Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

Ni kweli, ni kama vile ambavyo Lawyer hawezi elewa mwandiko wa Daktari, madaktari wao wanaelewana. Sheria ni taaluma kama zingine mkuu.

Kuhusu kesi: TL anataka kuidhibitishia mahakama hiyo kwamba, kati ya mashahidi wote 17, walioletwa na upande wa mashitaka. Ni Shahidi mmoja tuu ndie alikuwepo "eyewitness", ni mtu wa Jambo TV. Hapo anataka mahakama ione kwamba ushahidi wa hao watu (Mapolisi) pamoja na mavyeo yao sio "Credible" yaani hawakuwepo, na ushahidi wao hautoshi. Na nahisi kafanikiwa mpaka hapo. Ni punch ya maana hiyo kwenye mchezo wa sheria ya ushahidi. 😊

Ndio utaona Wakili wa Serikali, anampitisha kwenye mambo ya kumuingiza kingi, za kombati sijui vitu gani. 😊
Ni kweli, ila shida ni kwamba walimtambua kwenye Video sio live. Hapo ndipo Katuga anapata mkwamo.
 
TUNDU LISSU NAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Lissu anasoma Ibara ya 30 ya Katiba.

Naasoro Katuga: Ibara hiyo inasema huwezi kumzuia mtu kupata haki yake kama haki ya kupiga kura. Bado unasema ni haki kumzuia mtu kupiga kura?

Lissu: Ndiyo, kikatiba, kwa njia za kikatiba, inaruhusiwa.

Naasoro Katuga: Nakukumbusha wewe ni kaka yangu kwamba ninachokifanya hakina nia yoyote binafsi zaidi ya kusaidia Mahakama.

Lissu: Unamshitaki mtu kwa uhaini, halafu unasema huna nia yoyote?

Mahakama: Kicheko.

Nassoro Katuga: Tafsiri ya Kifungu cha 39, kinaposema “shall be liable”.

Kifungu cha sheria kinapotumia “liable”, ni discretion ya Mahakama.

Lissu: Sheria inaposema “shall be liable”, hakuna discretion ya Mahakama.

In fact, Wakili, sheria inasema “shall be sentenced to death”, siyo “liable to death”.

Naasoro Katuga: Unasoma Revised ya mwaka gani?

Lissu: Ya mwaka 2022.

Nassoro Katuga: Kaka, kuna sheria revised ya 2023. Wewe unasoma ya mwaka 2022 kivipi? Unajua kwamba kuna sheria ya mwaka 2023?

Lissu: Sijui.

Nassoro Katuga: Unajua kwamba hii ya mwaka 2023 inasema “shall be liable”?

Nakuondoa kule unaposema “nanyongwa miii, nanyongwa miii”.

Umesoma Sentencing Manual?

Lissu: Sentencing Manual ni sheria?

Naasoro Katuga: Unajua ikitumika neno “shall be liable” ni discretion ya Mahakama?

Lissu: Nimesema sijui.

Nassoro Katuga: Upo aware na kesi ya Muhagama?

Lissu: Naijua, na nipo Mahakamani na wewe unasoma hapo mbele yangu katika mtandao.

Nassoro Katuga: Basi tafuta kesi ya Mangoma.

Lissu: Natafutaje na nipo gerezani?

Nassoro Katuga: Najua una ma-researcher wako. Nataja ili wakatafute kesi ya Mangoma kuhusu Mahakama kutumia neno “liable”.

Lissu: Ndiyo, useme. Waambie ma-researcher wakatafute. Usiseme nikatafute na unajua sina mtandao huko gerezani.

Naasoro Katuga: Unaweza kutupa tafsiri ya neno “liable”?

Lissu: Sina kamusi.

Naasoro Katuga: Unaweza kutupa tofauti ya maneno “mkanganyiko” na “kukanganyika”?

Lissu: Mkanganyiko maana yake ni mvurugano.

Nassoro Katuga: Tusaidie tafsiri ya Kifungu cha 163 cha Sheria ya Ushahidi kati ya “contradiction” na “omission”.

Lissu: “Omission” katika Kifungu cha 163 cha Sheria ya Ushahidi halipo.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Dah mamaeee aloooh 😀😀
 
Anajaribu kutengenwza njia ya kugeuza hoja hili aje aseme vazi hilo ni la kijeshi, wewe umelitoa wapi....? Lakini LISSU mjanja kawaelewa mapema sana upuuzi wao

Hataweza asilani! Huyo aliepo mbele yake ni "Learned Brother". Sio kiazi, ni mtu ambaye maisha yake ni sheria. Kumtwisti, kumjaza ni ngumu sana. 😊
 
CCM sijui akili zao zikoje. Wanadhani neno "Kukinukisha" ni kosa kisheria .

Kwani kwa Sheria gani mtu akisema kukinukisha anakuwa ametenda kosa?

..wahaini kama Hatibu Gandhi, Hans Poppe, na wenzao walikuwa wamepanga njama kweli kweli.

..walikwenda mbali mpaka kujaribu ku recruit wanajeshi wakiwemo makomandoo.

..walipanga mpaka namna ya kugawiana madaraka.

..walipanga kuuwa baadhi ya viongozi na walikuwa wanafuatilia nyendo zao, wapi watatekeleza njama zao.

..mashahidi wa upande wa mashtaka walikuwa watu wazito kwelikweli.

..kuna mpaka Brigedia Jenerali alikwenda kutoa ushahidi upande wa mashtaka.

..kuna Komandoo mmoja waliyejaribu kum-recruit alitoa ushahidi. Na huyu mwanajeshi ni mmoja kati ya makomando wakufunzi wenye jina kubwa jeshini. Nadhani alikuja kustaafu na cheo cha Brigedia Jenerali.

..Tumeishakuwa na majaribio ya uhaini huko nyuma. Na tunajua uhaini unafananaje.

..Kwa maoni yangu, Tundu Lissu anaonewa kwa kushtakiwa kwa uhaini.
 
TUNDU LISSU ANAHOJIWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Nassoro Katuga: Isaidie Mahakama hii tukufu kuhusu sheria ya kupinga sheria ya uchaguzi. Kama kwa jina lako ulishawahi kufungua kesi ya uchaguzi?

Lissu: Kwa jina langu hapana, ila kwa chama changu hapana.

Nassoro Katuga: Nimekuuliza kwa jina lako.

Lissu: Naweza kufungua kwa jina langu au through organization.

Nassoro Katuga: Hayo mengine ni ya kwako, mie nimekuuliza jina lako.

Nassoro Katuga: Nimesikia umezungumza ya Jaji Chande sana.

Lissu: Yep, sasa kuna ya Jaji Chande ya haki jinai na October 29.

Nassoro Katuga: Ya October 29 nazungumzia. Ni kweli Tume imesema kuna matukio yalipangwa kabla?

Lissu: Ndiyo.

Lissu: Yalipangwa kuhusu Tume ya Uchaguzi na Katiba mpya.

Nassoro Katuga: Shahidi Tulia, kuna neno nilitaka kulisema ila nakuheshimu.

Lissu: Unaniheshimu wapi wakati unanishitaki ili ninyongwe?

Mahakama: Kicheko.

Nassoro Katuga: Nilisikia kuhusu Tume hiyo hiyo kuna sehemu imezungumzia kuhusu matukio ya October 29 yalipangwa kabla.

Lissu: Labda unikumbushe.

Nassoro Katuga: Katika hotuba yako kuna sehemu tukinukisha, watatuua?

Lissu: Hiyo sikumbuki.

Nassoro Katuga: Kuna sehemu ulisema sana sana, watanikamata, watanifungulia kesi ya uhaini?

Lissu: Hiyo sikumbuki.

Nassoro Katuga: Ulisema Majaji ni CCM?

Lissu: Hiyo nakumbuka.

Nassoro Katuga: Kuna sehemu umesema Mahakamani hakuendeki?

Lissu: Hiyo nimesema.

Nassoro Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema hapo ndiyo nia yako ilianza kujengwa? (Anacheka).

Lissu: Hapana. Kama ingekuwa kwamba sasa tuingie mtaani tuchukue dola, ingekuwa katika hati yenu ya mashitaka.

Nassoro Katuga: Nataka kuomba vielelezo, lakini naona tayari ni saa 11 na bado ndiyo kwanza tupo nusu.

Majaji wanateta.

Mawakili wa Serikali wanateta.

Lissu anapanga vitu vyake.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Naona Katuga anaruka hapa na pale. Kuna muda anasahau Hadi mashahidi wake Lissu anamsaidia. Kama Hana maswali akakae
Naamini mshahara wa mwezi huu atauchukua akiwa amehenyeka *******.

Huu ndio aina ya mshahara ambao mtu akiomba umkope unamuona mdwanzi asiye na haya.

Kwa mara ya kwanza kwenye kesi hii nikimuona Katuga anaomba hairisho naweza nikamuelewa.

This guy's been going through some real shit, man. He just needs a few days to cool his ass down.

I can't imagine putting myself in his position, this could be the toughest job in the World.
 
Huyo Wakili wa Serikali anawalia hela tuu akina Samia! 😊
Na ndio kiongozi kwenye hilo jopo, mpaka sasa sijaona swali lolote lenye "merit" kwenye ushahidi. Kumuuliza mtu kuhusu kombati ambalo ni vazi la chama chake na kama alitambuliwa na mashahidi, hasa wale mapolisi ni akili ndogo. 😊
Hakuna mtu hawezi tambua kombati za Chadema.

Kwa tunaofuatilia: Muuliza swali, anataka aipangue hoja ile ya Lissu, ya "eyewitness", TL katika utetezi wake huko juu kaeleza kwamba ni shahidi mmoja tuu ndiye "Eyewitness", yaani alikuwepo. Na ni mtu wa Jambo TV. The rest katika mshahidi upande wa mashitaka walitazama kupitia Video, ni "Hearsay" au "watchers from a distanc" ambao walitegemea video. Kama mimi hapa.

Video ambayo TL, amesema wazi ilikuwa ndefu, ila wao waliiona kwa dakika chache. Video hiyo TL pia kasema haijaletwa hapo Mahakamani. Hii mbinu ya TL ni nzuri sana. 😊

Hilo ni pigo kubwa sana kwa Mashitaka, sababu mashitaka yao yamejikita kwenye video. Ndio hapo utaona Wakili wa Serikali anataka kulazimisha utambuzi (Hasa kwa wale mashahidi/mapoti) kupitia video, yaani wale mashahidi ambao hawakuwepo, walimtambua kupitia video. Kwa namna nyinyine TL, anakusudia ku disqualify hao ambo hawakuwepo, na kafanikiwa nahisi. Jamaa kweli ni wakili mzuri.

Tayari TL amechimba shimo "poking a hole" kwenye jamvi kwa kete hiyo, kisheria hiyo ni maksi. Ku challenge ushahidi na shahidi. Tuendelee kufuatilia. 😊

Ulikuwepo? Uliona nini? Ulisikia nini? Ndicho TL anachosisitiza hapo. 😊
Kweli mkuu. Lissu amejitahidi kutembea na Katuga pole pole. Mpaka Sasa sijaona jipya la Katuga.
 
Back
Top Bottom