Kesi ya Trump ya uhaini dhidi ya Obama itawapa nguvu zaidi madikteta wa Africa

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
64,960
Reaction score
111,265
Tawala zisizo za kidemokrasia za Africa huwa zinapenda zaidi kuchukua mifano mibaya na makosa ya magharibi kuhalalisha maovu yao na ukandamizaji wanaowafanyia wapinzani na wakosaoji wao, ikiwa msukumo wa Trump na serikali yake pamoja uhanikizaji wa MAGA utafanikiwa kuwapa shinikizo waendesha mashitaka wa serikali ya Marekani kuwafungulia mashitaka Obama, Hillary Clinton, mkuu wa zamani wa CIA na maafisa wengine wa utawala wa Obama kwa mashitaka ya uhaini itakuwa pigo kubwa sana kwa wapinzani halisi wa Africa.
Screenshot_20250722_230303_X.jpg
20250722_225632.jpg
 
Safi tu Obama ndio kaleta machafuko Libya mwacheni kimkute kama mwenzio wa Ufaransa Nicolas Sarkozy nayeye kalipia zambi yake ya Libya !!

Obama nayeye ndio wakati wa kulipia machungu ya wa Libya.. Na Africa yote.

Libya ilikuwa msaada mkubwa kwa Africa na nguzo ya Africa..
 
View attachment 3415025View attachment 3415027
hili nalo takataka tupu in the history of America
 
Biden kabla hajatoka ofisini aliacha amemchomoa mwanae Jela kwa kutumia cheo/mamlaka cha/ya Urais

Neno demokrasia halina tofauti na neno unafiki
Demokrasia na unafiki ni vitu vinavyoenda sambamba bora udikteta kama nyeusi ni nyeusi kama nyeupe ni nyeupe ila demokrasia ni mwendo wa kunafikiana.
 
Mbona nyie haujawasaidia??
 
Safi tu Obama ndio kaleta machafuko Libya mwacheni kimkute kama mwenzio wa Ufaransa Nicolas Sarkozy nayeye kalipia zambi yake ya Libya !!

Obama nayeye ndio wakati wa kulipia machungu ya wa Libya.. Na Africa yote.

Libya ilikuwa msaada mkubwa kwa Africa na nguzo ya Africa..
kwa sababu alijenga msikiti dar? Ana faida gani kwa africa yule?
 
Acha wafu wazikane, hata yeye alifunguliwa mashitaka na utawala uliopita.
Sindio hao hao kina Obama walimfanyia hivyo nayeye now analipiza Ubaya ubwela tu 😂😂
 
Obama ni mzee wa msoga Aliye changamka

Mtu Fulani hivi anajifanya decent mbele ya camera kumbe ni Joka mla watu ,

Mimi binafsi nikisikia kuwa Obama na team yake wameshughulikiwa Nita chinja mbuzi na kugawa sadaka ,

Obama na team yake ndio chanzo kikuu Cha uvunjifu wa amani Duniani ni matapeli wa siasa wanyonya damu war mongas hapo Bado hatuja ongeleea masuala Yao machafu ya agenda zao za LGBTQ

Watu Fulani hivi ushetani upo ndani Yao na Wana Furahia kuuishi , In short Obama na team yake wanapaswa kupokwa power waliyonayo ili kui save Dunia Kwa kiwango Fulani
 
Back
Top Bottom