Kesi ya uhaini dhidi ya John Pambalu kutajwa mahakamani kesho Novemba 4, 2026

Kesi ya uhaini dhidi ya John Pambalu kutajwa mahakamani kesho Novemba 4, 2026

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuwa kesi ya uhaini inayomkabili Mkurugenzi wake wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uchaguzi, John Pambalu, inatarajiwa kutajwa kesho, Jumatano, Novemba 4, 2026, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, saa 3:00 asubuhi, mbele ya Hakimu Mkazi Mashasha.

Katika taarifa iliyotolewa leo, imesema kesi hiyo ni ya pili ya uhaini inayomkabili kiongozi wa chama hicho. Aidha, imedai kuwa kufunguliwa kwa kesi hiyo ni mwendelezo wa matumizi mabaya ya Sheria ya Uhaini yanayokandamiza demokrasia na uhuru wa kujieleza nchini.

CHADEMA imetoa wito kwa viongozi, wanachama, wadau wa haki na demokrasia pamoja na wananchi kwa ujumla kufika mahakamani kufuatilia mwenendo wa shauri hilo, ikieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu kama ilivyofanyika katika mashauri mengine yanayogusa haki na misingi ya demokrasia nchini.

Soma Pia: John Pambalu ashtakiwa kwa UHAINI

TAARIFA KWA UMMA (1).jpg
 
Wanafikiri matumizi ya dola ndio yatawafanya watu warudi nyuma.

Wajiulize wame- archive nini kwenye kuteka na kuua.

Halafu ndio Lema anataka kutuambia hawa ndio watu wakuwa handled kwa busara!

Kanisa Katoliki Mungu awabariki sana.
 
Dah;
Ila sasa kinchoendela hapa Naanza kuelewa kwa nini Lema alisema kwamba Jumba Bovu litwaangukia watu wengi sana.
 
The only institution iliyosimama against haya madudu catholic church
 
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuwa kesi ya uhaini inayomkabili Mkurugenzi wake wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uchaguzi, John Pambalu, inatarajiwa kutajwa kesho, Jumatano, Novemba 4, 2026, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, saa 3:00 asubuhi, mbele ya Hakimu Mkazi Mashasha.

Katika taarifa iliyotolewa leo, imesema kesi hiyo ni ya pili ya uhaini inayomkabili kiongozi wa chama hicho. Aidha, imedai kuwa kufunguliwa kwa kesi hiyo ni mwendelezo wa matumizi mabaya ya Sheria ya Uhaini yanayokandamiza demokrasia na uhuru wa kujieleza nchini.

CHADEMA imetoa wito kwa viongozi, wanachama, wadau wa haki na demokrasia pamoja na wananchi kwa ujumla kufika mahakamani kufuatilia mwenendo wa shauri hilo, ikieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu kama ilivyofanyika katika mashauri mengine yanayogusa haki na misingi ya demokrasia nchini.

Soma Pia: John Pambalu ashtakiwa kwa UHAINI

atavuna alichopanda
 
The only institution iliyosimama against haya madudu catholic church
catholic wako nyuma ya haya watafikiwa tu, kwasasa hao waliokimbia mmoja baada ya mwingine, nchi hii ya utawala wa sheria.
 
Dah;
Ila sasa kinchoendela hapa Naanza kuelewa kwa nini Lema alisema kwamba Jumba Bovu litwaangukia watu wengi sana.
si wanaropokaga bila kutumia akili,kwani hata osama kilichomcost si ni mdomo tu,,yule khamein kilichomcost ni mdomo tu,,LOOSE MOUTHS CAN SINK SHIPS
 
Sasa Makamanda nawapa home work, muulizeni John Pambalu anapenda zitumike 4R au atakomaa jela mpaka haki ishinde?

Maana vijana wengi hamuijui jela.
 
Sasa Makamanda nawapa home work, muulizeni John Pambalu anapenda zitumike 4R au atakomaa jela mpaka haki ishinde?

Maana vijana wengi hamuijui jela.
Hivi siku akishika nchi mpinzani,akaanza kulipa kisasi!Mtalaumu kweli?
Maana matamshi ambayo yameshatolewa na makada wa CCM ni makali ambayo yangetamkwa na upinzani basi ingehesabiwa ni Ugaidi!
Nchi hii hakuna haki bila kumwaga damu!
 
Dogo katelekezwa na mabwana zake Kenya maisha yakamchapa hatari!! So far jela ugali ni wa bure naona asaiv atanenepa!!
 
Kasikilize nyimbo ya kina Ndanda Cosovo kichaa na Fm Academia (Prison) ili angalau ujuwe jela ni nini maana unadhani jela ni mchezo wa kuigiza.
Mkuu, JELA UNAZOEA TU binadamu kaumbwa hivyo.

Japo sijawai PATA maswahibu ya kwenda JELA

Ila NIMEWAI ishi maisha ya kigereza gereza mfano kula chakula ambacho NGURUWE wakipewa wanagoma kula kula maharage YALIYO ozaa kuishi kwa sheria Kali tena bila kuwa na uhuru wowote

Ndio maana nasema JELA UNAZOEA tena JELA za mjini hakuna KAZI NYINGI nenda magereza ya kilimo kaka NSENDA KULE utalima matuta manane Kila siku

Matuta yenyewe ni marefu mnoo utaita maji mmaaa noma sanaa binadamu ana adapt
 
Hivi siku akishika nchi mpinzani,akaanza kulipa kisasi!Mtalaumu kweli?
Maana matamshi ambayo yameshatolewa na makada wa CCM ni makali ambayo yangetamkwa na upinzani basi ingehesabiwa ni Ugaidi!
Nchi hii hakuna haki bila kumwaga damu!
Wewe uko hapa siku nyingi ni lini mimi nimewahi kusimama upande wa wauwaji maccm?

Uandishi wangu ni fasihi kwa vijana wa kisasa wanaoona kila mwenye mtazamo mpya na tofauti tayari ana jina jipya la msaliti.

Hawa watoto waliovamia mitandaoni wengi hawajui Lema amekaa jela Kisongo na hawa hawa washenzi wa ccm walimpa kesi ya mchongo.

Sasa siasa hamuwezi kwenda kama nyumbu unafika wakati unachange strategy hata timu za mpira zinaposaka matokeo zinabadili mifumo.

Bahati nzuri sisi kwetu Tanganyika haya ni marudio tu shughuri ilikuwa Zanzibar wao kwa style yao wameamuwa kugawana nusu mkate, kule Kenya Odinga alipambana na Rutto then Rutto akawa mshindi, lakini karata za ODM zikaona waungane na Rutto.

Sasa hapa kwetu kuna tabia inaota mizizi hata humu JF, ukiwa na maoni tofauti na hawa watoto basi utaambulia matusi, upumbavu huu haukubaliki.

Lema huyuhuyu ndio alisimama kidete kuhakikusha kaka yake Mbiww anang'oka na Lisu akamfanya kuwa wakala wake yani ushindi wa Lisu ukaachwa mikononi kwa Lema.

Lei hii kundi la wapuuzi wachache bila vivid evidence wanamshambulia Lema hivi mnadhani yeye ana roho ya chuma asijibu mapigo?
 
Pambalu nae anaenda gerezani huku wafuasi wa Mange wakikesha mitandaoni kupiga kelele tu.

Siasa ni barabarani sio mitandaoni.
 
Back
Top Bottom