Kesi ya Mbowe: Namba A5340 kwanini imekuwa issue kubwa?

Nimechoka pale yule muuza mbege aliposema wakati wa tukio yeye alikuwa anafagia sasa leo mahita yule mama alijua anakula ina maana ule ufagio mahita alijua ni mwiko wa kupikia[emoji2][emoji2]
Na siyo hilo tuu Mahita yeye amesema hawakuwa grocery wala bar ila walikuwa vibanda umiza... Halafu askari waliofika kukamata ni 6 na wala siyo 5 aliosema muuza mbege... Pia Habari ya kwenda kupata nyama choma na ndizi yeye hajui hiyo [emoji12][emoji12][emoji12]
 
 
Suala kudaiwa kukutwa na hiyo bastola ni jambo moja, lakini kuihakikishia mahakama pasipo chembe yoyote ya shaka kupitia "finger prints" za mshtakiwa ni jambo lingine muhimu pia.

Na wamekwisha chemsha. Handling ya vidhibiti ilikuwa ya hovyo. Finger prints zingethibitisha kama mshitakiwa aliwahi kuishika na hata hizo kete alizifunga au alizihesabu!

Sio rahisi sana kukuta muuza madawa ya kulevya sio mtumiaji pia, je kun maabara imethibitisha kuwa yale ni madawa ya kulevya? Inashangaza kila shahidi aliyekuwa kwenye upekuzi anasema “kete za madawa ya kulevya” walipaswa angalau kusema “kete zinazodhaniwa ni madawa ya kulevya”.

Hawajui wakihojiwa kama kuna ripoti ya maabara na ikawa haipo basi hakuna uthibitisho ni madawa ya kulevya!? Polisi wanachukua risasi tatu kama kidhibiti lakini wanaleta moja eti mbili wamezitumia.

Vipi kama mtuhumiwa angedaiwa kuwa na bastola tu - wapimaji wangeshindwa kuthibitisha kama ni nzima au la?? Polisi na kitengo chao wanakosaje risasi za 9mm kwa ajili ya majaribio??!! Ugaidi gani ww kulipua vituo vya mafuta mikoa minne kwa risasi 3 na bastola??

Bahati mbaya Polisi wameshathibitisha finger prints hazikuchukuliwa. Ukiweka na huu mkanganganyiko wa Luvern, Luger na CZ 100 na mwenzake A50… unakuta jaji anapata shida!!

Shahidi anailizwa kama ana record za sauti za mratibu anasema hapana. Alitoa taarifa za uhalifu uliopangwa kwa walengwa, usalama wa taifa, kamati za ulinzi husika? Hapana!!

Kama sio uzembe basi walikuwa wanajua kabisa jambo zima halipo na hili ni rahisi kuonesha kuliko eti kulikuwa na uhalifu unaenda kutendeka!!
 
Mama mbege akasema walikamatwa watatu, mahita anasema aliwaona watatu ila ktk kukamata alikamata wawili....kijana msajili line wamemsahau au yumo kati ya mashahidi 25 wale
 
Namba ya mwenyekiti hiyo aligawa chumba watu wakapigia show. Ni ngumu kuelewa kwa sasa.

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app

Mnyalukolo katoa chozi jana. Hiyo namba haikuwahi kusajiliwa nchini.

Ingekuwa ya mwenyekiti mbona Kingai Sirro na wapambe wao wangefanya sherehe?
 
Nimechoka pale yule muuza mbege aliposema wakati wa tukio yeye alikuwa anafagia sasa leo mahita yule mama alijua anakula ina maana ule ufagio mahita alijua ni mwiko wa kupikia😃😃
Kijiko😀😀 mama mbege anasema aliitwa na alikuwa na dada Esther ila mahita kasema kulitokea tafran umati ukakusanyika ndo wakachagua mashahidi.....
 
Suala kudaiwa kukutwa na hiyo bastola ni jambo moja, lakini kuihakikishia mahakama pasipo chembe yoyote ya shaka kupitia "finger prints" za mshtakiwa ni jambo lingine muhimu pia.
Kama hamna finger prints?
 
Hii kesi yote kwa ujumla wake ni maigizo matupu, nachosubiri sasa ni kuuona mwisho wake tu ambao hata hivyo nimeshahisi utakuwaje.
 
Ukweli ni kwamba CZ100 Ni Bastola zinazo milikiwa na JWTZ! Sasa ilitokeje Amary? Ndo Maana Mapolisi wanahangaika na A5340 kumficha aliyeitoa ya JWTZ kumbambikia Adamoo.

Kwamba ilihitajika bastola ya kumbambikizia Adamoo?

Ziko silaha ngapi mikononi mwa polisi hata zikiwamo zilizokuwa za majambazi waliouwawa, ambazo wangeweza kuzitumia badala ya hii ya jeshi kama ilibidi?

Kwanini ya jeshi halafu kujaribu kumficha aliyeitoa?
 
Hii kesi yote kwa ujumla wake ni maigizo matupu, nachosubiri sasa ni kuuona mwisho wake tu ambao hata hivyo nimeshahisi utakuwaje.

Mwenendo na hukumu ya kesi vyote viko wazi.

Mwenendo:
--- hoja zote zisizoathiri hukumu ya kesi ya msingi zitaamriwa in favor ya utetezi.

--- Hoja zote zenye kuathiri hukumu ya kesi ya msingi zitaamriwa in favor ya mashaka.

Hukumu ya kesi ya msingi:

-- ipo tayari, ilikuwapo kabla ya kesi kuanza.
 
Ningelikuwa Mimi ni DPP ningelitupilia mbali alafu naenda kulima miogo bahati mbaya sikuwa ,hii kesi Bila kuwa upande wowote wa kisiasa investigator ndani ya jeshi la police mmechemka Sana ,ingawa kule Twitter mnafalijiwa na mtu anajiita kigogo.kibatala na wenzake wanawalia timing na itakuwa aibu kubwa Sana ,hata ninyi mjiulize kesi ya ugaidi

1.haina upelelezi kabla hajakamatwa upelelezi umeanzia alivyokamatwa

2. Jeshi la police kesi ni ya ugaidi mmeshindwaje kuwasilisha vidhibiti Kwa ushahidi wa kimaabara.Mwishoni mutaibika Sana Kuna maswali mtashindwa kuyajibu.
 
Raisi alitaarifiwa; hapana

DG wa tiss alitaarifiwa; hapana

Igp alitaarifiwa; hapana

RPC Dar, Arusha, Kilimanjaro, mmeanza, Morogoro Mbeya walitaarifiwa; hapana

RCO wa mikoa husika walitaarifiwa: hapana

Hii kesi ni siri ya kingai na mahita na jumanne na goodluck, ndo maana washitakiwa walitolewa central moshi- dar na kupeleka mbweni Ili kuficha uhuni wao
 
Kwanini basi focus ya marumbano kwenye a5340?
Me nilivyoelewa ni kwamba hiyo A5340 ni serial number ya silaha na Cz100 ni model, kwahiyo unapoongelea A5340 unakuwa very specific kwenye hiyo silaha husika ambayo haifanani na silaha nyingine yeyote duniani, Ila ukiongelea Cz100 maana yake zipo nyingi za model hiyo ikiwemo hiyo inayosemwa ni ya Adamoo no.A5340 sasa pengine kuna A5341, A5342 n.k Ni sawa na Corolla TI zipo nyingi ila namba T 123 DUD iko moja tu
 
Hapana mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…