Kesi ya Mbowe: Namba A5340 kwanini imekuwa issue kubwa?

Kesi ya Mbowe: Namba A5340 kwanini imekuwa issue kubwa?

Kwa hyo model ya silaha zote ni namba na pia zinakuwa na namba zikionyesha usajili au ni pistol tuu?
Kila silaha ina Model yake si lazima iwe namba. Mfano AKM ni mojawapo ya model za AK_47, na kila silaha ina Serial number ya kuitofautisha na silaha nyingine, usajili ni kitu kingine.
mfano ile silaha ya Adamoo ingekuwa imesajiliwa ingeweza kusomeka hivi :
Owner - Adamoo
Type- Luger
Model- Cz100
Serial- A5340

(Huu ni mfano)
 
Maana yake namba za usajili zilibadilishwa kukidhi nia ya kutenda uharifu bila ya kujulikana mmiliki halali ni yupi.

Serikali ndio msimamizi mkuu wa usajili wa silaha yoyote ya moto nchini Tanzania hivyo wanafahamu silaha ipi ilisajili lini wapi na mmilikishwaji ni nani kwahiyo hapo kuna mlengwa hatajwi tu kwa majina ila wanabishania utofauti wa namba kunusu au kusaidia ushahidi kumtia mtu mmowapo hatia kwamba aliruhusu silaha yake kutaka kutumika kinyume na sheria.
Silaya ya Lile Jambazi Lililokuwa DH Hai
 
Kuna limjaa flan lilikuwa mkoa mmoja una samaki wa maji barid lkn wakubwa! Alikuwa kila akiitisha press kupitia gesh ra porish anakuwa na mabunduki meng meng akidai yalikamatwa wakat wa mapambano na magambaz alikuwa anayaonyesha huku akiwa na glove nyeupe!

Ingawa kwa sasa tupo nae pale kwa mkapa kila mech ya ligi! Labda kipind kile aliwah kuitaja hyo namba a ngap ngap cjui! Sasa labda utetez wanajua hyo binduk iliwah kuonyeshwa kwenyd press! Huwez jua
 
Yasemekana mshitakiwa #2 alikamatwa na bastola ambalo anakanusha.

Kwamba alikamatwa na bastola au hakukamatwa na bastola, hayo ni mambo mengine.

Kukamatwa na bunduki kinyume cha sheria mbona bado ni msala usio kuwa na kifani?

Kwanini upande wa mashtaka wameshupalia zaidi namba kuliko hata kuwa mshitakiwa anatuhumiwa kukutwa na silaha kinyume cha sheria?

Kwanini pia upande wa utetezi wanasikika kuongea CZ 100 kwenye bastola na kuwa si A5340, badala ya kukomaa tu kuwa Adamoo hakukutwa na bastola?

Kwanini kumekuwa na marumbano haya kuhusiana namba A5340?

Ni kitu gani mahsusi kinatafutwa kwenye namba hii pendwa?
Imekuwa issue kubwa kwa sababu mtuhimiwa wa ujambazi ndio anakuwa Shahidi🤣🤣
 
Kuna limjaa flan lilikuwa mkoa mmoja una samaki wa maji barid lkn wakubwa! Alikuwa kila akiitisha press kupitia gesh ra porish anakuwa na mabunduki meng meng akidai yalikamatwa wakat wa mapambano na magambaz alikuwa anayaonyesha huku akiwa na glove nyeupe! Ingawa kwa sasa tupo nae pale kwa mkapa kila mech ya ligi! Labda kipind kile aliwah kuitaja hyo namba a ngap ngap cjui! Sasa labda utetez wanajua hyo binduk iliwah kuonyeshwa kwenyd press! Huwez jua
Mzee wa kuchakaza mpaka uchakae?
 
Ila sasa kuna upande unaotia mashaka makubwa zaidi. Huu ni ule uliotakiwa kuzingatia mwelekeo wa mihimili mingine kwenye utendaji kazi wao. Kumbuka hukumu za mapingamizi yote tokea:

1. hati ya mashtaka kukosewa na mahakama ya uhujumu uchumi kutokuwa mahali pake.

2. maelezo ya mshitakiwa kutopokelewa kama ungamo halali.

3. maelezo ya shahidi wa sita kutokuwemo kwenye furushi la committal.

4. Refa anasikia kutoka upande wa mashtaka gata ambayo upande huo hawakusema.

Hapo kupambana na refa mbona ni kazi zaidi basi kuliko hata kupambana timu pinzani?
Jaji amekuwa kama Wilson mahera wakati ea uchaguzi akawa anampigia kampeni Magufuli🤣
 
Naanza kuhisi ushahidi wa hovyo unaotolewa na mashahidi wa upande wa jamhuri mashahidi wameamua kwa makusudi kujiepusha na laana ya kikombe cha dhuluma kinachowanyemelea.

Huku sisi tukiwaona wajinga kwa ushahidi wa hovyo wanaotoa kumbe wao wanafanya hivyo makusudi ilimradi kuwaridhisha mabosi wao waliowatuma kwa kutoa ushahidi mradi watimize wajibu wao wa kwenda mahakamani.
Wanatoa ushahudi wa kuzuga bora liende wameshakula advance
 
Na wamekwisha chemsha. Handling ya vidhibiti ilikuwa ya hovyo. Finger prints zingethibitisha kama mshitakiwa aliwahi kuishika na hata hizo kete alizifunga au alizihesabu! Sio rahisi sana kukuta muuza madawa ya kulevya sio mtumiaji pia, je kun maabara imethibitisha kuwa yale ni madawa ya kulevya? Inashangaza kila shahidi aliyekuwa kwenye upekuzi anasema “kete za madawa ya kulevya” walipaswa angalau kusema “kete zinazodhaniwa ni madawa ya kulevya”. Hawajui wakihojiwa kama kuna ripoti ya maabara na ikawa haipo basi hakuna uthibitisho ni madawa ya kulevya!? Polisi wanachukua risasi tatu kama kidhibiti lakini wanaleta moja eti mbili wamezitumia. Vipi kama mtuhumiwa angedaiwa kuwa na bastola tu - wapimaji wangeshindwa kuthibitisha kama ni nzima au la?? Polisi na kitengo chao wanakosaje risasi za 9mm kwa ajili ya majaribio??!! Ugaidi gani ww kulipua vituo vya mafuta mikoa minne kwa risasi 3 na bastola??

Bahati mbaya Polisi wameshathibitisha finger prints hazikuchukuliwa. Ukiweka na huu mkanganganyiko wa Luvern, Luger na CZ 100 na mwenzake A50… unakuta jaji anapata shida!!

Shahidi anailizwa kama ana record za sauti za mratibu anasema hapana. Alitoa taarifa za uhalifu uliopangwa kwa walengwa, usalama wa taifa, kamati za ulinzi husika? Hapana!!

Kama sio uzembe basi walikuwa wanajua kabisa jambo zima halipo na hili ni rahisi kuonesha kuliko eti kulikuwa na uhalifu unaenda kutendeka!!
Dah! safi Sana ,
Wewe jamaa una Akili Sana,
Unafaa kuwa mwamuzi wa haki.
 
Raisi alitaarifiwa; hapana

DG wa tiss alitaarifiwa; hapana

Igp alitaarifiwa; hapana

RPC dar, arusha, kilimanjaro, mmeanza, morogoro mbeya walitaarifiwa; hapana

RCO wa mikoa husika walitaarifiwa: hapana

Hii kesi ni siri ya kingai na mahita na jumanne na goodluck, ndo maana washitakiwa walitolewa central moshi- dar na kupeleka mbweni Ili kuficha uhuni wao
Kamati za Ulinzi na Usalama za Wilaya,Mkoa na taifa hazikutaarifiwa,wala time ya Uchaguzi hazikutaarifiwa na Mbowe akashiriki Uchaguzi na Ugaidi wake.
 
Hii kesi yote kwa ujumla wake ni maigizo matupu, nachosubiri sasa ni kuuona mwisho wake tu ambao hata hivyo nimeshahisi utakuwaje.
denooJ, hapa hakuna kesi...

Mwisho wake ndiyo huo na sababu ni hizi;

1. KWA UPANDE WA WAANDAAJI WA IGIZO HILI NA KULIITA "KESI YA UGAIDI WA MBOWE:"

å Usifikiri kwamba waandaaji wa igizo hili hawajuti huko waliko na kujiona wajinga waliopindukia....

å Wanajuta na wanakutana kila mara kwenye vikao vyao vya "kupanga uovu" ili kushauriana kuona namna ya kuichomoa hii kuepuka kuaibika...

å Bahati mbaya kwao ni kuwa, wakiitoa mahakamani kwa maana ya kutumia ile kauli yao maarufu ya "DPP hana nia ya kuendelea nayo", bado itakula kwao na ikiendelea hadi mwisho matokeo yake ni hasara ileile upande wao..!!

2. NA KWA UPANDE WA MAHAKAMA NA JAJI ATAKAYETOA HUKUMU:

å Usidhani kuwa mpaka sasa Jaji hajaona kuwa Jamhuri wameleta kitu cha hovyo kabisa mahakamani na inakuwa ni kazi ngumu sana kuwabeba..

å Jaji Luvanda aliona hill; Jaji Mustapha Siyani aliona hili. Na huyu anayesikiliza sasa ameona hili. Unafikiri kwanini wanajitoa? Tegemea hili: Kwa kuogopa karma, usishangae siku moja huyu naye akalala mbeleeee...!!

å Ndo kusema, kuna wakati simba hula majani iwapo nyama nyikani haionekani!. Maana yangu hapa ni kuwa, Jambo hili [ukweli ktk kesi hii] uko wazi mno kuwa JAMHURI IMELETA KESI YA UONGO/YA KUSADIKIKA na uthibitisho wake ni mleta mashtaka haya kushindwa kuyathibitisha UKWELI WAKE mahakamani...

√• Nakuhakikishia jambo moja kuwa, hata walete mashahidi 100, mpàka hatua hii, hayupo wa kuupindua uongo huu kuwa ukweli...!!

å Ndo kusema kwamba, ni Jaji UNPROFESSIONAL na MJINGA PEKEE anayeweza kufunga mtu kwa ushahidi wenye matobo tobo kiasi hiki. Na Jaji yeyote akiamua kuuvaa UJINGA na UWENDAWAZIMU na kuikanyaga haki ya ndugu zetu hawa wanaonewa na kuteswa bila sababu, hakipa ATALIPA GHARAMA KUBWA SANA KTK MAISHA YAKE kuliko ile ya "Jiwe"anayolipia sasa huko kaburini kwake....!!!

å Kuna wakati hata MWIZI akijikuta ameingia kwenye nyumba ya wakwe zake kupora, huona aibu na kutoka bila kuchukua chochote anapokutanisha uso na baba mkwe wake..!
 
Yasemekana mshitakiwa #2 alikamatwa na bastola ambalo anakanusha.

Kwamba alikamatwa na bastola au hakukamatwa na bastola, hayo ni mambo mengine.

Kukamatwa na bunduki kinyume cha sheria mbona bado ni msala usio kuwa na kifani?

Kwanini upande wa mashtaka wameshupalia zaidi namba kuliko hata kuwa mshitakiwa anatuhumiwa kukutwa na silaha kinyume cha sheria?

Kwanini pia upande wa utetezi wanasikika kuongea CZ 100 kwenye bastola na kuwa si A5340, badala ya kukomaa tu kuwa Adamoo hakukutwa na bastola?

Kwanini kumekuwa na marumbano haya kuhusiana namba A5340?

Ni kitu gani mahsusi kinatafutwa kwenye namba hii pendwa?
Kwenye ushahidi upande wa mashtaka na utetezi kila mmoja ukiona kuna tofauti kwenye maelezo inakuwa ni sehemu ya kujenga hoja kwamba huu ushahidi unaunganika vizuri au haunganiki. Baadhi ya mashahidi wanadai watuhumiwa walikutwa na hiyo bastola na hizo kete za madawa ya kulevya na hawa walishuhudia upekuzi ukifanyika.

Mashahidi wengine walioshuhudia wanadai walikamatwa pia na baadhi ya pes na laini za simu. Baadhi ya mashahidi walioshuhudia walisema walikamatwa wakati wakisajili laini za simu. Wengine wanasema walikamatwa wakiwa wanatembea.

Nadhani tofauti hizi: 1) Walikamatwa wakifanya nini? 2) Walikuwa na nini? 3) Hiyo bastola ilikuwa na namba zinazosomekaje? 4) Ilikuwa namba moja tu au mbili au zaidi? 5) Je, ni aina gani ya silaha? 6) Ilikuwa na risadsi, ngapi? 7) Kitu kingine kilichokamatwa?

Maswali yote haya na majibu yake ndiyo yanayoweza kuonyesha ushahidi umeunganika (hauachi chembe ya shaka) au hauunganikia(unazua maswali mengi). Kwa hiyo, ukiona jambo linafanyiwa rejea mara kwa mara, ujue ni sehemu ile ya 'to pick holes from a person's evidence'.
 
Binafsi nimekupata na kukuelewa vizuri. Sasa tupitie hoja moja baada ya nyingine;

Kwenye ushahidi upande wa mashtaka na utetezi kila mmoja ukiona kuna tofauti kwenye maelezo inakuwa ni sehemu ya kujenga hoja kwamba huu ushahidi unaunganika vizuri au haunganiki.

Ni kweli, no doubt about this...
Baadhi ya mashahidi wanadai watuhumiwa walikutwa na hiyo bastola na hizo kete za madawa ya kulevya na hawa walishuhudia upekuzi ukifanyika. Mashahidi wengine walioshuhudia wanadai walikamatwa pia na baadhi ya pes na laini za simu.

Kwa hoja yako, unadhani kwa utofauti huu, kuna muunganiko hapo? Mbona kila shahidi anasema lake? Binafsi nasema, HAKUNA MUUNGANIKO!
Baadhi ya mashahidi walioshuhudia walisema walikamatwa wakati wakisajili laini za simu. Wengine wanasema walikamatwa wakiwa wanatembea.

Jibu ni kama la juu, HAKUNA MUUNGANIKO...
Nadhani tofauti hizi: 1) Walikamatwa wakifanya nini?

Mashahidi karibu wote wakiwemo polisi wenyewe wakamataji, wametofautiana. HAKUNA MUUNGANIKO..!!
2) Walikuwa na nini?

Kila shahidi kajibu kivyake. Hii ni ishara ya uongo. HAKUNA MUUNGANIKO
3) Hiyo bastola ilikuwa na namba zinazosomekaje?

Wamejichanganya kupita kiasi. Oral evidence baadhi wanasema A5340 yule mtaalamu wa ballistic anasema mara CZ100. HAKUNA MUUNGANIKO...
4) Ilikuwa namba moja tu au mbili au zaidi?

Mbili. A5340 na CZ100 lakini bastola ni moja. HAKUNA MUUNGANIKO!
5) Je, ni aina gani ya silaha?

Kila shahidi amekuja na jina lake. Wengine Luger wengine.......HAKUNA MUUNGANIKO!
6) Ilikuwa na risadsi, ngapi?

Kwenye maelezo yao 3 lakini mahakamani kama ushahidi wameleta 1. HAKUNA MUUNGANIKO!
7) Kitu kingine kilichokamatwa?

Kwa maelezo ya mdomo ni vingi na kila shahidi ana orodha yake. Lakini mahakamani kilicholetwa kama ushahidi ni bastola 1 na risasi 1. Tatizo, HAKUNA MUUNGANIKO!!
Maswali yote haya na majibu yake ndiyo yanayoweza kuonyesha ushahidi umeunganika (hauachi chembe ya shaka) au hauunganikia(unazua maswali mengi). Kwa hiyo, ukiona jambo linafanyiwa rejea mara kwa mara, ujue ni sehemu ile ya 'to pick holes from a person's evidence'.
YES, ndivyo ilivyo. Lakini kwa huu, USHAHIDI wa MASHAHIDI wote haupatani asilani [kwa lugha yako - ni HAUUNGANI]...

Hukumu yangu:

USHAHIDI HAUJITOSHELEZI, UNATIA MASHAKA, UNA MATOBO MAKUBWA MAKUBWA MENGI MNO, Natamka kuwa, WASHITAKUWA HAWANA KESI YA KUJIBU, NA NAAMURU WAACHIWE HURU KUANZIA SASA...

Kooooti.......!!!!
 
Back
Top Bottom