Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI

Katika hizo timu 3, timu ninayotaka kutolea ushahidi ni Timu ya Operesheni, ndiyo ilikuwa inahusika na ukamataji.

Nilimuuliza swali: Je, ni wewe ndiyo uliamuru nikamatwe? Akasema hapana.

Kiongozi Mkuu wa Timu ya Operesheni, nikamuuliza: Unafahamu ni nani aliamuru nikamatwe? Jibu lake ni hapana.

Nikamuuliza ilikuwaje nikakamatwa, na jibu lake likawa nilipigiwa simu na DCP Ramadhani Ng’anzi kuwa mtuhumiwa amekamatwa Mbinga na anasafirishwa kuletwa Dar es Salaam.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, huyo aliyetoa taarifa kwamba nimekamatwa ni DCP Ramadhani Ng’anzi, ambaye anasema ndiye aliyemuunganisha na DCI Ramadhani Kingai na, presumably, Camilius Wambura.

Kwa hiyo, ni ushahidi wangu kwamba nilikamatwa kwa maelekezo ya DCI Ramadhani Kingai na, presumably, Camilius Wambura, ambao kwa miaka kadhaa wamekuwa na mikakati ya kujaribu kunifunga.

Waheshimiwa Majaji, hayo aliyoyasema PW1 yalithibitishwa substantially na PW16, Assistant Commissioner of Police Amini Mahamba.

Waheshimiwa Majaji, mashahidi wengine wa Polisi ni PW2, PW3, PW6, PW9, PW12 na PW15.

Ushahidi wao wote kwa ujumla wao ni ushahidi wa watu wa Ramadhani Kingai na Camilius Wambura.

Maafisa wa Polisi ambao wakubwa wao wamekuwa na mikakati ya kunifunga kwa miaka 24.

Nitakapofanya majumuisho ya ushahidi huu (final submission), ushahidi wa mashahidi hawa ni legally worthless.

Ushahidi ambao hauna thamani.

Unahitaji kuthibitishwa na mashahidi huru.

Jaji Ndunguru: Sasa si umesema utaleta baadaye?

Lissu: Ndiyo, nitaleta baadaye, nitaleta baadaye.

Sasa naomba kuzungumzia ushahidi wa mashahidi ambao hawakuwa Polisi: PW4, PW5, PW7, PW8, PW10 na PW17. Hao ndiyo mashahidi ambao hakuna anayewajua isipokuwa ma-Prosecutor.

Mashahidi hawa wote tuna ushahidi wao wa maandishi na ushahidi wa mdomo wakiwa hapa niliposimama.

Na, in bracket, hata mashahidi wa Polisi wote isipokuwa PW1, lakini wote tuna ushahidi wao wa maandishi.

Sasa nirudi kwa hawa mashahidi wa kificho, Waheshimiwa Majaji.

Waheshimiwa Majaji, ukimuachia PW4, wengine wote 7, that is, walisema hivi kwa maandishi na wakiwa kizimbani hapa:

1. “Walipanga njama za kufanya uhalifu wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka...” kwa maelezo yao Polisi.

Jaji Ndunguru: Walifanya?

Lissu: Walisema kwamba walipanga kufanya vurugu, kuchoma vituo vya Polisi, kupiga Polisi.

Na hayo maelezo yao ni utetezi kwangu.

Na wote hao, ukiachilia PW4, wote walikamatwa na Polisi.

Na wote walikamatwa katika hizo siku 4 za kati ya tarehe 04 na 08 April. Polisi walikuwa wanawajua na wakawakamata within 4 days.

Jambo la tatu: Wote hawa, baada ya kukamatwa na Polisi, walikiri mbele ya Polisi (waliconfess) kwamba tunapanga kufanya uhalifu, kwa maandishi na wakiwa kizimbani.

Na jambo la nne: Wote waliachiwa ili wakaendelee kupanga njama.

La tano: Wote waliitwa na Polisi na kuambiwa: “Kubalini muwe mashahidi dhidi ya Tundu Lissu.”

Na mkikubali kuwa mashahidi dhidi ya Tundu Lissu, tunafuta mashitaka yenu.

Na wote walifutiwa mashitaka yao.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE UJUMBE UFIKE MBALI
Inaitwa Kachags twende hii..anazidi kuchanganya...
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI

Kama wanataka kukitumia, wakitumie. Na kama wanasema watakuwa na furaha, kwa nini walalamike?

Kwa hiyo, tuendelee, Waheshimiwa Majaji.

Wao walikuwa hawataki wakitumie, ndiyo maana hawakusoma. Sasa wakitumie tu. Ni kwa ajili ya kesi hii, mimi nitakitumia.

MAJAJI WANATETA KIDOGO

Bado Mahakama ipo kimyaaaaaaa. Majaji wanateta.

Swali la watu wengi humu: Kwa nini Jaji Ndunguru anazungumza na kuteta na Jaji mmoja wa upande wake wa kulia tu, na wa kushoto huwa hashirikishwi lolote? Jaji wa kushoto siku zote yupo bize na laptop yake tu.

Jaji Ndunguru: “Linda, tuseme kwamba kwa sababu kielelezo kimeshaingia Mahakamani, tunashindwa kusema kitumike kwa namna gani. Isipokuwa tusitumie kielelezo kwa kusoma chote; badala yake useme umeona nini.”

Lissu: “Asante, Waheshimiwa Majaji. Siku wanasoma chote nilijua nasoma specific kwa nia.”

Sasa, Waheshimiwa Majaji, shahidi Amini Mahamba anasema: “Na mwenzangu tuliposikiliza video hii, ndiyo tukaona kuna makosa ya jinai ya uhaini na kuchapisha taarifa za uongo.”

Kwa hiyo, Waheshimiwa Majaji, PS16 aliona nia? Je, PW2 aliona nia?

PW2 John Kaaya aliandika hivi katika picha hiyo ya mjongeo: “Nilimuona ndugu Tundu Antipas Lissu akitamka matamshi yenye viashiria vya jinai.”

Hakuna mahali popote alipozungumza kwamba ameona uhaini au nia ya uhaini, ila anasema aliona matamshi yenye viashiria vya jinai.

PW17 kwenye maelezo yake aliona yafuatayo, na PW17 ndiye aliyepiga picha.

Katika mkutano huo uliokuwa unaongozwa na Tundu Antipas Lissu, alikuwa akizungumza kuhusu “No Reform, No Election” na masuala ya uchaguzi katika majimbo yao.

Hakuona uhaini.

Anasema nilikuwa nikizungumzia masuala ya matatizo katika uchaguzi.

Hakuna mahali popote kuna habari ya uhaini.

Na PW17, katika mashahidi wote, ndiye shahidi pekee aliyekuwepo katika mkutano na hakuona uhaini wala kuona kosa lolote katika mkutano huo.

Waheshimiwa Majaji, kwenye kesi hii hoja ya pili inayogombaniwa ni manifestation ya nia (hayo maneno yanayodaiwa ni uhaini).

“Msimamo huu unaashiria uasi. Ni kweli, ni kweli kwa sababu tunaenda kuzuia uchaguzi. Uchaguzi huu tutauvuruga sawasawa, kwa sababu tunakwenda kukinukisha kisawasawa.”

Sasa, ushahidi unasemaje juu ya haya maneno?

Waheshimiwa Majaji, kuhusiana na haya maneno, PW1, PW2 na PW16 ushahidi wao unafanana.

Unafanana kwa sababu wanasema waliona hiyo video, na waliyasikia hayo maneno.

Na ushahidi wao unafanana kwa sababu wote wanasema mimi ndiye niliyechapisha, mimi ndiye niliyepeleka Jambo TV.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa PW17 unasemaje? (The eyewitness.)

Waheshimiwa Majaji, shahidi namba 17 katika maelezo yake D16 anasema hivi:

“Katika mkutano huo, masuala ambayo yalikuwa yakizungumzwa na viongozi hao wakiongozwa na Tundu Antipas Lissu yalikuwa yakihusu matatizo ya uchaguzi.”

Waheshimiwa Majaji, shahidi ambaye alikuwepo hajayaona haya maneno wala hajayasikia.

Angeyaona angeandika; angesikia angesema pia.

Hakuyaona na ndiye the eyewitness.

Na kuhusu uchapishaji, PW17 alisema katika kielelezo chake na alisema hapa Mahakamani kuwa yeye ndiye aliyechapisha kwa kupiga picha kwa kutumia camera ya Sony HXA-NX100, yeye na wenzake wanne wa Jambo TV.

Na PW17 alisema kwa maandishi katika kielelezo chake na Mahakamani kuwa yeye ndiye aliyepeleka na kuhifadhi katika mtandao wa Jambo TV, katika YouTube na mtandao wa X.

Mashahidi wasiokuwepo wanasema maneno yalisemwa, ila shahidi aliyekuwepo hajasema hayo maneno na amesema yeye ndiye kasambaza kwa publications and distribution, kwa ushahidi wa maandishi na kwa ushahidi wa mdomo hapa Mahakamani.

Lissu anarejesha vielelezo.

Waheshimiwa Majaji, PW17 aliulizwa katika cross-examination kuwa alisikia kauli yoyote ya kijinai. Jibu lake: Hapana.

Nikamuuliza: Ulisikia kauli yoyote ya kihaini? Jibu lake: Hapana.

Waheshimiwa Majaji, ushahidi wangu juu ya hiyo publications, intention na distribution, juu ya mashahidi, umejichanganya namna hiyo. Wasiokuwepo wanasema kulikuwa na kosa, ila aliyekuwepo anasema hapakuwa na kosa.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI

Ambapo Dar es Salaam waliuawa watu zaidi ya 300 katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana.

Na wawili, PW5 na PW10, walitoka Arusha, na huko Arusha, kwa mujibu wa Jaji Chande, waliuawa watu 53.

Na wawili walitoka Mbeya, ambapo kwa mujibu wa Jaji Othman Chande, huko Mbeya waliuawa watu 80.

Songea walitoka mashahidi wawili, PW5 na PW7, na kwa mujibu wa Tume ya Jaji Othman Chande, Songea pia waliuawa watu, lakini idadi yake hawakuitaja.

Waheshimiwa Majaji, PW16, ACP Amini Mahamba, mbele ya Mahakama hii alisema yeye alikuwa katika timu ya upelelezi ya matukio ya mauaji ya Oktoba 29.

Nikamuuliza, hawa waliosema watafanya fujo, na fujo zikatokea, watu wakauwawa namna hii, mmewachukulia hatua yoyote? Jibu lake lilikuwa: Hapana.

Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa wahalifu wa namna hii una uzito kiasi gani kisheria?

Huu ndiyo ushahidi wa Serikali dhidi yangu.

Ushahidi wa mashahidi waliokiri uhalifu, wakakamatwa, wakakiri, wakaachiwa, wakarudi katika maeneo yao kufanya uhalifu na watu wakauwawa, ni ushahidi wa namna gani?

Ushahidi wa namna hii, kwa kusema kwa pole, ni totally unsafe and totally unreliable.

Waheshimiwa Majaji, shitaka dhidi yangu linasema kwamba nilitengeneza nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

Na nikathibitisha (manifest) nia hiyo kwa kutamka yale maneno maarufu.

Sasa, Waheshimiwa Majaji, kuhusiana na shitaka hili na kwa mujibu wa maamuzi ya kisheria ambayo tumeyazungumza sana mbele yenu ya Grey, Makungu na Ghandi.

Kuhusu utiifu kwa Serikali, hilo halina mjadala.

Lakini zinasemaje kuhusu nia ya kutenda kosa la uhaini?

Kwenye hoja hii, Waheshimiwa Majaji, mashahidi waliotoa ushahidi kuthibitisha ni PW1 George Byagemu, PW2 Inspector John Kahaya, PW16 ACP Amini Mahamba na PW17, mwandishi wa habari.

Waheshimiwa Majaji, kwa ridhaa yenu, naomba nipatiwe vielelezo D1, D15 na D16.

Waheshimiwa Majaji, kielelezo D1 ni maelezo ya onyo ya PW2 John Kahaya.

Jaji Ndunguru: Twende taratibu.

Lissu: Nimesema nipatiwe kielelezo D1, maelezo ya John Kahaya, na D15, maelezo ya Amini Mahamba, na maelezo ya shahidi wa 17.

Jaji Ndunguru: Umeshapewa?

Lissu: Sinapewa bado.

Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka mnalolote?

Mawakili wa Serikali: Apewe, Mheshimiwa.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, PW1 ni shahidi pekee ambaye maelezo yake hayakuwasilishwa Mahakamani.

Waheshimiwa Majaji, PW1 katika ushahidi wake alisema mimi nimetengeneza nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kuhamisha, kusimamisha uchaguzi, na kwamba Serikali ndiyo inasimamia uchaguzi, kwa hiyo akaona nia katika inayodaiwa kuwa kauli niliyoitoa.

Waheshimiwa Majaji, shahidi mwingine aliyeona nia hiyo ni PW16 Amini Mahamba.

Waheshimiwa Majaji, kwenye kielelezo D15, maelezo yake ya onyo Polisi alisema maneno yafuatayo:

“Kuonyesha kwamba nilikuwa na nia ya kutenda hilo kosa la uhaini.”

“Mimi pamoja na timu nzima ya upelelezi tuliitizama na kusikikiza video hiyo, ndiyo tulipobaini kuna makosa ya jinai, kosa la kwanza ni uhaini na kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo.”

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga: Samahani, Waheshimiwa Majaji, kielelezo hiki kimepokelewa kwa mujibu wa kifungu 163 cha Sheria ya Ushahidi kuanza kurejea na kutumia kama content yake itakuwa ina contradict, kwa sababu kilitumika kwa mazingira maalumu.

Sasa anakirejea kwa misingi ipi na sisi tunakitumia dhidi yake?

Kama anachokifanya ni sahihi kwa uelewa wake wa sheria, itakula pande zote mbili.

Mimi nilidhani anacontradict tu kielelezo.

Sasa yeye anakisoma baada ya kuwa kimepokelewa. Je, kwa misingi ipi?

Sisi tunataka kukitumia kielelezo hiki dhidi yake.

Tunaomba Mahakama itoe mwongozo.

Waheshimiwa, ni hayo tu.

(Anakaa chini.)

Anasimama tena Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga:

Waheshimiwa, ni kwamba ilikuwa ni kwa ajili ya ku-contradict.

Lissu: Nianze kwa wao kusema itakuwa furaha. Mimi nitakuwa more happy wakikitumia.

Wanasema watakitumia pia dhidi yangu, sasa mimi nasema Mahakama itoe ruhusa wao wakitumie dhidi yangu.

Waheshimiwa Majaji, kielelezo kilitengenezwa kwa ajili ya kesi hii.

Hawakutaka kisomwe ili nisiweze kumuhoji shahidi wao, ila Mahakama ilishakipokea na kielelezo kipo kwa ajili ya ushahidi.

Kama kielelezo kipo kwa ajili ya kesi, nitakitumia kwa ajili ya kesi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Dragon mzee
 
Ni wach1che wenye memory capacity kunwa kama huyu mwamba
Huyo Jamaa Ubongo wake ni 1000T
Huyu mtu ni kama ana kamemory card kichwan sio kwa kukumbuka yote hayo. Mungu atasimama na wewe lissu na wote waliokufanyia huo uhuni wajue kwamba barabara ya kwenda mbinguni haipiti kwao.
Jamaa ana kumbukumbu kana kwamba hata ukiwa na Nondo unasoma wewe utakosea ila yeye atapata,🤣
 
aah,
kibaraka kaja kumalizia hotuba zake za kuaga ndugu, jamaa na marafiki kabla ya kuhukumiwa kifungo jela na kunyongwa hadi kufa, right?🐒
Mkata viuno wa lumumba buku7fc lissu sio mhaini mhaini NI samuya na genge lake walifanya mapinduzi Kisha wakajiapisha na waliuwa watanganyika wasiokua na idadi
 
Huyo Jamaa Ubongo wake ni 1000T

Jamaa ana kumbukumbu kana kwamba hata ukiwa na Nondo unasoma wewe utakosea ila yeye atapata,🤣
Huyo jamaa kama mimi sema amenizidi attention yake hata kwenye mazingira kama hayo mimi nisingetoboa, lakini kwa kumbukumbu nipo vizuri hasa za maongezi kati yangu na mtu huwa sisahau kilarahisi
 
Back
Top Bottom