... hii sheria ni mbaya iwe kwa mwanamme au mwanamke. Mahusiano ya Vicky na Likwelile hayakuwa siri; yalikuwa open na kila mtu alijua hivyo. Kama mwenye ndoa (huyo mke au hata kama ingekuwa mume) asipojitokeza itajulikana vipi?
Ni wakati sasa wa hii sheria kufanyiwa amendment, kwamba anayehisi kuibiwa mume/mke aandike barua kumtaarifu "mwizi" kwamba anamuibia mkewe/mumewe na (huyo mwizi) akabidhiwe barua chini kiapo cha afisa wa mahakama au kwa utaratibu mwingine wa kisheria utakaowekwa ili kesho na keshokutwa asije kusema sikujua - aambiwe very clearly unaiba mke/mume wa mtu.
Vinginevyo mwenye mke/mume akiamua kukaa kimya ndani ya kipindi ambacho sheria itaweka; "mwizi" asilaumiwe baadaye maana mwenye "mali" haku-declare interest from the beginning kuzuia wizi. Otherwse, hii sheria itasumbua wengi; hawara atakutumia huku akijua ana mke na hataki ujue kwa sababu zake.
Madanga wasichekwe; bali kuwe na taratibu za kijamii za kuwasaidia kwani nao ni watoto wetu na sehemu ya jamii. Cc:
Victoire,
Mamndenyi,
Joanah,
Sky Eclat,
FaizaFoxy,
Zurie, et. al. tieni neno hapa; leo kwa Vicky, kesho kwenu!