuwe tumekosa hoja kwani kesi inaonekana inavyowatesa mashahidi.

Sent from my TECNO K8 using JamiiForums mobile app
Kesi imewakalia vibaya mashahidi
 
Kesi ya kuambiana ambiana kingai kaambiwa aliyemwambia kingai kaambiwa, alieambiwa kaambiwa na mbowe nae kingai akawaambia wenzake.porokodio modona somalo fankulu makuka dio polko!
hearsay stories
 
Kuna haja ya kuwa wanarekodi haya mahojiano aisee, kwanza teknolojia imekua sana na pia hii ingeondoa kabisa huu ubishi kwamba mimi nimesikia hivi wewe hujasikia..
Kwahiyo hayarekodiwi? Tubategemea anachoandika Jaji ma Kurepotiwa na Martin Masese?
 
Hii kesi haina msingi wowote serikali futeni,shahidi mmoja wapo Ni Afande jumanne ambaye kafukuzwa kazi kwa tuhuma za kumbambikizia mtu meno ya tembo.Aliyetaka kuuawa Ni Sabaya ambaye amefungwa miaka 30 kwa ujambazi was kutumia silaha.
Na kiongozi anayedaiwa kutaka kuuliwa amefungwa miaka 30 kwa kosa la ujambazi wa kutumia siraha.
 
Hii kesi yote kwa ujumla wake ni maigizo matupu, nachosubiri sasa ni kuuona mwisho wake tu ambao hata hivyo nimeshahisi utakuwaje.
Ingekuwa ni kesi mtu kashikwa ugoni, au kakwapua hereni za msichana, ni sawa kufuta kesi. Ugaidi ni tofauti, gaidi hawezi kuachwa huru kwa sababu tu umekosea tarehe. Ossama bin Laden alikuwa na wafuasi wake dunia nzima anawalipa kutumia tigo walipue majengo. Ni wajibu tigo kushirikiana na polisi kuzuia magaidi wasilipue majengo mengine. Ingekuwa ni salamu za mapenzi I LOVE YOU kulmbe ni mume wa mtu hiyo ni siri yake.
 
Mimi naona katika kesi nzima Mbowe hajaguswa na ushahidi wa Mawakili wa Serikali. Kama hakuna exhibit ya kikao, kulipua vituo vya mafuta, kuwashambulia viongozi wa Serikali,na hajapatikana na bastola n.k. Sana sana kinachomgusa Mbowe ni zile fedha Tshs.500,000 alizomtumia Urio. Lakini mtu unaweza kumtumia fedha kama rafiki, yule mwenye shida, anayekuomba kwa hiari labda kuwepo na mazungumzo kati ya aliyetuma fedha na aliyetumiwa fedha kuhusiana na masuala ya ugaidi.
 
Kila kitu huwa ni sawa hadi hapo shida inapotokea- 500,000 kwenda kwa urio, urio kamtafuta Adamoo , adamoo kenda Moshi , Kaaya kasema aliwaona wote kwenye hotel ya MBowe, nk nk mnyororo wa thamani unaanza kuzalisha 500. 000 kuwa bilioni.
 
Yasemekana mshitakiwa #2 alikamatwa na bastola ambalo anakanusha.

Kwamba alikamatwa na bastola au hakukamatwa na bastola, hayo ni mambo mengine.

Kukamatwa na bunduki kinyume cha sheria mbona bado ni msala usio kuwa na kifani?

Kwanini upande wa mashtaka wameshupalia zaidi namba kuliko hata kuwa mshitakiwa anatuhumiwa kukutwa na silaha kinyume cha sheria?

Kwanini pia upande wa utetezi wanasikika kuongea CZ 100 kwenye bastola na kuwa si A5340, badala ya kukomaa tu kuwa Adamoo hakukutwa na bastola?

Kwanini kumekuwa na marumbano haya kuhusiana namba A5340?

Ni kitu gani mahsusi kinatafutwa kwenye namba hii pendwa?
Unadhani kuwa na Gaidi nchini ni issue ndogo tena Gaidi aliyedhamilia kuuwa viongozi na kulipia visima.
 
Huo mnyororo haumgusi Mbowe. Urio alipopeleka fedha ataeleza mwenyewe. Kama kuna written document toka kwa Mbbowe iwe produced kupeleka hizo fedha kwa watuhumiwa wengine. Kwenye kesi hakuna rafiki, ndugu wote mtajikana na kila mmoja anataka kujinasua. Kila mtuhumiwa atataka kujinasua peke yake.
 
Back
Top Bottom