Baada ya jana kuahirishwa, Kesi ya mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe inaendelea kuunguruma leo mahakamani. Jana kesi iliahirishwa kutokana shahidi kupata dharura ya kiafya na upande wa utetezi haukutoa kikwazo chochote kwenye sababu hiyo. Jaji aliahirisha mpaka leo. Kuwa nami.
==============
Jaji ameingia.
Kesi inatajwa
Robert Kidando anatambulisha Jopo lake
Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Tulimanywa Majige
Peter Kibatala anatambulisha Jopo la mawakili wa utetezi
Peter Kibatala
John Malya
Fredrick Kiwhero
Dickson Matata
Idd Msawanga
Nashon Nkungu
Maria Mushi
Khadija Aron
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shauri lina kuja kwa ajili ya Kusikilizwa na Leo tuna shahidi Mmoja Tupo tayari kuendelea
Wakili wa Serikal: Mmoja anatoka kwenda Kumfuata
Jaji: upande wa Utetezi
Wakili Peter Kibatala: Na sisi pia tupo tayari Kuendelea
Jaji: Shahidi Wenu?
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji ameenda Kufuatwa Anaingia Shahidi Mfupi Kavaa Kaunda
Jaji: Majina yako
Shahidi: SSP Sebastien Madembwe
Jaji: umri
Shahidi: 46
Jaji: Kabila
Shahidi: Mhehe
Jaji: Shughuli zako
Shahidi: Afisa wa Polisi
Jaji: Dini yako
Shahidi: Mkrito
Shahidi: Mimi SSP sebastian Madenge Naapa Kwamba Ushahidi nitakaotoa ni Kweli tupu Eeeh Mwezi Mungu nisaidie
Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Shahidi Ataongozwa na Wakili wa Serikali Pius Hilla
Wakili wa Serikali: Shahidi umesema Majina yako kwa ukamilifu ni nani
Shahidi: SSP sebastian Madenge
Wakili wa Serikali: Unaishi Wapi
Shahidi: Iyumbu Kule Dodoma
Wakili wa Serikali: Mkazi wa Dodoma tangu lini
Shahidi: Mwezi wa Nane 2020
Wakili wa Serikali: Kabla ya hapo ulikuwa unaishi Wapi
Shahidi: Nilikuwa naishi Muongo la Ndege Ukonga, Nikiwa Ofisa wa Polisi Makao Makuu, iliyokuwa Makao Makuu Dar es Salaam
Wakili wa Serikali: Uliajiliwa lini kama Polisi
Shahidi: 02 Mwezi 09 Mwaka 1999
Wakili wa Serikali: Katika Jeshi la Polisi Upo kamisheni gani
Shahidi: Nipo kamisheni ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai
Wakili wa Serikali: Kitengo Gani
Shahidi: Udhibiti na Usajili wa Silaha
Wakili wa Serikali: Kwa Kizungu Mnaitaje
Shahidi: Arms Management and Registration Unit
Wakili wa Serikali: Kitengo hilo kina husika na Nini
Shahidi: Usajili wa Silaha za Raia Utoaji wa Leseni za Kumiliki silaha Kibali Vya Kuingiza Silaha Nchini Vibali Vya Usafirishaji wa Silaha na Risasi Hapa Nchini