Kesi ya Ugaidi: Kingai na genge lake waumbuliwa

Embu Waamue basi...Mtu kama Gaidi...Gaidi. .au kama sio Gaidi sio Gaidi...Ujue na sisi tunaosubiri Hatma tunachoka pia !
Mkuu hakuna kitu kigumu na kinachotesa Nafsi Kama kutoa HUKUMU ambayo siyo ya HAKI na ipo kinyume na HaKI uku ukijua ninachofanya siyo HAKI. hii hukumu inachelewa sababu Kuna watu wanataka batili iwe HAKI.
 
Jaji wa hovyo kabisa kuwahi kutokea
Amedhalilisha sana heshima ya ujaji katika jamii.
Awali ilifikiriwa kuwa mtu anayeteuliwa kuwa jaji basi ni mtu mwadilifu, mweledi na aliyejaa hekima. Lakini kumbe hata muhuni tuu mradi awe na LLB basi anaweza kupewa ujaji na sio Jaji Kiongozi au Jaji mkuu anaye weza kumnyoosha akipinda
 
Ameonyesha waziwazi kuwa ameletwa ajili ya kumfunga Mbowe na hakuna kingine
Halafu wanamfunga kwa kipi sijui. Maelezo ya watuhumiwa wengine ndio kitu pekee wanachotaka kitumike lakini sasa ni wazi kuwa waliwatesa na kuwalazimisha kusaini.
Taifa lina laanika kwa kuwatungia uongo raia wake wawatese. Hivi hawaogopi laana hizo? Yaani hata mwaka tuu haujaisha washasahau yale ya 17th March?
 
Katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mh Mbowe na wenzake watatu,leo Shahidi upande wa utetezi Ndg Lembrus Mchome mkaazi wa Wilaya ya Mwanga kaithibitishia Mahakama kwamba D/C Msemwa alikuwa akihudumu kituo cha police Oysterbay na si Central Police kama alivyodai wakati akitoa ushahidi wake kwamba alimpokea mshitakiwa Mohammed Ling’wenya.

Ndg Lembrus alikuwa akikabiliwa na kesi ya makosa ya mtandao.Pamoja na kutoa ushahidi wake mbele ya Jaji anayesikiliza kesi hiyo pia aliweza kuwasilisha nyaraka mbali mbali zenye kuunga mkono madai yake.

Kupitia ushahidi huu ambao mawakili wa Serekali hawakuutarajia kabisa ni wazi sasa madai ya washitakiwa Adamo na Ling’wenya kwamba hawakuwahi kufikishwa Central police hata mara moja badala yake walipelekwa Vituo vya Police TAZARA na Mbweni yatakuwa yamepata nguvu kubwa kweli kweli.
Sasa napata shida kidogo

DC Msemwa anadai alikuwa anafanyakazi Oysterbay Police lakini aliwapokea Lingwenya na wenzake.

Lingwenya na mwenzake wanasema walipelekwa Tazara Police na Mbweni.

Hebu tuwaze hapo, Oysterbay inahusikaje ambapo haijatajwa hata na washtakiwa
 
Kwenye heading umemtaja kingai humu ndani umetaja watu wangine
 
Kwa hiyo Mchome ndiye muajiri/bosi wa Msemwa. Au ktk kesi hiyo ya Mchome, Msemwa ndiye alikuwa mpelelezi wake? Yaani mchome amekuja na orodha ya askari walipangiwa kufanya kazi Oysterbay? Tusishangilie mwisho ukawa "kama ulimuona atakuwa alikuwa anapita tu kituochake ni Central"😇😇
 
Katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mh Mbowe na wenzake watatu,leo Shahidi upande wa utetezi Ndg Lembrus Mchome mkaazi wa Wilaya ya Mwanga kaithibitishia Mahakama kwamba D/C Msemwa alikuwa akihudumu kituo cha police Oysterbay na si Central Police kama alivyodai wakati akitoa ushahidi wake kwamba alimpokea mshitakiwa Mohammed Ling’wenya.

Ndg Lembrus alikuwa akikabiliwa na kesi ya makosa ya mtandao.Pamoja na kutoa ushahidi wake mbele ya Jaji anayesikiliza kesi hiyo pia aliweza kuwasilisha nyaraka mbali mbali zenye kuunga mkono madai yake.

Kupitia ushahidi huu ambao mawakili wa Serekali hawakuutarajia kabisa ni wazi sasa madai ya washitakiwa Adamo na Ling’wenya kwamba hawakuwahi kufikishwa Central police hata mara moja badala yake walipelekwa Vituo vya Police TAZARA na Mbweni yatakuwa yamepata nguvu kubwa kweli kweli.
Hv mtu anatunga uongo kwa binadamu mwenzake ili apate nn ? Lkn malip hapa hapa dunian cku moja mh mbowe atakuwa huru na wenzake
 
Mkuu Retired unadhani yote hayo hajui/hawajui? Wanajua sana kutokana na yanayojadiliwa kwenye mitandao ya kijamii kwani wanaisoma, na siku hizi wanaifuatilia sana. Hata hao mawakili wa serikali hadi wanapiga simu kuuliza vijiwe vyao wanavyo nywea bia watu wanasemaje.
Shida ni kiburi na kujisahau. Lakini kulikuwa na wenye viburi, ubabe na dharau kama Sabaya au Bashite? Wana hali gani? Ni mashaka na hudhuni tuu mioyoni mwao. Jaji asijidanganye kuwa anaweza kutenda uovu akawa salama siku zote, hata Hagaya mwenyewe uovu hauwezi kum guarantee usalama maana tumeona wababe kabisa kama Albashir, Mubarak, Mugabe au Gaddafi wakitepeta.

Mtu mwema jamii itakupigania na katikati ya mateso uta tabasamu. Ona Mbowe alivyo sasa, hafichi uso akija mahakamani na anasalimia kwa bashasha na watu wanasimama kumpa heshima.
Mbowe anatia huruma. Amechoka na anaelekea kukata tamaa mapingamizi yanavyotupwa tupwa.
 
Mchome kanifurahisha sana leo wakati akihojiwa na wakili wa Serekali.

1. Mashahidi wa kuchongwa .......
2. Mawakili michongo sababu wanatetea mashahidi wa uongo.
3. Majaji michongo kwasababu wanatoa hukumu ambazo hazipo sawa.

Mahakama kicheko haaaaaaa haaaaa Mawakili wa Serekali wabaki na mshangao.
 
Katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mh Mbowe na wenzake watatu,leo Shahidi upande wa utetezi Ndg Lembrus Mchome mkaazi wa Wilaya ya Mwanga kaithibitishia Mahakama kwamba D/C Msemwa alikuwa akihudumu kituo cha police Oysterbay na si Central Police kama alivyodai wakati akitoa ushahidi wake kwamba alimpokea mshitakiwa Mohammed Ling’wenya.

Ndg Lembrus alikuwa akikabiliwa na kesi ya makosa ya mtandao.Pamoja na kutoa ushahidi wake mbele ya Jaji anayesikiliza kesi hiyo pia aliweza kuwasilisha nyaraka mbali mbali zenye kuunga mkono madai yake.

Kupitia ushahidi huu ambao mawakili wa Serekali hawakuutarajia kabisa ni wazi sasa madai ya washitakiwa Adamo na Ling’wenya kwamba hawakuwahi kufikishwa Central police hata mara moja badala yake walipelekwa Vituo vya Police TAZARA na Mbweni yatakuwa yamepata nguvu kubwa kweli kweli.

Ndiyo maana juhudi kubwa ilifanyika mwanzo wa kusikilizwa kwa kesi hii inayowakabili mwenyekiti pamoja na walinzi wake 3, umma usiruhusiwe kuingia mahakamani kusikiliza mwenendo wa kesi hii kwa manufaa mapana ya umma kuelewa ukweli wa tuhuma zinazowakabili washtakiwa, ushahidi, pamoja na utendaji wa maofisa wa vyombo vya mihimili ya dola.
 
Sasa napata shida kidogo

DC Msemwa anadai alikuwa anafanyakazi Oysterbay Police lakini aliwapokea Lingwenya na wenzake.

Lingwenya na mwenzake wanasema walipelekwa Tazara Police na Mbweni.

Hebu tuwaze hapo, Oysterbay inahusikaje ambapo haijatajwa hata na washtakiwa

Kweli kuna mchanganyiko sana lakini ninadhani washitakiwa walipokelewa Oysterbay na kisha siku ya pili Tazara na baada ya Bwire kukamatwa wakahamishiwa Mbweni mpaka walipofikishwa mahakamani. Uongo hapa ni kuwa DC Msemwa aliwapokea akiwa Central! Na shahidi wa leo ndio anathibitisha kuwa mpk karibia kabisa na tarehe za kukamatwa washitakiwa, Msemwa alikuwa bado Oysterbay (kinyume na alivosema alikuwa amehamishiwa Central). Umbuka barua ya Lingw’enya iliyokataliwa na Jaji?? Ilikuwa ikitaka documents kuthibitisha uwepo wa Msema kituoni siku hiyo. Kumbuka maelezo yaliyoandikwa na Msemwa Central yana jina lake tu na sio sahihi kwenye DR. Barua ile ilikataliwa kwa sababu ilikuwa inaalika nyaraka kuja mahakamani ambazo zingeharibu picha nzima. Tuaibiri kuona kama bado itajibiwa na hizo nyaraka kutolewa.
 
Katika kesi ya ugaidi inayomkabili Mh Mbowe na wenzake watatu,leo Shahidi upande wa utetezi Ndg Lembrus Mchome mkaazi wa Wilaya ya Mwanga kaithibitishia Mahakama kwamba D/C Msemwa alikuwa akihudumu kituo cha police Oysterbay na si Central Police kama alivyodai wakati akitoa ushahidi wake kwamba alimpokea mshitakiwa Mohammed Ling’wenya.

Ndg Lembrus alikuwa akikabiliwa na kesi ya makosa ya mtandao.Pamoja na kutoa ushahidi wake mbele ya Jaji anayesikiliza kesi hiyo pia aliweza kuwasilisha nyaraka mbali mbali zenye kuunga mkono madai yake.

Kupitia ushahidi huu ambao mawakili wa Serekali hawakuutarajia kabisa ni wazi sasa madai ya washitakiwa Adamo na Ling’wenya kwamba hawakuwahi kufikishwa Central police hata mara moja badala yake walipelekwa Vituo vya Police TAZARA na Mbweni yatakuwa yamepata nguvu kubwa kweli kweli.
Mungu ibariki Chadema
 
Back
Top Bottom