Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

TUNDU LISSU ANAHOJIWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI.

Nassoro Katuga: Inaposema mtu akitengeneza nia kwa dhumuni la kutishia Serikali, tafsiri kama mwanasheria, kuna takwa la kisheria kwamba lazima hiyo Serikali iwe imetishika au la?

Lissu: Una maana ya Section 39(2)(d)? Hakuna hiyo provision.

Lakini—

Nassoro Katuga: Hakuna cha “lakini”.

Lissu: Nataka nisaidie Mahakama, kwa sababu Kifungu cha 10(2)(d), kwamba panapokuwa na intention lazima kuwa na result.

Nassoro Katuga: Kwani umeshitakiwa na Kifungu cha 10?

Lissu: Hapana. Kifungu cha 10 kinasema ukishitakiwa kwa intention lazima kuwe na results.

Nassoro Katuga: Nilisikia unataka mashahidi wa Jeshi la Polisi kwamba wametumwa na IGP Wambura na Kingai.

Lissu: Nimesema wametumwa na Wambura.

Nassoro Katuga: Je, ni ushahidi wako kwamba wakati wanatumwa ulikuwepo?

Lissu: Hao wanafanya kazi chini ya Wambura na Kingai.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo hawa wametumwa na Wambura na DCI Kingai?

Lissu: Nilisema hawa wametumwa kwa maelekezo ya Wambura, na maelezo yapo Mahakamani katika ushahidi wao.

Nassoro Katuga: Ni kweli umewaita Wambura na Kingai?

Lissu: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo ni mashahidi wako?

Lissu: Siyo mashahidi wangu, ila ni mashahidi wanaojua ukweli.

Nassoro Katuga: Sawa, nitakuletea.

Lissu: Wewe hutowaleta, watakumbwa na Mahakama.

MAHAKAMA KICHEKO

Nassoro Katuga: Ulisema wakati unakamatwa au ukichukuliwa?

Lissu: Nilikamatwa.

Nassoro Katuga: Ulikamatwaje?

Lissu: Nyie ambao hamjawahi kukamatwa hamuwezi kujua.

Nassoro Katuga: Wewe unajuaje kama sijawahi kukamatwa?

Lissu: Nyie mnaofungulia watu mashtaka ya burebure, mnakamatwaje?

Nassoro Katuga: Kwa hiyo ulikamatwa au kukamatwa?

Lissu: Nilikamatwa.

Nassoro Katuga: Hebu turudi kwenye dhumuni la preliminary hearing.

Lissu: Ni kupembua masuala yanayobishaniwa na masuala yasiyobishaniwa.

Nassoro Katuga: Na wewe ulikuwepo katika preliminary hearing?

Lissu: Nilikuwepo.

Nassoro Katuga: Unajua kwamba mambo ambayo hayabishaniwi hayahitaji formal proof?

Lissu: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Ni kweli suala la wewe kukamatwa tarehe 09 na kuletwa Dar es Salaam ni suala ambalo halibishaniwi?

Lissu: Ni kweli.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Maintaining psychological advantage .
IQ ya Lisu ni kubwa sana.
Fikiria mpinzani wake pale mahakamani anakuwa na hali gani kuona mtu anaekabiliwa na kesi ambayo hukumu yake ni kifo, yuko happy 😁, laughing 😁, joking 😃
 
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Nassoro Katuga: Kwa kuwa hilo suala halikubishaniwa, wakati unawaambia Waheshimiwa kwamba hawakuletwa hawa mashahidi waliokukamata Mbinga kukuleta Dar es Salaam, hawa mashahidi wangekuja kufanya kitu gani?

Lissu: ASP Lugano Bwasi alikuwa amezungumza kuhusu uhalali wa kukamatwa kwangu. Nilitaka aje kuzungumza kuhusu uhalali wa kukamatwa.

Nassoro Katuga: Uliiambia Mahakama katika preliminary hearing kwamba unabisha hukukamatwa?

Lissu: Suala la kukamatwa na uhalali wa kukamatwa, it’s something else.

Nassoro Katuga: Unasema kwamba ni kweli tarehe 03 Aprili 2025 ulikuwa Mwenyekiti ambaye ulitoa hotuba kwa watia nia wa chama cha CHADEMA?

Lissu: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Pia ulisema ulitoa hotuba hii mbele ya waandishi wa habari?

Lissu: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kama ulitoa ushahidi wako kwamba uliwaambia waandishi wa habari wasitoe habari zile.

Lissu: Sikuwaambia.

Nassoro Katuga: Ukiwa unataka habari yake iende kwa walaji au hukutaka?

Lissu: Nilikuwa nataka.

Nassoro Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema ulitaka hotuba yako isambae kwa wananchi?

Lissu: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Katika ushahidi wako ukisema umetoa mipaka, huyu asikie na huyu asisikie?

Lissu: Sikuruhusu.

Nassoro Katuga: Wakati unatoa hotuba, wale uliokusudia kuongea nao walikuwa pale?

Lissu: Ni kweli, walikuwepo.

Nassoro Katuga: Waambie Waheshimiwa Majaji kwamba PW17 alisema walikuwa wanaonyesha moja kwa moja (live streaming).

Lissu: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Waambie Majaji kama uliwapa hotuba yako kabla hawajarusha live.

Lissu: Sikuwapa na sikuzungumza nao.

Nassoro Katuga: Ulichokuwa unaenda kuongea walikuwa hawajui?

Lissu: Ndiyo.

Nassoro Katuga: Ulikuwa umewapa ulichokuwa unaenda kuongea?

Lissu: Sikuwapa.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo, kwa kuwa walikuwa hawajui, nitakuwa sahihi nikisema haya maneno ya “tunaenda kuzuia uchaguzi”, “tunaenda kukinukisha” ni maneno PW17 walikuwa hawajui kama utaenda kuyasema?

Lissu: Walikuwa hawayajui.

Nassoro Katuga: Katika mashahidi wa Jamhuri, katika ushahidi wao katika ile video au kitu kinachoitwa video, walikuwa wanasema ulikuwa umevaa combat?

Lissu: Nilisikia.

Nassoro Katuga: Kuna sehemu yoyote uliyokanusha kwamba hukuwa umevaa combat?

Lissu: Nakanushaje na combat ni vazi langu?

Nassoro Katuga: Kwa hiyo, physical dress code yako ulikuwa umevaa hivyo?

Lissu: Ndiyo, vazi langu la siku zote.

Nassoro Katuga: Kwa hiyo ni sahihi mashahidi wa Jamhuri walikuwa sahihi katika kukutambua?

Lissu: Ndiyo, walinitambua.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE IWAFIKIE WATU WENGI ZAIDI
 
Aisee watu ni balaa

Mnaediti vitu hv tena?

Kuna sehemu amekiri kuwa "alisema atakinukisha"

Humu hamuandiki, mnamfariji nani?
 
TUNDU LISSU ANAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Nassoro Katuga: Unajua principle ya constructive? Construction, publication and constructive possession?

Lissu: Sifahamu, labda unielezee.

Nassoro Katuga: Katika sheria, mtu atakutwa na kitu fulani hata kama hakukutwa nacho, ilimradi anajua hicho kitu kiko wapi. Kitu cha Juma kimekutwa kwa Tundu.

Possession na control ya kitu.

Lissu: Hiyo najua.

Nassoro Katuga: Mtu ataonekana amepublish kwa kuwa amesababisha au ameruhusu kuwa published.

Lissu: Hiyo siyo kweli. Umesema utakuwa na control, sasa lazima uwe na control na hiyo publication.

Nassoro Katuga: Sasa unajua kuna kitu kinaitwa constructive publication?

Lissu: Hiyo sijui.

Nassoro Katuga: Kama nimekuelewa, umeiambia Mahakama hivi kwamba PW17 amesema yeye ndiye amechapisha ile video. Je, ni nani alisababisha publication?

Lissu: Ni PW17.

Nassoro Katuga: Angeweza kupublish au kutopublish, kwa hiyo ni yeye.

Nassoro Katuga: Kama unakumbuka vizuri ushahidi wa PW17, ulimuuliza swali akasema, “Tulipublish sisi kupitia wewe.”

Lissu: Ndiyo, alivyosema kama amepublish yeye kupitia mimi.

Sasa nyie mnasema nimepublish mimi.

Mmekuja pazuri.

Nassoro Katuga: Unapotoa hotuba kwa umma, si kila mtu ana haki ya kuitafsiri vile alivyoielewa?

Lissu: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Na kila mtu ana haki ya kuitekeleza alivyoielewa?

Lissu: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Maneno ya kwamba “tutazuia uchaguzi”, si kila mtu ana haki ya kuzuia kwa jinsi alivyoelewa?

Lissu: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Maneno ya “tutavuruga uchaguzi”, si kila mtu ana haki ya kuvuruga uchaguzi kwa vile alivyoelewa?

Lissu: Ni kweli.

Nassoro Katuga: Unakumbuka PW3 alivyosema kwamba alisema watazuia uchaguzi kwa kupiga mawe?

Lissu: PW3 ni Kahaya.

Nassoro Katuga: Samahani, ila unakumbuka? Namzungumzia PW13.

Lissu: Unamzungumzia shahidi namba ngapi?

Nassoro Katuga: PW13.

Lissu: Sawa.

Nassoro Katuga: Unakumbuka PW13 alisema walipanga kuzuia uchaguzi kwa kupiga watu mawe?

Lissu: Nakumbuka.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Mungu akupambanie kamanda
 
Mh, huu moyo mbona kama wa gas vile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…