Kesi ya Mirathi ya Dkt. Likwelile: Vicky Kamata ashindwa, mahakama yasema ndoa yao haikuwa halali

Ndoa ya kikristo haina wake wawili na huyo mzee anasemekana ana mkewe ...Ina maana ypo ndani ya ndoa yey huyo Vicky ni danga hata kama wamezaa hapa ndio tatizo.
wakati anamuoa vicky, sijui kwa ndoa ya bomani au ya wapi, ndoa yake ya awali bado ilikuwa hai (hakutoa talaka) na mke wake wa awali bado alikuwa hai. kufunga ndoa ya pili wakati ile ya awali bado ipo hai ni batili, inaifanya ndoa hiyo ya pili kuonekana kuwa bure kabisa ni sawa na hakuna kilichofungwa, na hata wakikaa kinyumba miaka miwili au zaidi presumption of marriage haiwezi kumuokoa kwasababu presumption of marriage huwa haiokoi mahawara walioishi pamoja na mwanadoa inayoendelea. vicky alikuwa hawara tu, hakuwa mke, na hana haki yeyote pale. ndivyo mahakama ilivyosema. na mahakama ipo sahihi. gold diggers mkome.
 
Ooohhhh..... Hapa unamaanisha na zile ambazo Vick ana shares.... Ila jamani busara itumike. Hizi Mali za kugombania sijui Kama huwa Zina mwisho mzuri sana
ana share katika lipi. Hana share katika mali yo yote, alighushi nyaraka kuonyesha kuwa ana share
 
... hii sheria ni mbaya iwe kwa mwanamme au mwanamke. Mahusiano ya Vicky na Likwelile hayakuwa siri; yalikuwa open na kila mtu alijua hivyo. Kama mwenye ndoa (huyo mke au hata kama ingekuwa mume) asipojitokeza itajulikana vipi?

Ni wakati sasa wa hii sheria kufanyiwa amendment, kwamba anayehisi kuibiwa mume/mke aandike barua kumtaarifu "mwizi" kwamba anamuibia mkewe/mumewe na (huyo mwizi) akabidhiwe barua chini kiapo cha afisa wa mahakama au kwa utaratibu mwingine wa kisheria utakaowekwa ili kesho na keshokutwa asije kusema sikujua - aambiwe very clearly unaiba mke/mume wa mtu.

Vinginevyo mwenye mke/mume akiamua kukaa kimya ndani ya kipindi ambacho sheria itaweka; "mwizi" asilaumiwe baadaye maana mwenye "mali" haku-declare interest from the beginning kuzuia wizi. Otherwse, hii sheria itasumbua wengi; hawara atakutumia huku akijua ana mke na hataki ujue kwa sababu zake.

Madanga wasichekwe; bali kuwe na taratibu za kijamii za kuwasaidia kwani nao ni watoto wetu na sehemu ya jamii. Cc: Victoire, Mamndenyi, Joanah, Sky Eclat, FaizaFoxy, Zurie, et. al. tieni neno hapa; leo kwa Vicky, kesho kwenu!
 
hata kama mahusiano yao hayakuwa ya siri, sheria imefanya hivyo ili kulinda sanctity of marriage (utakatifu wa ndoa), ili uingie kwenye ndoa nyingine, ila ya awali yapaswa ivunjwe, usipovunja kwanza ndio kama hayo. pia inalinda ndoa dhidi ya gold diggers. kiukweli, hata Mungu anapinga kuingiliwa kwa ndoa. michepuko mingi imekuwa ikiiba kabisa ndoa na mwanamke anafukuzwa, nadhani ni bora sheria iendelee kuwa hivi.
 
... shida ni mwenye ndoa kutokuwa mkweli kwa mwenzie kwamba nina ndoa. Pili, hata kama akiwa mkweli (kwa kauli), kuwe na utaratibu wa kisheria wa kuuweka ukweli huo kwa faida ya "mwizi" maana kwa kauli anaweza asiamini - mambo ya mapenzi tena si unayajua?
 
Fundisho KWA MAHARAWA!
 

Sawa kaka angu sina ukaribu nae ila Nina mfahamu tu.
 
although, kiuhalisia, namwoena huruma Vicky kama aliwekeza chochote pale, hatakipata. wanadamu huwa tunaishi kwa kujifunza kutokana na makosa, hakuna mkamilifu na mara nyingi makosa tunayofanya tunatakiwa kuyakubali na kurekebika. sisi sote hakuna mkamilifu, tunahitaji neema ya Mungu.
 
Ujanja .wingi mbele kiza familia ilitaka kumpa sehemu ya mali akakataa kutaka bule akome na alipe gharama za kesi
 
Hii elimu inatakiwa isambazwe, ukishafunga ndoa nenda kasajili cheti RITA.
 
Hii elimu inatakiwa isambazwe, ukishafunga ndoa nenda kasajili cheti NIDA
... sio tu kusajili ila pia RITA wawe na huduma ya wananchi kukagua vyeti vya ndoa (of course kwa utaratibu maalumu). Mfano, huduma hiyo ingekuwepo, Vicky angeweza kwenda kukagua kama Dr. Likwelile aliwahi kuwa na ndoa na kama bado iko hai. Ingesaidia sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…