Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

Huyu Lissu sisi tunamchukulia kawaida kwasababu yupo kwetu.

Huyu angekuwa Kenya ungeona namna wenzetu wangemtumia kama asset ya kui brand nchi yao.

Nchi nyingine tayari zingemtafutia specialist wa kukagua afya yake daily ili nchi iweze kufaidi akili yake kwa miaka mingi baadaye.

Huku sisi kwasababu tuna viongozi ndio kwanza yanamfunga gerezani.
 
Katuga ameanza kusahau ma
Katuga ameanza kusahau mashahidi wake mpaka akumbushwe na Lissu.
 
Naona Katuga anaruka hapa na pale. Kuna muda anasahau Hadi mashahidi wake Lissu anamsaidia. Kama Hana maswali akakae
 
Sisi huku akina dotto magari ndio wanaonekana wa maana. Nchi ya ajabu sana.
 
TUNDU LISSU NAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Lissu anasoma Ibara ya 30 ya Katiba.

Naasoro Katuga: Ibara hiyo inasema huwezi kumzuia mtu kupata haki yake kama haki ya kupiga kura. Bado unasema ni haki kumzuia mtu kupiga kura?

Lissu: Ndiyo, kikatiba, kwa njia za kikatiba, inaruhusiwa.

Naasoro Katuga: Nakukumbusha wewe ni kaka yangu kwamba ninachokifanya hakina nia yoyote binafsi zaidi ya kusaidia Mahakama.

Lissu: Unamshitaki mtu kwa uhaini, halafu unasema huna nia yoyote?

Mahakama: Kicheko.

Nassoro Katuga: Tafsiri ya Kifungu cha 39, kinaposema “shall be liable”.

Kifungu cha sheria kinapotumia “liable”, ni discretion ya Mahakama.

Lissu: Sheria inaposema “shall be liable”, hakuna discretion ya Mahakama.

In fact, Wakili, sheria inasema “shall be sentenced to death”, siyo “liable to death”.

Naasoro Katuga: Unasoma Revised ya mwaka gani?

Lissu: Ya mwaka 2022.

Nassoro Katuga: Kaka, kuna sheria revised ya 2023. Wewe unasoma ya mwaka 2022 kivipi? Unajua kwamba kuna sheria ya mwaka 2023?

Lissu: Sijui.

Nassoro Katuga: Unajua kwamba hii ya mwaka 2023 inasema “shall be liable”?

Nakuondoa kule unaposema “nanyongwa miii, nanyongwa miii”.

Umesoma Sentencing Manual?

Lissu: Sentencing Manual ni sheria?

Naasoro Katuga: Unajua ikitumika neno “shall be liable” ni discretion ya Mahakama?

Lissu: Nimesema sijui.

Nassoro Katuga: Upo aware na kesi ya Muhagama?

Lissu: Naijua, na nipo Mahakamani na wewe unasoma hapo mbele yangu katika mtandao.

Nassoro Katuga: Basi tafuta kesi ya Mangoma.

Lissu: Natafutaje na nipo gerezani?

Nassoro Katuga: Najua una ma-researcher wako. Nataja ili wakatafute kesi ya Mangoma kuhusu Mahakama kutumia neno “liable”.

Lissu: Ndiyo, useme. Waambie ma-researcher wakatafute. Usiseme nikatafute na unajua sina mtandao huko gerezani.

Naasoro Katuga: Unaweza kutupa tafsiri ya neno “liable”?

Lissu: Sina kamusi.

Naasoro Katuga: Unaweza kutupa tofauti ya maneno “mkanganyiko” na “kukanganyika”?

Lissu: Mkanganyiko maana yake ni mvurugano.

Nassoro Katuga: Tusaidie tafsiri ya Kifungu cha 163 cha Sheria ya Ushahidi kati ya “contradiction” na “omission”.

Lissu: “Omission” katika Kifungu cha 163 cha Sheria ya Ushahidi halipo.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Dah na mimi nisie lawyer ndio nimeelewa sasa maana nasoma tuu.

Ni kweli, ni kama vile ambavyo Lawyer hawezi elewa mwandiko wa Daktari, madaktari wao wanaelewana. Sheria ni taaluma kama zingine mkuu.

Kuhusu kesi: TL anataka kuidhibitishia mahakama hiyo kwamba, kati ya mashahidi wote 17, walioletwa na upande wa mashitaka. Ni Shahidi mmoja tuu ndie alikuwepo "eyewitness", ni mtu wa Jambo TV. Hapo anataka mahakama ione kwamba ushahidi wa hao watu (Mapolisi) pamoja na mavyeo yao sio "Credible" yaani hawakuwepo, na ushahidi wao hautoshi. Na nahisi kafanikiwa mpaka hapo. Ni punch ya maana hiyo kwenye mchezo wa sheria ya ushahidi. 😊

Ndio utaona Wakili wa Serikali, anampitisha kwenye mambo ya kumuingiza kingi, za kombati sijui vitu gani. Hiyo tayari ni uppercut, katika mchezo wa ngumi, hata kama mpinzani hajaanguka "knocked out " lazima refa akuhesabie pointi zako ubaoni. 😊
 
sasa mkuu kiongozi la 3 b ataipenda akili kubwa kama hii

shabiki wa kiongozi ni chawa anasifia alipwe buku 2-3 ataipenda akili hii

yaani ukiwa ujasoma unakuwa na chuki na walio soma kama kwamba wao ndio walikuzuia usisome ama usiwe na akili
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…