TUNDU LISSU NAULIZWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI
Lissu anasoma Ibara ya 30 ya Katiba.
Naasoro Katuga: Ibara hiyo inasema huwezi kumzuia mtu kupata haki yake kama haki ya kupiga kura. Bado unasema ni haki kumzuia mtu kupiga kura?
Lissu: Ndiyo, kikatiba, kwa njia za kikatiba, inaruhusiwa.
Naasoro Katuga: Nakukumbusha wewe ni kaka yangu kwamba ninachokifanya hakina nia yoyote binafsi zaidi ya kusaidia Mahakama.
Lissu: Unamshitaki mtu kwa uhaini, halafu unasema huna nia yoyote?
Mahakama: Kicheko.
Nassoro Katuga: Tafsiri ya Kifungu cha 39, kinaposema “shall be liable”.
Kifungu cha sheria kinapotumia “liable”, ni discretion ya Mahakama.
Lissu: Sheria inaposema “shall be liable”, hakuna discretion ya Mahakama.
In fact, Wakili, sheria inasema “shall be sentenced to death”, siyo “liable to death”.
Naasoro Katuga: Unasoma Revised ya mwaka gani?
Lissu: Ya mwaka 2022.
Nassoro Katuga: Kaka, kuna sheria revised ya 2023. Wewe unasoma ya mwaka 2022 kivipi? Unajua kwamba kuna sheria ya mwaka 2023?
Lissu: Sijui.
Nassoro Katuga: Unajua kwamba hii ya mwaka 2023 inasema “shall be liable”?
Nakuondoa kule unaposema “nanyongwa miii, nanyongwa miii”.
Umesoma Sentencing Manual?
Lissu: Sentencing Manual ni sheria?
Naasoro Katuga: Unajua ikitumika neno “shall be liable” ni discretion ya Mahakama?
Lissu: Nimesema sijui.
Nassoro Katuga: Upo aware na kesi ya Muhagama?
Lissu: Naijua, na nipo Mahakamani na wewe unasoma hapo mbele yangu katika mtandao.
Nassoro Katuga: Basi tafuta kesi ya Mangoma.
Lissu: Natafutaje na nipo gerezani?
Nassoro Katuga: Najua una ma-researcher wako. Nataja ili wakatafute kesi ya Mangoma kuhusu Mahakama kutumia neno “liable”.
Lissu: Ndiyo, useme. Waambie ma-researcher wakatafute. Usiseme nikatafute na unajua sina mtandao huko gerezani.
Naasoro Katuga: Unaweza kutupa tafsiri ya neno “liable”?
Lissu: Sina kamusi.
Naasoro Katuga: Unaweza kutupa tofauti ya maneno “mkanganyiko” na “kukanganyika”?
Lissu: Mkanganyiko maana yake ni mvurugano.
Nassoro Katuga: Tusaidie tafsiri ya Kifungu cha 163 cha Sheria ya Ushahidi kati ya “contradiction” na “omission”.
Lissu: “Omission” katika Kifungu cha 163 cha Sheria ya Ushahidi halipo.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI