TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI
Heche: Mwenyekiti, upo salama?
Lissu: Nipo salama. Ongeza moto, naona wameanza kutoana maini.
MAHAKAMA KICHEKO
Majaji wanaingia: “HIGH COOOOOOOOOURT!”
Mahakama inatulia na Majaji wanateta kidogo.
Lissu amesimama kizimbani na Mawakili wa Serikali wanajiandaa.
Kesi inasomwa: Jamhuri dhidi ya Tundu Lissu.
Mawakili Wakuu wa Serikali wanajitambulisha:
- Job Mrema
- Teddy Mwinnuka
- Tawabu Issa
- Kasara
- Nassoro Katuga
Lissu: Waheshimiwa, nipo tayari kuendelea. Na leo nipo na mashahidi wangu wote. Naomba watoke wakiwa tayari waje; naomba wasikae mbali.
Ananyanyuka John Heche, John Mnyika, Amani Golugwa na Brenda kutoka nje.
Jaji Ndunguru: Tuendelee.
Lissu: Asante, Waheshimiwa Majaji.
Jaji Ndunguru: Unakumbuka ulipoishia?
Lissu: Haitakuwa mbaya mkinikumbusha.
Jaji Ndunguru: Mara ya mwisho ulizungumzia mlipoenda sehemu mbalimbali, kama kwa Warioba na wetu wengine.
Lissu: Asante sana, Waheshimiwa Majaji. Leo nitazungumzia kuhusu mashitaka.
Sehemu ya kwanza nilizungumzia kuhusu mashahidi walioletwa Mahakamani.
Ni mashahidi wa namna gani na ushahidi wao upewe uzito wa namna gani. Hilo la kwanza.
La pili, la utangulizi, nilizungumzia kuhusu ushahidi uliozungumziwa na mashahidi wenyewe.
Na nitatoa ushahidi wangu kwamba ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka kwamba hakuna ushahidi na hakuna kosa lolote la jinai.
Nianze na mashahidi waliotoa ushahidi mbele ya Mahakama hii.
Waheshimiwa Majaji, wakati wa Preliminary Hearing, upande wa mashitaka ulileta orodha ya mashahidi 30.
Walisema hao ndiyo watakaotoa ushahidi wa kuthibitisha tuhuma za uhaini dhidi yangu.
Waheshimiwa Majaji, upande wa mashitaka haukuleta mashahidi hao 30; badala yake ulileta 17 pekee.
Hao 13 ambao hawakuletwa, hawakuletwa kwa sababu muhimu fulani.
Nitaelezea.
Hao mashahidi 13, hiyo omission, hawakuletwa siyo kwa sababu hawana maana na siyo kwa sababu hawana umuhimu.
Na nimesema nitaeleza kwa kifupi.
Katika mashahidi 17 walioletwa, mashahidi 8 ni askari Polisi.
Mashahidi 9 waliobaki ni mashahidi wa kificho.
Waheshimiwa Majaji, hao mashahidi 9 Mahakama haiwafahamu majina yao na haiwafahamu kabisa.
Haiwafahamu wanaishi wapi.
Haiwafahamu wanafanya kazi gani.
Haiwafahamu chochote zaidi ya majina waliopewa ya P1, P2, P3 na P nini.
Inaweza kuwa tumekuwa nao throughout kesi inaendelea.
Kwa sababu Mahakama haiwajui na upande wa utetezi hauwajui hata kidogo.
Kwa hiyo, ushahidi wa hao mashahidi 9 ni ushahidi wa watu wasiojulikana na Mahakama wala utetezi.
Watu pekee wanaowajua ni waendesha mashitaka, kwa sababu ndiyo waliowaleta.
Inawezekana ni mapolisi, inawezekana ni anyone, na hao ndiyo mashahidi wa kesi ya uhaini.
Mashahidi 8 ni mashahidi wa Jeshi la Polisi linaloongozwa na IGP Camillius Wambura na DCI Kingai, ambao nimeonyesha nina ugomvi nao binafsi (personal vendetta) kwa miaka 25. Vendetta ni neno la Kiitaliano lenye maana ya chuki.
Ushahidi wa mashahidi wa aina hiyo ndiyo ulipo Mahakamani dhidi yangu.
Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa shahidi namba 1 na namba 16, yaani PW1 na PW16, ni muhimu sana, Waheshimiwa Majaji, na ni muhimu siyo kwa sababu ya uzito wowote, lakini ni kwa sababu unaonyesha aina ya ushahidi ulioletwa.
Waheshimiwa Majaji, PW1, Assistant Commissioner of Police George Byagemu, Naibu Mkuu wa Upelelezi wa Kanda.
Upo hivi:
Kwamba yeye ndiye aliongoza upelelezi wa kesi hii, kuanzia tarehe 04 hadi 08 April.
PW1, kwa maneno mengine, shahidi alikuwa mpelelezi hadi siku moja kabla sijakamatwa, kwa sababu nilikamatwa tarehe 09 April.
PW1 alisema katika ushahidi wake in chief na aka-confirm katika cross-examination kwamba alikuwa anaongoza upelelezi kwa kuwasiliana moja kwa moja kupitia Deputy Commissioner of Police Ramadhani Ng’anzi.
Waheshimiwa Majaji, kwenye cross-examination nilimuuliza kama aliwahi kuwasiliana hata mara moja na Zonal Police Commanders. Akasema hapana.
His immediate boss.
Jaji Ndunguru: Zonal...?
Lissu: Zonal Police Commander.
Na akasema hapana.
Nilimuuliza kama aliwasiliana na DPP. Alisema hapana.
Kwa sababu DPP ndiye anaongoza kesi za jinai, na alisema hapana.
Nilimuuliza kama aliwasiliana na Regional Security Officer (Afisa Usalama wa Taifa Mkoa). Akasema hapana.
Kesi serious ya uhaini, ya kwanza kwa ukubwa.
Kama aliongea na mtu wa Ujasusi wa Mkoa, akasema hapana.
Mtu pekee aliyewasiliana naye ni DCI Kingai kupitia Deputy Commissioner of Police Ramadhani Ng’anzi.
Waheshimiwa Majaji, mtakumbuka PW1 alisema aliunda timu 3 katika upelelezi wake:
1. Timu ya Operesheni
2. Timu ya Intelijensia
3. Timu ya Ushauri
WEKA EMOJI KAMA UNAFUATILIA
NISAIDIE KUSHARE UJUMBE UFIKE MBALI.