Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

Huyo jamaa kama mimi sema amenizidi attention yake hata kwenye mazingira kama hayo mimi nisingetoboa, lakini kwa kumbukumbu nipo vizuri hasa za maongezi kati yangu na mtu huwa sisahau kilarahisi
Na vitabu huwa unakumbuka page zote? Mi nadhani ni Chakula nilichokula utotonk, yaani kumbu kumbu zangu ziko mbali sana, nilisema taarifa bila kurudia rudia zinampita huku zinatokea huku
 
kwahiyo wewe hapo ukijiasses unajiona una akili gentleman, right? :pedroP:
Ebi pisha uzi huu tafadhari sio level yako, wewe kasifie upuuzi wa CCM huko. Harafu si huwa unaanzisha nyuzi unaishia matusi na kupuuzwa umeshakataa tamaa siku izi? unavamia sehemu za watu wenye akili ili uonekane umechangia? Hapa zinatumika fact sio mipasho kenge wewe umeona kumbukumbu zilizofumuliwa hapo ulitegemea? Wewe mbwa mtu nimekupima jana nikajua wewe ni boga bovu kabisa pale ulipokuwa unabisha eti " makamu ajiudhuru aende wapi" punga wewe una kazi ya kufanya uchawa na hao unaojipendekeza kwao hawakutambui maana kwa unavyojionesha utadhani unajua sana kumbe mbugila tu.
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI

Kama wanataka kukitumia, wakitumie. Na kama wanasema watakuwa na furaha, kwa nini walalamike?

Kwa hiyo, tuendelee, Waheshimiwa Majaji.

Wao walikuwa hawataki wakitumie, ndiyo maana hawakusoma. Sasa wakitumie tu. Ni kwa ajili ya kesi hii, mimi nitakitumia.

MAJAJI WANATETA KIDOGO

Bado Mahakama ipo kimyaaaaaaa. Majaji wanateta.

Swali la watu wengi humu: Kwa nini Jaji Ndunguru anazungumza na kuteta na Jaji mmoja wa upande wake wa kulia tu, na wa kushoto huwa hashirikishwi lolote? Jaji wa kushoto siku zote yupo bize na laptop yake tu.

Jaji Ndunguru: ā€œLinda, tuseme kwamba kwa sababu kielelezo kimeshaingia Mahakamani, tunashindwa kusema kitumike kwa namna gani. Isipokuwa tusitumie kielelezo kwa kusoma chote; badala yake useme umeona nini.ā€

Lissu: ā€œAsante, Waheshimiwa Majaji. Siku wanasoma chote nilijua nasoma specific kwa nia.ā€

Sasa, Waheshimiwa Majaji, shahidi Amini Mahamba anasema: ā€œNa mwenzangu tuliposikiliza video hii, ndiyo tukaona kuna makosa ya jinai ya uhaini na kuchapisha taarifa za uongo.ā€

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, PS16 aliona nia? Je, PW2 aliona nia?

PW2 John Kaaya aliandika hivi katika picha hiyo ya mjongeo: ā€œNilimuona ndugu Tundu Antipas Lissu akitamka matamshi yenye viashiria vya jinai.ā€

Hakuna mahali popote alipozungumza kwamba ameona uhaini au nia ya uhaini, ila anasema aliona matamshi yenye viashiria vya jinai.

PW17 kwenye maelezo yake aliona yafuatayo, na PW17 ndiye aliyepiga picha.

Katika mkutano huo uliokuwa unaongozwa na Tundu Antipas Lissu, alikuwa akizungumza kuhusu ā€œNo Reform, No Electionā€ na masuala ya uchaguzi katika majimbo yao.

Hakuona uhaini.

Anasema nilikuwa nikizungumzia masuala ya matatizo katika uchaguzi.

Hakuna mahali popote kuna habari ya uhaini.

Na PW17, katika mashahidi wote, ndiye shahidi pekee aliyekuwepo katika mkutano na hakuona uhaini wala kuona kosa lolote katika mkutano huo.

Waheshimiwa Majaji, kwenye kesi hii hoja ya pili inayogombaniwa ni manifestation ya nia (hayo maneno yanayodaiwa ni uhaini).

ā€œMsimamo huu unaashiria uasi. Ni kweli, ni kweli kwa sababu tunaenda kuzuia uchaguzi. Uchaguzi huu tutauvuruga sawasawa, kwa sababu tunakwenda kukinukisha kisawasawa.ā€

Sasa, ushahidi unasemaje juu ya haya maneno?

Waheshimiwa Majaji, kuhusiana na haya maneno, PW1, PW2 na PW16 ushahidi wao unafanana.

Unafanana kwa sababu wanasema waliona hiyo video, na waliyasikia hayo maneno.

Na ushahidi wao unafanana kwa sababu wote wanasema mimi ndiye niliyechapisha, mimi ndiye niliyepeleka Jambo TV.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa PW17 unasemaje? (The eyewitness.)

Waheshimiwa Majaji, shahidi namba 17 katika maelezo yake D16 anasema hivi:

ā€œKatika mkutano huo, masuala ambayo yalikuwa yakizungumzwa na viongozi hao wakiongozwa na Tundu Antipas Lissu yalikuwa yakihusu matatizo ya uchaguzi.ā€

Waheshimiwa Majaji, shahidi ambaye alikuwepo hajayaona haya maneno wala hajayasikia.

Angeyaona angeandika; angesikia angesema pia.

Hakuyaona na ndiye the eyewitness.

Na kuhusu uchapishaji, PW17 alisema katika kielelezo chake na alisema hapa Mahakamani kuwa yeye ndiye aliyechapisha kwa kupiga picha kwa kutumia camera ya Sony HXA-NX100, yeye na wenzake wanne wa Jambo TV.

Na PW17 alisema kwa maandishi katika kielelezo chake na Mahakamani kuwa yeye ndiye aliyepeleka na kuhifadhi katika mtandao wa Jambo TV, katika YouTube na mtandao wa X.

Mashahidi wasiokuwepo wanasema maneno yalisemwa, ila shahidi aliyekuwepo hajasema hayo maneno na amesema yeye ndiye kasambaza kwa publications and distribution, kwa ushahidi wa maandishi na kwa ushahidi wa mdomo hapa Mahakamani.

Lissu anarejesha vielelezo.

Waheshimiwa Majaji, PW17 aliulizwa katika cross-examination kuwa alisikia kauli yoyote ya kijinai. Jibu lake: Hapana.

Nikamuuliza: Ulisikia kauli yoyote ya kihaini? Jibu lake: Hapana.

Waheshimiwa Majaji, ushahidi wangu juu ya hiyo publications, intention na distribution, juu ya mashahidi, umejichanganya namna hiyo. Wasiokuwepo wanasema kulikuwa na kosa, ila aliyekuwepo anasema hapakuwa na kosa.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI

Waheshimiwa Majaji, juu ya mkanganyiko kuhusu maneno yaliyosemwa au hayakusemwa, kama palikuwa na nia au hapakuwa na nia, jambo hili lingeweza kutatuliwa kama pangekuwa na video yenyewe.

Na wajibu wa kuleta video na kuthibitisha ni wajibu wa upande wa mashitaka, lakini hawakuleta.

Mahakama haiwezi kukaa na kujua kuhusu mazungumzo yaliyomo kwenye video wakati video yenyewe haikuletwa.

Na kosa nililoshitakiwa nalo linasema ni kosa la kuchapisha maneno kwenye video kwenye mtandao. Kwa hiyo, proof ni video, na haipo. Hawakuleta hiyo video, Waheshimiwa Majaji.

Waheshimiwa Majaji, wakati wa Preliminary Hearing, upande wa mashitaka ulihaidi kuleta vielelezo 11, na vimeorodheshwa katika memorandum iliyoandaliwa na Mahakama.

Walisema vielelezo vya maandishi ni 9 na visivyo vya maandishi ni 2, lakini hawajaleta hata kimoja. Hata kimoja. Hata kimoja. Ni maneno tu. Na maneno matupu hayavunji mfupa.

Maneno hayatengenezi uhaini. Katika kesi ya Grey, Makungu Matata na Gandhi, tumeletewa maneno matupu.

Waheshimiwa Majaji, kwenye kesi hii na kwa ushahidi ambao umeletwa Mahakamani, kuna matukio mengi ya ukiukwaji wa sheria na taratibu za upelelezi, za ukamataji. Kuna extreme of illegalities, na illegalities hizi zinatengeneza mashaka makubwa juu ya kesi nzima hii.

Waheshimiwa Majaji, kitendo cha kwanza cha ukiukwaji wa taratibu wakati wa upelelezi wa hili shauri ni sheria, na sheria yenyewe ni Sheria ya Mamlaka ya Mashitaka.

Mamlaka ya upelelezi ni Mamlaka ya Mashitaka, kwa sababu wao ndiyo wanaoratibu Criminal Investigation kupitia mamlaka haya.

Nassoro Katuga: Mheshimiwa Jaji, Sama Hani Shahidi aliapa kama shahidi, lakini naona sasa anatoa opinion. Najua ni mtaalamu wa sheria, lakini sasa anatoa opinion badala ya kufanya utetezi.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, nalay foundation katika ushahidi wangu. Kama Wakili wa Serikali hapendi niseme matukio ya kiharamu ni yapi, nitaacha.

Jaji Ndunguru: Twende direct.

Lissu: Sawa, Waheshimiwa Majaji.

Kwa hiyo, ni ushahidi wa namba 1 na shahidi namba 16 katika ushahidi wao niliwauliza hivi?

Jaji Ndunguru: Haya tuliyoandika.

Lissu: Yafuteni kama Wakili wa Serikali hayapendi.

Lissu: Sasa nikawauliza PW1 kwamba DPP ndiye aliyeratibu huu upelelezi, wakajibu hapana.

Nikauliza tena: Mwakilishi wa DPP alikuwepo katika timu ya upelelezi? Wakajibu hapana, ila mwenzie akajibu alikuwepo. Nimemsahau jina, ana jina la Kibantu, ila huyo wa jina la Kibantu hayupo katika orodha ya mashahidi wala ushahidi wake.

Waheshimiwa Majaji, shahidi namba 1, 2 na namba 16 niliwauliza kwamba mnajua PGO 1 ya 3 inaeleza kuhusu haki za kikatiba za watuhumiwa wakati wa upelelezi?

Haki zenyewe ni haki ya kutoa maoni, haki ya kujieleza na haki ya kujumuika. Wakasema ndiyo, wanafahamu.

Na nikawauliza, je, mnafahamu kwenye PGO mmeamuliwa kutokwenda nje ya hizo kanuni? Wakajibu ndiyo.

Nikawaambia waeleze namna ambavyo wamezingatia hizo haki zangu, na hawakuwa na cha kusema.

Waheshimiwa Majaji, mashahidi hao hao, PW1 na PW16, niliowaonyesha matakwa ya vifungu vya 55(2) na 63(B) vya Kanuni ya Adhabu. Kimsingi, ulipinga Serikali, ukitoa kauli za kuishambulia Serikali, ukitoa maneno ambayo yanapinga Serikali, lengo likiwa kuonyesha Serikali imekosea katika Katiba.

Vifungu hivyo vinasema unakuwa hujatenda kosa, wakasema ndiyo, hivyo ndivyo vifungu vinavyosema.

Nikawauliza: Hayo maneno yana shida gani kama tukisema ubovu wa Katiba, ubovu wa sheria, na yalikuwa na lengo la kubadilisha vyote hivyo? Na hawakuwa na chochote cha kusema.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI WATU WASOME
 
Na vitabu huwa unakumbuka page zote? Mi nadhani ni Chakula nilichokula utotonk, yaani kumbu kumbu zangu ziko mbali sana, nilisema taarifa bila kurudia rudia zinampita huku zinatokea huku
Kwenye kukumbuka page hapana niwe mkweli, mimi nipo ivi tukizungumza kitu hata kwa muda mrefu huwezi kuja kunibadilishia story nitakuwa nakumbuka kila kitu mzee. Kuna story moja ipo kwenye kichwa changu hadi leo niliisikia kwenye redio fulani moro kilikuwa ni kifo cha kiongozi fulani wakati kinaanza kutangazwa ilikuwa asubuhi mzee lile Tangazo lilisemwa mara moja tu na hapo likabadilishwa! Lakini sure nakwambia nilisikia na hamna kusahau
 
Mashahidi 8 ambao ni Mapolisi hao ni mashahidi wa Jeshi la Polisi linaloongozwa na IGP Camilius Wambura na DCI Ramadhani Kingai ambao nimeonesha kuwa nina ugomvi nao wa zaidi ya miongo miwili.

Person vendetta dhidi yangu, Hii vendetta ni neno la kiitaliano lenye maana ya Chuki.
Hawa watu wamekuwa na chuki dhidi yangu ndio wameleta hao mashahidi waje kunitolea ushahidi wa uhaini.
Sasa naanza kuelewa kwanini siku ya kwanza alianza na Historia ya Mapambano yake
 
ā€œMsimamo huu unaashiria uasi. Ni kweli, ni kweli kwa sababu tunaenda kuzuia uchaguzi. Uchaguzi huu tutauvuruga sawasawa, kwa sababu tunakwenda kukinukisha kisawasawa.ā€
Ninachokiona hapa LISSU anaweka wazi kwamba kilichompandisha kizimbani ni Mvutano wa kimaana wa maneno hayo hapo juu, Hivyo kama hakuna aliethibitisha uwepo wa uhaini, kinachovutana ni tafsiri ya maneno sio uhaini wenyewe.

Kumpa kesi ya uhaini wamefail sana kesi ilitakiwa kuwa ni "Uchochezi", Wange win kwa mujibu wa kauli zake hizi.

Lakini uhaini hapana, na ni kwa ukweli kwamba uhaini unathibitishwa na vielelezo sio Tafsiri yako binafsi ya kile mtu mwengine amezungumza.
 
Back
Top Bottom