Mkuu
Retired unadhani yote hayo hajui/hawajui? Wanajua sana kutokana na yanayojadiliwa kwenye mitandao ya kijamii kwani wanaisoma, na siku hizi wanaifuatilia sana. Hata hao mawakili wa serikali hadi wanapiga simu kuuliza vijiwe vyao wanavyo nywea bia watu wanasemaje.
Shida ni kiburi na kujisahau. Lakini kulikuwa na wenye viburi, ubabe na dharau kama Sabaya au Bashite? Wana hali gani? Ni mashaka na hudhuni tuu mioyoni mwao. Jaji asijidanganye kuwa anaweza kutenda uovu akawa salama siku zote, hata Hagaya mwenyewe uovu hauwezi kum guarantee usalama maana tumeona wababe kabisa kama Albashir, Mubarak, Mugabe au Gaddafi wakitepeta.
Mtu mwema jamii itakupigania na katikati ya mateso uta tabasamu. Ona Mbowe alivyo sasa, hafichi uso akija mahakamani na anasalimia kwa bashasha na watu wanasimama kumpa heshima.