TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI
Ni ushahidi wangu kwamba The Executive inaweza kuwa Rais kwa sababu Rais ni Chief Executive. Inaweza kuwa Vice President au Prime Minister, wote hao ni Executive.
Inaweza kuwa ni Ministers au Deputy Ministers, wote hao ni Executive.
Inaweza kuwa Regional au District Commissioners, wote hao ni Executive.
Waheshimiwa Majaji, Wakurugenzi wa Halmashauri wanaitwa Executive Directors. Kwa hiyo wanaweza kuwa wa Manispaa, wa Majiji; wao wote ni Executive.
Waheshimiwa Majaji, Executive wanaweza kuwa ni Watendaji wa Kata, wanaitwa Ward Executive Officers.
Executive wanaweza kuwa Village Executive Officers au Watendaji wa Mitaa, ambao wanaitwa Mtaa Executive Officers.
Na wanaweza kuwa ni Watendaji au Watumishi wowote wa Serikali ambao si Watendaji wa Mahakama au wa Bunge.
Kwa hiyo, kifungu cha 39(2)(d) kinachosema hivyo, ni ushahidi wangu kwamba kipo too broad.
Ukikosana na Mtendaji wa Kijiji upewe uhaini, hakuna atakayeponea. Kipo too broad.
Ndiyo maana hii kesi hawawezi kuthibitisha na wameshindwa kuthibitisha.
Umemtisha nani, Rais au mtendaji? Hakuna.
Ni ushahidi wangu kwamba kifungu hicho kilichotungwa specifically baada ya Makungu Matata, wakati wa chama kimoja, hakifai tena kuwepo katika sheria zetu. Ndiyo ushahidi wangu.
Waheshimiwa Majaji, kwenye ushahidi wa upande wa Mashitaka, hakuna shahidi hata mmoja aliyetoa ushahidi kwamba hiyo nia yangu ya kuitishia Serikali ilitekelezeka au la.
Hakuna aliyesema Serikali waliogopa sana. Ilikuwa hapakukalika siku hiyo.
Waheshimiwa Majaji, kukosekana kwa ushahidi huo kuna maana kubwa sana.
Ni ushahidi wangu kwamba kwenye kosa kama hili la uhaini, ambapo ni intention ya kosa, upande wa Mashitaka ulitakiwa waeleze matokeo ya hiyo intention.
Upelelezi wa kesi hii ulifanyika kienyeji enyeji sana, bila kuzingatia sheria.
Waheshimiwa Majaji, nilikamatwaje?
Wakati wa ukamataji, Waheshimiwa Majaji, Jeshi la Polisi liliendelea kufanya mambo kienyeji enyeji kwa kutokuzingatia sheria.
Waheshimiwa Majaji, nilikamatwa mji wa Mbinga, Mkoa wa Ruvuma, siku ya tarehe 09 April mwaka jana, majira ya saa 12 jioni.
Mimi ndiyo nilikuwa nahutubia mkutano huo wa hadhara.
Mikutano yetu inaisha saa 12. Kabla ya kumalizia mkutano, nilifuatwa na Polisi jukwaani. Simkumbuki jina, ila alijitambulisha kuwa ni OCD wa Mbinga.
Akaniambia kwamba, “Nakutaka kituoni sasa hivi,” jukwaani.
Nikamuuliza, “Unanitakia nini na nimefanya kosa gani?”
Akaniambia, “Wewe twende, utajua hayo mbele ya safari.”
Nikawambia, “Afande, hiyo siyo utaratibu wa kisheria wa nchi hii. Huna mamlaka ya kunipeleka kituoni kama huniambii kosa langu, na usiponiambia siendi.” Hivyo ndivyo nilivyomwambia.
Huyo Bwana OCD alishuka kwenye jukwaa, nikaendelea kuwaaga wananchi.
Nikasikia kishindo cha mabomu ya machozi.
Wakapiga watu kwa mabomu ya machozi mengi sana na wakapiga watu kwa virungu.
Na mimi sijui nilikamatwa vipi, ila nikajikuta katika gari ya Polisi, nimewekwa chini sakafuni na nimekanyagwa kwenye shingo.
Sikuwa peke yangu. Tulikuwa na wenzangu watatu. Tulipofika Polisi, walinipeleka kwenye Ofisi ya OC CID. Hawakunipeleka mahabusu. Sitatoa ushahidi wa uongo.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI