TUNDU LISSU ANAHOJIWA MASWALI YA DODOSO NA WAKILI WA SERIKALI
Nassoro Katuga: Uliposema hatujaleta video, wewe umeleta maneno na nini?
Lissu: Sina kazi ya kuthibitisha kama wewe.
Nassoro Katuga: Ni sheria ipi inasema natakiwa kuleta video?
Lissu: Sheria ya Ushahidi.
Nassoro Katuga: Umesema kwa mujibu wa Sheria ya Ushahidi, anayetakiwa kuthibitisha anatakiwa kuja na ushahidi?
Lissu: Siyo kifungu cha ngapi, bali sheria inasema unapoleta ushahidi wa nyaraka lazima ulete nyaraka.
Nassoro Katuga: Sheria ipi?
Lissu: Principles of sheria ya ushahidi.
Nassoro Katuga: Twende taratibu, tutavunja undugu. Usilete ujuaji.
Lissu: Siyo lazima uwe ndugu yangu na mimi ni mjuaji haswa.
Nassoro Katuga: Principle ya wapi?
Lissu: Principle ya sheria.
Nassoro Katuga: Ile sheria ya mtu anayeleta shutuma must prove, wewe umeprove?
Lissu: Mimi nimeprove mtu safi.
Nassoro Katuga: Ulisema hii ni nchi huru.
Lissu: Ndiyo, ni nchi huru.
Nassoro Katuga: Ukiwa shahidi, kuna sehemu yoyote umekanusha maneno ya “Tutakinukisha, tutazuia uchaguzi, tutahamasisha uasi”?
Kama nimekusikia, umesema haya maneno kwamba wameyatoa katika video ya masaa matatu.
Katika ushahidi wako wote, kuna neno lolote katika Mahakama hii umesema maneno haya siyo ya kwangu na ukitaka kuyaelewa lazima usikilize video yote?
Lissu: Maneno ya mashahidi wenu.
Nassoro Katuga: Mimi siwezi kutumia yale maneno yako. Ulikuwa unauliza mashahidi kwamba “una akili timamu.” Wewe ni kaka yangu.
Nassoro Katuga: Ulisema siyo ya kwako, hukusema?
Lissu: Sikusema.
Nassoro Katuga: Sasa wewe ni kaka yangu, unajizungusha-zungusha muda wote nini?
Lissu: Sijakataa, nimesema haya. Shida nakataaje na hayana shida.
Nassoro Katuga: Umesoma historia?
Lissu: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Ni kweli wakoloni waliwatumia viongozi wenye tamaa ya uongozi?
Lissu: Viongozi gani?
Nassoro Katuga: Je, wazungu waliingia Afrika kwa kutumia viongozi wenye tamaa?
Lissu: Waliwatumia viongozi kupitia mikataba.
Nassoro Katuga: Kwa hiyo Waarabu waliingia kama wakoloni kwa kutumia viongozi wenye tamaa?
Lissu: Waarabu hawakuwa wakoloni, walikuja kama wafanyabiashara.
Nassoro Katuga: Kwa hiyo unakubali kwamba waliingia mikataba?
Lissu: Ndiyo, kama wanavyoingia mikataba kina Samia leo. Hawakuingia na watu wa chini huku.
Nassoro Katuga: Ulisema kuhusu utetezi wa madini?
Lissu: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Na ukawa unatetea makinikia yatoke?
Lissu: Huko sikusema, lakini ukitaka nitakwambia kuhusu taarifa ya Magufuli kwamba ilikuwa “professorial rubbish.”
Nassoro Katuga: Unasema mtetezi wa madini na unapigania yatoke?
Lissu: Ukitaka huko twende tu.
Nassoro Katuga: Nitarudi baadaye.
Nassoro Katuga: Ulisema ulikuwa Rais wa TLS?
Lissu: Ndiyo.
Nassoro Katuga: Umeiambia Mahakama kwamba ulishaitakiwa wakati ukiwa Rais wa TLS katika kesi hii?
Lissu: Hapana.
Nassoro Katuga: Nilisikia unasema wewe ni mtaalamu wa kesi za uchaguzi.
Lissu: Ni kweli.
Nassoro Katuga: Je, ni namna gani sheria inasema Tanzania namna ya kupiga uchaguzi, au sheria inayokinzana na Katiba?
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI