Ndugu
MpendaTz , ni kweli watu wengi na dunia karibu yote imeshaona kuwa hapo hakuna kesi bali ni watawala wachache kuitumia mahakama kukomoa wapinzani wao kisiasa....
Na kwa hiyo, na kwa lugha rahisi ni kusema kuwa, huu ni mchezo wa siasa tu uliopewa sura ya "UJINAI" na jinai anageuziwa mtu mwingine aonekanaye kikwazo kwa mambo ya watawala....
LAKINI WAFANYEJE SASA? Maana hata Rais Samia Suluhu mwenyewe bila shaka ameshaelewa kuwa, ni KWELI AMEDANGANYWA kwenye hili naye bila kujua akaingia mkenge...?
Mimi nina hakika ANALO LA KUFANYA lakini lililo na gharama za kulipa KISIASA. Na hapo ndipo ugumu ulipo. Kwamba aumeze UONGO wake au ASHUPAZE shingo ivunjike..?
UONGO WAKE kwa sababu alishautangazia ulimwengu kuwa Freeman Mbowe ni gaidi na mhalifu na wenzake anaoshirikiana nao tayari walishahukumiwa kifungo cha jela huku ukweli ukiwa kinyume chake...!!
Aidha, kesi iko mahakamani lakini cha ajabu
Rais Samia Suluhu na wenzake huko serikalini na CCM completely wameshashindwa kujenga msingi wa UGAIDI na UHALIFU wa Freeman Mbowe na hakuna hata mmoja aliyekwisha hukumiwa jela kama Rais Samia na Polisi wake wanavyodai....!!