Kesi ya Ugaidi: Kingai na genge lake waumbuliwa

Tunatatakiwa kuwa na vyombo vya dola na mahakama zinazoheshimika kwa kutoa haki kwa Kila mwananchi.
Haki lazima itendeke na ionekane kwamba imetendeka.
Ni hatari sana kama wananchi walio wengi wakikosa imani kwa vyombo vya dola na mahakama.
Viongozi lazima waelewe hivi kwa mustakabali mwema wa taifa.
Kazi ya jaji ni kutoa haki na kuonesha kwamba haki imetendeka.
Ni busara yanapokuwepo malalamiko ya watuhumiwa, jaji atumie mahakama kuthibitisha ukweli au uongo wa tuhuma hizo kwa uwazi bila kuegemea zaidi kwenye mbinu za kisheria zisizoeleweka na walio wengi na zisizotoa haki.
Siyo lazima uwe mwanasheria mbobezi kujua haki ipo wapi.
 
simba,syami,tiganga hamuoni aibu?
 
I am thinking of a situation where I can tell the judge kuwa Mh Jaji upande mwingine una upa uzito zaidi kuliko unavyotupa sisi/ au mzania kati yetu na wenzetu unaelemea upande mmoja (kutumia lugha ya kisaarabu) halafu unamuachia ameze au ateme!
Ni bora kumwambia moja kwa moja imwingie vizuri, maana hata ukilemba yeye bado ataelekea upande uleule unaompeleka chooni.
 
Kwa uongo huo wa polisi tutaamini vipi kama na mshtaka sio ya uongo? P. Kibatala et al wanafanya kazi nzuri sana.
 
Kova alikua anahojiwa na clouds 360 akasema tangu astaafu akiwapigia simu marafiki zake hawapokei simu Tena siku hizi.
Alisema hata Makonda siku hizi hampokelei simu yake. Kova yuko ktk mtanzuko wa kisaikolojia mkubwa sana baada ya kustafu.
 
Sabaya alikuwa anaangalia chini muda wote akikwepa kamera. Guiltness!
 
Wanazidi kuumbuka.

Si kidogo yaani ACP Kingai kupitia kesi alipiga hesabu umri wa kustaafu IGP Sirro umekaribia sana.Kwakuwa kafanikiwa kumbambikia kesi Mbowe angefikiriwa kuchukua mikoba ya Sirro.

Alirejesha kumbukumbu nyuma jinsi Mahita alivyoukwaa uIGP kwa kumpiga mabomu Lyatonga Mrema.

Hili sasa limekuwa tatizo la vyombo vyetu vya usalama na hata Mahakama tuliona jinsi Jaji aliyekuwa akisikiliza kesi alivyopandishwa haraka haraka kuwa Jaji Kiongozi.

Katiba mpya itaondoa huu ujinga.

Ngongo kwasasa Chato shule ya Museveni
 
Vyombo vya dola ukimfurahisha mfalme hata ukimwaga damu za watu unaitwa mchapa kazi jasiri usiye na woga. Unapewa cheo kikubwa zaidi.
 
Hivi hawa police wakistaafu huwa wanaendelea kulindwa?
Walindwe na Nani? Kuna yule mmoja alikua RPC Dar, baada ya kustaafu na kukosa pesa za rushwa alizokua amezoea alichoka mpaka akkaajiriwa na wahindi Kama mlinzi wa bureau de change pale Kona ya India na Zanaki. Silaha aliyokua anatumia Ni Ile migobore iliyotumika Vita kuu ya kwanza.
Just imagine RPC he Hawa wabeba bunduki.
Mimi huwa nawaangaliyaga mapolisi, nawaangaliyaaaaa......nasemaga fainali uzeeni.
Kwanza wenyewe kwa wenyewe hawspendani. Polisi akistaafu anakaa hata mwaka hajapewa nauli ya kurudi kwao usweken. Mafao Sasa ndio balaaa....
 

Yaani wakati mwingine unabaki unashangaa,kwasababu maovu yote waliyotenda yawatafuna hadi watoto wao.
 

Nasikia macho yanazidi kumtoka muda wowote yanaweza kudondoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…