1.) Kwenye kesi ndogo hakuna asiye fahamu Jaji aliye iamua hiyo kesi, alikuwa ameshapewa rushwa ya madaraka na aliye washitaki watuhumiwa.
2.) Kwenye pingamizi la jana, Mawakili wa utetezi walikuwa wako sahihi pia kwa mtazamo wao, maana shahidi aliletwa katika mazingira ya usiri kwa lengo la kuepukana na fedheha ya kuulizwa maswali magumu kama ilivyo tokea kwa mashahidi wenzake walio mtangulia.
Lakini baada ya ufafanuzi, wote walikubaliana kwa hoja, na shahidi akapigwa maswali ya kutosha tu na kama kawaida! Ameishia tu kujichanganya kwenye maelezo yake.
Ikumbukwe kwenye mapingamizi ni uamzi (hukumu) wala si ufafanuzi. Uamuzi wa Jaji ukishatoka iwe umeridhika au hujaridhika ndiyo basi hadi mwisho wa kesi ya msingi.
Kutumia neno ufafanuzi itakuwa ni kusema kwa kumnanga jaji huku ukimwangilia usoni.