Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza kuwa kesi ya uhaini inayomkabili Mkurugenzi wake wa Oganaizesheni, Mafunzo na Uchaguzi, John Pambalu, inatarajiwa kutajwa kesho, Jumatano, Novemba 4, 2026, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, jijini Dar es Salaam, saa 3:00 asubuhi, mbele ya Hakimu Mkazi Mashasha.
Katika taarifa iliyotolewa leo, imesema kesi hiyo ni ya pili ya uhaini inayomkabili kiongozi wa chama hicho. Aidha, imedai kuwa kufunguliwa kwa kesi hiyo ni mwendelezo wa matumizi mabaya ya Sheria ya Uhaini yanayokandamiza demokrasia na uhuru wa kujieleza nchini.
CHADEMA imetoa wito kwa viongozi, wanachama, wadau wa haki na demokrasia pamoja na wananchi kwa ujumla kufika mahakamani kufuatilia mwenendo wa shauri hilo, ikieleza kuwa hatua hiyo ni muhimu kama ilivyofanyika katika mashauri mengine yanayogusa haki na misingi ya demokrasia nchini.
Soma Pia: John Pambalu ashtakiwa kwa UHAINI