TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI
Alijitambulisha Assistant Superintendent of Police, Lugano Bwasi, kuwa OC CID.
Nimekaa pale takribani saa nzima.
Nikamuuliza Afande, kwa nini mmenikamata na kunidhalilisha namna hii? Nimefanya kosa gani?
Akaniambia, “Tumepewa amri ya kukukamata na RPC wetu, na hajatuambia kosa lako ni nini. Utajua mbele ya safari.”
Waheshimiwa Majaji, baada ya kukaa Mbinga around saa moja, giza limeingia, nikapelekwa ofisi ya RPC.
Anaitwa Michael Chilia.
Nilimuuliza RPC Chilia, “Watu wako wa Mbinga wamenikamata. Wewe ndiyo umewaamuru? Niambie nimefanya kosa gani?”
RPC Chilia alisema yeye alipokea maelekezo kutoka Dodoma kwamba nikamatwe na nipelekwe Dar es Salaam, ambapo kuna kesi imefunguliwa, lakini hakusema ni kesi gani.
Waheshimiwa Majaji, ni RPC Chilia ndiye aliniambia, “Tunakusafirisha Dar es Salaam usiku huu huu.”
Siku hiyo, tarehe 09, toka asubuhi nilikuwa nimesafiri hadi Mbamba Bay. Mimi na watu wangu tulikuwa hatujala kabisa.
Nassoro Katuga: Samahani Waheshimiwa Majaji, naona kama ushahidi unaanza upya. Naona kama proceedings zinavurugika.
Lissu: Ninachotaka kusema hapa ni kwamba RPC Chilia hakuniambia kosa langu.
Sasa, katika orodha ya mashahidi ambapo upande wa mashtaka walisema watawaleta kutoa ushahidi, ni pamoja na ASP Lugano Bwasi, ambaye alinikamata, pamoja na Makunja, RCO wa Ruvuma, ambao waliorodheshwa lakini hawakuja hapa.
Ni ushahidi wangu kwamba kama wangeletwa, wangedhibitisha jinsi zoezi la ukamataji lilivyofanyika kinyume na sheria. Ndiyo maana hawakuletwa.
Waheshimiwa Majaji, sehemu yangu ya mwisho ya ushahidi haitakuwa ndefu.
Jaji Ndunguru: Itachukua muda gani?
Lissu: Sijui, ila naelekea kumaliza.
Waheshimiwa Majaji, ipo hivi...
Jaji Ndunguru: Ukisema leo masaa mawili na muda umezidi tayari.
Lissu: Na mimi sijui saa kwa sababu nipo gerezani.
Jaji Ndunguru: Sasa hivi ni saa 7.
Lissu: Haitofika saa 7.
Waheshimiwa Majaji, mashahidi wote 17 waliandika maelezo Polisi.
Katika hao mashahidi 17, mashahidi 16, maelezo yao ni vielelezo vya utetezi wangu.
Waheshimiwa Majaji, mashahidi wote 17 wametoa ushahidi wa maneno kwa kiapo katika kizimba hiki.
Na wote, without exception, wametoa ushahidi wa maneno ambao haulingani na vielelezo vilivyopo hapa Mahakamani.
Wote wameongeza mambo kwenye ushahidi wa mdomo ambayo hawakuyasema kwenye ushahidi wa maandishi.
Na niliwahoji wote.
Waheshimiwa Majaji, ni ushahidi wangu kwamba ushahidi wa maneno unaotofautiana na ushahidi wa maandishi kwenye jambo hilo hilo ni ushahidi usioaminika.
Ndiyo kusema, katika ushahidi wangu, ushahidi wote wa mashtaka hauaminiki.
Mwisho, kuhusiana na huo ushahidi usioaminika...
Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa PW1, PW2, PW6, PW9, PW12 na PW16, hawa wote ni Polisi.
Mashahidi wote hawa, wakiandika maelezo yenyewe, wakajikanya wenyewe, wakajishuhudia wenyewe, na niliwauliza wote ni sheria gani inawaruhusu kufanya hiki. Wakasema wao wamezoea kufanya hivyo.
Kwa sababu ni Polisi, wanahisi wapo juu ya sheria.
Na vielelezo vyao vya wote, D1 ya PW2, D2 ya PW3, D3 ya PW6, D15 ya PW15, kwa sababu ni Polisi.
Ni shahidi mmoja tu wa Polisi ndiye aliandika maelezo yake mbele ya Polisi mwingine kama inavyotakiwa na sheria, ambaye ni Detective Corporal Amani Michael.
Waheshimiwa Majaji, wape Mapolisi wa Ruvuma, ASP Lugano na ACP Makunja, maelezo yao yaliandikwa na Polisi wengine, lakini hawakuletwa.
Wangekuja tungethibitisha maelezo yao waliandika kwa usahihi, lakini hawakuletwa.
Waheshimiwa Majaji, ushahidi wangu ni huo.
Nimemaliza, na mtani samahani, nimevuta-vuta kidogo.
Jaji Ndunguru: Shahidi, unaweza kutufafanulia hapa mwisho kuhusu Mapolisi walioandika maelezo yao wenyewe?
Lissu: Kwa sababu ni ushahidi, Waheshimiwa Majaji, huo ushahidi ambao wa aina hiyo ya attitude unafanya ushahidi wa Prosecution kuwa unreliable.
Naomba hiyo hiyo final statement iongezewe kuwa ushahidi wa namna hii, na ukijumuisha makosa ya namna hii, unafanya ushahidi wote kuwa unreliable kwa kosa kubwa la namna hii.
Jaji Ndunguru: Umemaliza?
Lissu: Nimemaliza, Waheshimiwa Majaji.
Jaji Ndunguru: Upande wa mashtaka.
Wakili wa Serikali: Waheshimiwa Majaji, tunaomba health break tupate ahirisho.
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, tunakubaliana?
Wakili wa Serikali: Waheshimiwa Majaji, tunaomba saa moja.
Lissu: Naomba nyongeza ya nusu saa niongee na mashahidi wangu.
Jaji Ndunguru: Kwa hiyo tuta-resume Mahakamani saa 8 na nusu.
Majaji wanatoka HIGH COURT.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI