Kesi ya pili ya Uchochezi inayomkabili Tundu Lissu inaendelea mahakamani muda huu

Kesi ya pili ya Uchochezi inayomkabili Tundu Lissu inaendelea mahakamani muda huu

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
2,536
Reaction score
7,194
Wakuu,


Shauri Na. 8606/2025 la uchochezi na kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa YouTube linalomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antiphas Lissu imeahirishwa mpaka pale mahakama kuu itakapotoa majibu hivyo shauri limeahirishwa kwa muda usiojulikana na kupangiwa muda na tarehe nyingine.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeahirisha kwa muda usiojulikana Shauri Na. 8606/2025 la uchochezi na kuchapisha taarifa za uongo kwenye mtandao wa YouTube linalomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Tundu Antiphas Lissu.

Hakimu Mfawidhi Godfrey Mhini amesema ameahirisha shauri hilo kutokana na kuwepo kwa kesi ya mapitio ya shauri hilo la uchochezi katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam ambayo ilifunguliwa na Lissu, na ambayo inatarajiwa kutolewa uamuzi tarehe 11 Julai 2025.



​
 
Mbona wamebadili hakimu? Yule mwingine kapatwa na nini?
 
Wengine wako mahakamani kutetea na kuweka vifungu vya sheria sawa ila wengine wapo uraiani wanachukua fomu kwa ajili ya kuwaibia wananchi kidogo walichonacho.
 
Maza ana roho mbaya sn na katili kupita kiasi
1751365208182.jpg

Picha inajieleza kabisa mkono shavuni
 
Back
Top Bottom