ZeMarcopolo,
Asante kwa post yako. Hata hivyo:
1.
i) Mgombea Urais wa CHADEMA ndiye pia Katibu Mkuu wa CHADEMA. Katibu Mkuu wa Chama na kwa maana hii, ndiye mpishi Mkuu wa Mikakati ya Chama. Inashangaza kuona mtu asiyefahamu kinachoendelea Chama kutangaza hadharani kuwa hakuna mkakati unaoendelea na kuwa wanachadema wamahadaika. Ninatoa Mwito kwa Wanachadema halisi kukataa upotoshaji huu wa makusudi, kwa malengo ya kuindoa Chadema kwenye mikakati yake. Napenda kumjulisha mhusika na wote wenye fikra hizo kuwa wamepotea njia na wasubiri. Kama anayeandika ni mwanachadema, basi ni vizuri aandike jina lake la kweli ili tumjue na tujue anajua nini, au anapindisha nini na kwa lengo gani. Wanachama ninawaomba watulie tuli kwa kuwa Viongozi wao ni makini, na meli inayoongozwa na viongozi wao makini haitayumbishwa hata tone na force au mtu mwingine yeyote popote alipo na kwa nia yoyote aliyo nayo.
ii) Chadema inafanya kazi zake kwa mujibu wa Katiba yake, Kanuni yake na maadili yake. Haifanyi kazi kwa pressure za nje. Haifanyi kazi hata kwa pressure za wanachama wake kwa vile Wanachama ndani ya Chadema wana wajibu wao, majukumu yao na haki zao. Viongozi wana wajibu wao, majukumu yao na haki zao. Siyo kila mwanachama kwa kila kitu anaweza kufahamu kila hatua ya utekelezaji au ya mipango. Hata nyumbani mama anapopika jikoni siyo wote waliokaa sebuleni wanajua kinachoendelea jikoni. Subira pekee ndio itakayoeleza ni nini kilikuwa kinapikwa, labda wakisie tu kutokana na harafu harufu inayonukia.
iii) Kwa msingi huo ukifuatilia para ya kwanza kuwa kuna wafuasi wa chadema wamehadaika, mtoa ataarifa, japo haelezi yeye ni nani, source ya information yake ni nini jambo ambalo kwa dhahiri lingeliweza kuwatoa mashaka wanachadema anaowaita "wamehadaika". Ningemshauri kama ana nia njema ajitambulishe kwa hao anaowashauri yeye ni nani kama ni mwanachadema cheo chake ni nini na kama siyo mwanachadema amepata wapi taarifa yake kiasi cha kutaka kuwadanganya na kuwapotosha siyo tu wanachadema lakini Watanzania wengi walioipigia Kura. Hakuna maficho kuwa mamilioni ya Watanzania waliipigia kura Chadema na wao ndio hasa wenye kuongojea hatima ya kura zao kuliko wanachadema. Inalekea ZeMarcopolo siyo mdadisi, mtafiti wa kutosha kujua centre of conflict iko wapi. Napenda kumfahimisha kuwa Centre of Conflict haiko chadema bali kwa Watanzania maelfu kila kona ya nchi ambao kura zao zilichakachuliwa na wao ndio mashahidi wa awali wa uchakachuaji huo. Kama lengo la mwandishi ni kupotosha umma huo, basi amepotoka, na hilo halitatokea kwa kuwa kama mgombea Urais na Katibu Mkuu wa Chadema nina mawasiliano ya karibu sana na Watanzania hao wala siyo wana Chadema tu. Watanzania watapenda kujua kama ZeMarcopolo atakuwa jasiri na kujitambulisha kwa jina lake halisi na kwa cheo chake ili tuweze kuthamini ushauri wake. Atakuwa mtanzania wa karne ya 47 atakayesikiliza ushauri wa mtu asiye na ujasiri wa hata kuonyesha jina lake halisi. Ndio maana Dr. Slaa niko hapa kwa jina langu bila maficho, na wako humu jamvini wapambanaji ambao hawajifichi wako kwa majina yao, na wanaposimamia jambo kila mmoja anajua ujasiri wao.
2) ZeMarcopolo unasema kuwa 'shughuli za chadema zimeelekezwa kwenye shughuli za kibunge'. Chadema imepewa kura hata baada ya uchakachuaji zaidi ya 2 Millioni. Sasa ulitaka wafanye nini walale na kustarehe na hizo kura? Watanzania wengi wanaiona Chadema ndio matumaini yao pekee ya kuwakomboa kwenye makucha ya CCM na umaskini uliosababishwa na CCM. Hivyo ni dhahiri, pamoja na mikakakati yake mingine Chadema inashughulikia maswala ya kuimarisha Wabunge wake ( wabunge wanajua mipango na mikakati iliyoko kuwaimarisha), ipo kwenye mipango ya kuunda Baraza lake la Mawaziri kivuli (baada ya Serikali kuundwa-wengi hawaelewi tafsiri ya hili baada ya msimamo wa Chadema kukataa kutambua Matokeo ya Uchaguzi ningeliwashauri wawasiliane na Wanasheria wao ili kujua tafsiri halisi ya Hatua hiyo). Hiyo nayo ni shughuli za Bunge na Watanzania wengi wanahamu ya kujua Baraza Kivuli litakuwa na sura gani na itatendaji kazi zake kwa maslahi yao na Taifa kwa ujumla. Ni mtu asiyejua tu anaweza kutoa kauli kama ya ZeMarcopolo. Chadema haina kazi mmoja tu wala mkakati mmoja tu katika ukombozi wa Taifa hili. Aliyefunga akili yake kwa malengo anayofahamu tu ndiyo anaweza kutoa kauli na ushauri wa aina hiyo.
3) ZeMarcopolo ni vema akajua kuwa Chadema inaendeshwa kwa katiba, Kanuni, Maadili na Itafaki inayojulikana. Chadema siyo Brief case political party kama anavyofikiri. Kama ni mtafiti angelijua hilo au kama hana nia na lengo lilifichika pia angelikuwa na njia nyingi za kujua hilo. Hivyo, ni vyema akajua kuwa Chadema katika utekelezaji wa majukumu yake haisukumwi na mtu yeyote wala wanachama wa kawaida ( wanachama wanaelimishwa na wakielimishwa wanaridhika kama tulivyofanya kwa wale waliotaka kujua nini kinaendelea). Wanachama ndani ya Chadema wana haki zao, majukumu na wajibu wao, na viongozi nao wana majukumu, haki na wajibu wao. Hivyo katika utekelezaji wa majukumu hatusukumwi na pressure ya mtu awaye yeyote, wa ndani au wa nje kwa vile tunasukumwa tu na Katiba, Kanuni, Maadili na Itifaki ya chama. Mchakato unaoendelea utakapopitia kwenye vyombo vyote vya maamuzi utatolewa hadharani na si kabla ya hapo. Pamoja na hilo, ni vyema ZeMarcopolo akaelewa kuwa walaio chakachuliwa kura ni watanzania na wao wanamawasiliano kwa njia mbalimbali na Chama na wanaridhika na hatua tunazochukua. Kama yuko ambaye haridhiki ana lake jambo, na kwa vyovyote vile si rahisi kumridhisha kila mtu mmoja mmoja japo tunajitahidi. Ndio maana naandika kwa kina ili ZeMarcopolo aelewe kuwa kazi na hasa maswala magumu kama haya hayafanywi kwa emotions, wala kukurupuka. Yeye mwenyewe anajua uwezo wa Dr. Slaa kufanya utafiti, na kuwa hatoi kauli mpaka utafiti umefika mahali pake. Ningependa pia ZeMarcopolo aelewe kuwa vidhibiti ni watanzania wenyewe waliochakachuliwa kura zao, na Dr.Slaa ni conduit tu ya kukataa matokeo hayo. Kama haamini haya atashangaa wakati mwafaka utakapofika.
4) ZeMarcopolo anatoa ushauri kwa wafuasi wa CHADEMA kuwa waendelee na kazi zao. Hapa kuna jambo. Sijui ZeMarcopolo lini amekuwa msemaji wa Chadema kiasi cha kuwataka Wanachadema "waendelee na kazi zao" Nadhani mwenye macho haambiwi kutazama na nipende tu kumwambia ZeMarcopolo kuwa Watanzania wa 2010 siyo mwaka 47 wanaweza kuchambua pumba na mchele. Nadhani wanafahamu kabisa malengo ya ushauri huu, na ni kwa manufaa ya nani. Tumekusoma ZeMarcopolo. Hata Kauli kuwa "viongozi wanagombea uongozi wa Kambi ya Upinzani ni wa upotoshaji". Ah, nani anagombea. Kambi imeisha kuundwa, tayari kuna Kiongozi wa Kambi rasmi ya Upinzani, kuna Mnadhimu Mkuu wa Kambi (Chief Whip) na kuna Deputy Leader. Sasa nafasi zipi zinagombaniwa na viongozi. Kwa kauli hii tu unaweza pia kumsoma lengo lake ni nini ZeMarcopolo.
5) ZeMarcopolo anatoa ushauri kuwa tuwape Mwongozo wafuasi wetu. Nataka kumjulisha kuwa Tumeisha kutoa mwongozo siyo tu kwa Wafuasi wa Chadema bali kwa Watanzania walioibiwa na kuchakuliwa kura zao. Kimsingi licha ya miongozo mingine ya ndani, kuwa " Tumekataa kutambua matokeo na kumtambua Rais aliyepatikana kwa matokeo haya ( issue hapa ni UHALALI WA RAIS NA SI UWEPO wa kisheria wa Rais mtu asipoelewa au kutaka kutambua tofauti kati ya maneno haya mafupi ya kisheria atateseka daima). Huu ni mwongozo kwa Watanzania wategemee nini. Matokeo ya jambo la kutegemewa limekwisha kuonekana kwa matendo "Kususia shughuli anazofanya Rais" kuna mwongozo gani zaidi ya huu. Wabunge wametoka nje ya Bunge na Chadema imepongezwa na wote wenye nia njema na Taifa hili, na kitendo cha kutoka nje ya Bunge Duniani kote ni kitendo cha kawaida kwenye Mabunge. Kuna mwongozo gani zaidi ya huu. Au ZeMarcopolo anataka tumwage hadharani na mengine ambayo yako Jikoni? Naomba avute subira atayaona, kama siyo kwa matendo basi kwa kauli.
Chadema inapenda na inakaribisha Ushauri. Lakini Upotoshaji wa aina yeyote ile utajibiwa papo hapo ili Malengo yetu yasivurugwe na wasioitakia mema, na pia kulinda Watanzania tuliowaahidi kuwa tutawatumikia bila maslahi yeyote binafsi.