Kesi ya 'Ugaidi' inayomkabili Freeman Mbowe kuendelea tena Ijumaa hii, Wanachama wote wa CHADEMA Mnakaribishwa Mahakamani kufuatilia

Kesi ya 'Ugaidi' inayomkabili Freeman Mbowe kuendelea tena Ijumaa hii, Wanachama wote wa CHADEMA Mnakaribishwa Mahakamani kufuatilia

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
143,138
Reaction score
288,731
Mwamba wa siasa za Tanzania usiotikisika , Laingwanan , Mtemi Isike ama Ustaadhi Aboubakar Mbowe kama anavyofahamika huko Zanzibar , kesho anafikishwa tena Mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi waliyomtungia ya Ugaidi .

Natoa wito kwa wananchi wote na hususani ni wanachama wa Chadema kujitokeza kwa wingi kusikiliza kesi hiyo ya uongo hapo kesho , Kwa mujibu wa sheria za Tanzania haijawahi kuwa kosa kisheria kuhudhuria Mahakamani kwa usikilzaji wa kesi yoyote zaidi ya zile za faragha ambazo nyingi ni za ubakaji, ndio maana wanachama wote wa Chadema waliokamatwa kutokana na kadhia ya kesi hii wameachiwa bila masharti yoyote.

Binafsi nitakuwepo Mahakamani Mapema asubuhi ili kukuletea kila kinachojiri

Mungu ibariki Chadema

Duh.jpg
 
Hilo jina Abubakar ulilompa ndiyo limemtia nuksi, maana hayo majina na mambo anayofanya kizani yanafanana
 
Kama tunavyosherekea wagunduzi wa vitu mbalimbali na kuwapa tuzo, mfano akina Einstein, Tesla basi hapa Tanzania mnamo mwaka 2015 mara baada ya mzee wa nywele nyeupe kuwa mgombea wa chama fulani ambacho kilimtaja kwenye list of shame, hivyo mashabiki wa chama hicho kulazimishwa kumsafisha na kumpigia kampeni ili awe rais na wao wakakubali kwa kufuta list of shame kwenye tovuti ya chama chao na mara moja wakaanza kuzunguka nchi nzima wakiimba kwa kuzungusha mikono kuwa kama mtu huyu angekuwa fisadi kweli basi angefungwa maana yake walikiri kuwa walimsingizia tu!.

Baada ya mkengeuko huo ndipo akajitokeza mgunduzi wa jina la nyumbu akiwafananisha na mnyama nyumbu ambaye hanaga akili ya kufikiri mara mbili pale wanapokatiza mto Mara, hata mto uwe umejaa mamba, nyumbu kiongozi akishajirusha humo basi wote wanaofuatia watajirusha humo na kuliwa.

Leo miaka 5 imepita lakini jina la nyumbu linaendelea kuwafaa wafuasi hawa. Wao kila kitu ni kupinga na kutetea kila aina ya ujinga ili mradi tu huo ujinga umeungwa mkono na kiongozi wao.
Basi napendekeza aliyebuni jina la nyumbu asakwe huko aliko na apewe tuzo.
 
Mama Samia Suluhu Hassan hakudhania kama atakuja kuwa Rais wa JMT, ipo siku wapinzani wata washangaza ccm kuchukuwa nchi. Never say never


Lunatic [emoji2957][emoji2957][emoji2957]
 
Mwamba wa siasa za Tanzania usiotikisika , Laingwanan , Mtemi Isike ama Ustaadhi Aboubakar Mbowe kama anavyofahamika huko Zanzibar , kesho anafikishwa tena Mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi waliyomtungia ya Ugaidi...
Tutakuwapo Kisutu. Bila shaka ule uhuru ukiwamo wa vyombo vya habari aliousema SSH kwenye kuionyesha dunia haki kutendeka utaheshimiwa.

Tutakuwapo kwa wingi zaidi ili kumsaidia kuionyesha dunia kuwa amedhamiria kuona haki inatendeka.

Tukutane Kisutu Ijumaa.
 
Kama tunavyosherekea wagunduzi wa vitu mbalimbali na kuwapa tuzo, mfano akina Einstein, Tesla basi hapa Tanzania mnamo mwaka 2015 mara baada ya mzee wa nywele nyeupe kuwa mgombea wa chama fulani ambacho kilimtaja kwenye list of shame...
Wewe ni mfano tosha wa jinsi CCM ya sasa ilivyo na "vilaza" kupindukia.

Kilaza hawezi andika hoja kulingana na topic husika,yeye ni kukopi na kupesti kitu hicho hicho kimoja.

CCM ya vilaza.

Hamna hoja bali viroja.
 
Mi naomba kujua tu kuhudhuria kwenu kwa wingi kunaweza kusibugudhi watu wengine au shughuli zingine?

Labda eneo linaweza kumudu watu 200 nyie mkaenda 500 hamtoleta usumbufu?

Labda pia kwa wingi huo wengine wanaimba hamtaleta usumbufu?

Labda basi mko nje mmejazana barabarani hamtoleta usumbufu kwa wengine na shughuli zao kiujumla?

Wakati mnataka uhuru huo wa kuachwa muhudhurie kwa wingi mnaotaka, mkumbuke pia kuna watu nao wanaouhuru wa kufanya shughuli zao bila bugudha zenu.
 
Kama tunavyosherekea wagunduzi wa vitu mbalimbali na kuwapa tuzo, mfano akina Einstein, Tesla basi hapa Tanzania mnamo mwaka 2015 mara baada ya mzee wa nywele nyeupe kuwa mgombea wa chama fulani ambacho kilimtaja kwenye list of shame...
Ni baraka kwa Mungu kusheherekea gaidi mbowe kuliwa na papasi lockup

USSR
 
Watanzania sisi ni tatizo. Polisi wakisema mbowe ni gaidi mnasema polisi wanaingilia kazi za mahakamani, mtoa mada anasema ni kesi ya uongo 😂😂 kwani ww mtoa mada ni mahakama.?
 
Mwamba wa siasa za Tanzania usiotikisika , Laingwanan , Mtemi Isike ama Ustaadhi Aboubakar Mbowe kama anavyofahamika huko Zanzibar , kesho anafikishwa tena Mahakamani kwa ajili ya kusikiliza kesi waliyomtungia ya Ugaidi ...
Kuweni.makini sana tu huko hiyo Ijumaa.
 
Back
Top Bottom