Kesi ya Uhaini: Tundu Lissu kuhitimisha ushahidi Mkuu leo, Agosti 26, 2026 Mahakamani

Ni kweli, ila shida ni kwamba walimtambua kwenye Video sio live. Hapo ndipo Katuga anapata mkwamo.
 
Dah mamaeee aloooh πŸ˜€πŸ˜€
 
Anajaribu kutengenwza njia ya kugeuza hoja hili aje aseme vazi hilo ni la kijeshi, wewe umelitoa wapi....? Lakini LISSU mjanja kawaelewa mapema sana upuuzi wao

Hataweza asilani! Huyo aliepo mbele yake ni "Learned Brother". Sio kiazi, ni mtu ambaye maisha yake ni sheria. Kumtwisti, kumjaza ni ngumu sana. 😊
 
CCM sijui akili zao zikoje. Wanadhani neno "Kukinukisha" ni kosa kisheria .

Kwani kwa Sheria gani mtu akisema kukinukisha anakuwa ametenda kosa?

..wahaini kama Hatibu Gandhi, Hans Poppe, na wenzao walikuwa wamepanga njama kweli kweli.

..walikwenda mbali mpaka kujaribu ku recruit wanajeshi wakiwemo makomandoo.

..walipanga mpaka namna ya kugawiana madaraka.

..walipanga kuuwa baadhi ya viongozi na walikuwa wanafuatilia nyendo zao, wapi watatekeleza njama zao.

..mashahidi wa upande wa mashtaka walikuwa watu wazito kwelikweli.

..kuna mpaka Brigedia Jenerali alikwenda kutoa ushahidi upande wa mashtaka.

..kuna Komandoo mmoja waliyejaribu kum-recruit alitoa ushahidi. Na huyu mwanajeshi ni mmoja kati ya makomando wakufunzi wenye jina kubwa jeshini. Nadhani alikuja kustaafu na cheo cha Brigedia Jenerali.

..Tumeishakuwa na majaribio ya uhaini huko nyuma. Na tunajua uhaini unafananaje.

..Kwa maoni yangu, Tundu Lissu anaonewa kwa kushtakiwa kwa uhaini.
 
TUNDU LISSU ANAHOJIWA MASWALI YA DODOSO MAHAKAMANI

Nassoro Katuga: Isaidie Mahakama hii tukufu kuhusu sheria ya kupinga sheria ya uchaguzi. Kama kwa jina lako ulishawahi kufungua kesi ya uchaguzi?

Lissu: Kwa jina langu hapana, ila kwa chama changu hapana.

Nassoro Katuga: Nimekuuliza kwa jina lako.

Lissu: Naweza kufungua kwa jina langu au through organization.

Nassoro Katuga: Hayo mengine ni ya kwako, mie nimekuuliza jina lako.

Nassoro Katuga: Nimesikia umezungumza ya Jaji Chande sana.

Lissu: Yep, sasa kuna ya Jaji Chande ya haki jinai na October 29.

Nassoro Katuga: Ya October 29 nazungumzia. Ni kweli Tume imesema kuna matukio yalipangwa kabla?

Lissu: Ndiyo.

Lissu: Yalipangwa kuhusu Tume ya Uchaguzi na Katiba mpya.

Nassoro Katuga: Shahidi Tulia, kuna neno nilitaka kulisema ila nakuheshimu.

Lissu: Unaniheshimu wapi wakati unanishitaki ili ninyongwe?

Mahakama: Kicheko.

Nassoro Katuga: Nilisikia kuhusu Tume hiyo hiyo kuna sehemu imezungumzia kuhusu matukio ya October 29 yalipangwa kabla.

Lissu: Labda unikumbushe.

Nassoro Katuga: Katika hotuba yako kuna sehemu tukinukisha, watatuua?

Lissu: Hiyo sikumbuki.

Nassoro Katuga: Kuna sehemu ulisema sana sana, watanikamata, watanifungulia kesi ya uhaini?

Lissu: Hiyo sikumbuki.

Nassoro Katuga: Ulisema Majaji ni CCM?

Lissu: Hiyo nakumbuka.

Nassoro Katuga: Kuna sehemu umesema Mahakamani hakuendeki?

Lissu: Hiyo nimesema.

Nassoro Katuga: Nitakuwa sahihi nikisema hapo ndiyo nia yako ilianza kujengwa? (Anacheka).

Lissu: Hapana. Kama ingekuwa kwamba sasa tuingie mtaani tuchukue dola, ingekuwa katika hati yenu ya mashitaka.

Nassoro Katuga: Nataka kuomba vielelezo, lakini naona tayari ni saa 11 na bado ndiyo kwanza tupo nusu.

Majaji wanateta.

Mawakili wa Serikali wanateta.

Lissu anapanga vitu vyake.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Naona Katuga anaruka hapa na pale. Kuna muda anasahau Hadi mashahidi wake Lissu anamsaidia. Kama Hana maswali akakae
Naamini mshahara wa mwezi huu atauchukua akiwa amehenyeka *******.

Huu ndio aina ya mshahara ambao mtu akiomba umkope unamuona mdwanzi asiye na haya.

Kwa mara ya kwanza kwenye kesi hii nikimuona Katuga anaomba hairisho naweza nikamuelewa.

This guy's been going through some real shit, man. He just needs a few days to cool his ass down.

I can't imagine putting myself in his position, this could be the toughest job in the World.
 
Kweli mkuu. Lissu amejitahidi kutembea na Katuga pole pole. Mpaka Sasa sijaona jipya la Katuga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…