Inaitwa Kachags twende hii..anazidi kuchanganya...TUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI
Katika hizo timu 3, timu ninayotaka kutolea ushahidi ni Timu ya Operesheni, ndiyo ilikuwa inahusika na ukamataji.
Nilimuuliza swali: Je, ni wewe ndiyo uliamuru nikamatwe? Akasema hapana.
Kiongozi Mkuu wa Timu ya Operesheni, nikamuuliza: Unafahamu ni nani aliamuru nikamatwe? Jibu lake ni hapana.
Nikamuuliza ilikuwaje nikakamatwa, na jibu lake likawa nilipigiwa simu na DCP Ramadhani Ngβanzi kuwa mtuhumiwa amekamatwa Mbinga na anasafirishwa kuletwa Dar es Salaam.
Sasa, Waheshimiwa Majaji, huyo aliyetoa taarifa kwamba nimekamatwa ni DCP Ramadhani Ngβanzi, ambaye anasema ndiye aliyemuunganisha na DCI Ramadhani Kingai na, presumably, Camilius Wambura.
Kwa hiyo, ni ushahidi wangu kwamba nilikamatwa kwa maelekezo ya DCI Ramadhani Kingai na, presumably, Camilius Wambura, ambao kwa miaka kadhaa wamekuwa na mikakati ya kujaribu kunifunga.
Waheshimiwa Majaji, hayo aliyoyasema PW1 yalithibitishwa substantially na PW16, Assistant Commissioner of Police Amini Mahamba.
Waheshimiwa Majaji, mashahidi wengine wa Polisi ni PW2, PW3, PW6, PW9, PW12 na PW15.
Ushahidi wao wote kwa ujumla wao ni ushahidi wa watu wa Ramadhani Kingai na Camilius Wambura.
Maafisa wa Polisi ambao wakubwa wao wamekuwa na mikakati ya kunifunga kwa miaka 24.
Nitakapofanya majumuisho ya ushahidi huu (final submission), ushahidi wa mashahidi hawa ni legally worthless.
Ushahidi ambao hauna thamani.
Unahitaji kuthibitishwa na mashahidi huru.
Jaji Ndunguru: Sasa si umesema utaleta baadaye?
Lissu: Ndiyo, nitaleta baadaye, nitaleta baadaye.
Sasa naomba kuzungumzia ushahidi wa mashahidi ambao hawakuwa Polisi: PW4, PW5, PW7, PW8, PW10 na PW17. Hao ndiyo mashahidi ambao hakuna anayewajua isipokuwa ma-Prosecutor.
Mashahidi hawa wote tuna ushahidi wao wa maandishi na ushahidi wa mdomo wakiwa hapa niliposimama.
Na, in bracket, hata mashahidi wa Polisi wote isipokuwa PW1, lakini wote tuna ushahidi wao wa maandishi.
Sasa nirudi kwa hawa mashahidi wa kificho, Waheshimiwa Majaji.
Waheshimiwa Majaji, ukimuachia PW4, wengine wote 7, that is, walisema hivi kwa maandishi na wakiwa kizimbani hapa:
1. βWalipanga njama za kufanya uhalifu wakati wa Uchaguzi Mkuu wa mwaka...β kwa maelezo yao Polisi.
Jaji Ndunguru: Walifanya?
Lissu: Walisema kwamba walipanga kufanya vurugu, kuchoma vituo vya Polisi, kupiga Polisi.
Na hayo maelezo yao ni utetezi kwangu.
Na wote hao, ukiachilia PW4, wote walikamatwa na Polisi.
Na wote walikamatwa katika hizo siku 4 za kati ya tarehe 04 na 08 April. Polisi walikuwa wanawajua na wakawakamata within 4 days.
Jambo la tatu: Wote hawa, baada ya kukamatwa na Polisi, walikiri mbele ya Polisi (waliconfess) kwamba tunapanga kufanya uhalifu, kwa maandishi na wakiwa kizimbani.
Na jambo la nne: Wote waliachiwa ili wakaendelee kupanga njama.
La tano: Wote waliitwa na Polisi na kuambiwa: βKubalini muwe mashahidi dhidi ya Tundu Lissu.β
Na mkikubali kuwa mashahidi dhidi ya Tundu Lissu, tunafuta mashitaka yenu.
Na wote walifutiwa mashitaka yao.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE UJUMBE UFIKE MBALI
Haya Mkuu..tumeacha....nyie endeleeni kuteka watu hiyo ni haki ya Binadamuunampotosha mdau innocent kabisa wa JF gentleman, plz acheni kuvunja haki za binadamu namna hiyo gentleman π
huna haja ya kubabaika na porojo gentleman πHaya Mkuu..tumeacha....nyie endeleeni kuteka watu hiyo ni haki ya Binadamu
Ngoja tuone moto unavyowashwajamaa anapiga spana sana, yaani kesi kubwa ya jinai lakini mtu hawasiliani na watu wa usalama
Utaelewa tuππππ
Ni wach1che wenye memory capacity kunwa kama huyu mwambaHuyu mtu ni kama ana kamemory card kichwan sio kwa kukumbuka yote hayo. Mungu atasimama na wewe lissu na wote waliokufanyia huo uhuni wajue kwamba barabara ya kwenda mbinguni haipiti kwao.
HahhahHilo ni tatizo kiutendaji...tena kubwa....,'Uviziaje/Opportunist'..badala ya kusimamia Sheria na Misingi ya kazi...
Moja ya Tatizo kubwa sana lililotengenezwa na CCM.
Huyo Jamaa Ubongo wake ni 1000TBNi wach1che wenye memory capacity kunwa kama huyu mwamba
Dragon mzeeTUNDU LISSU ANAENDELEA KUJITETEA MAHAKAMANI
Ambapo Dar es Salaam waliuawa watu zaidi ya 300 katika uchaguzi wa Oktoba mwaka jana.
Na wawili, PW5 na PW10, walitoka Arusha, na huko Arusha, kwa mujibu wa Jaji Chande, waliuawa watu 53.
Na wawili walitoka Mbeya, ambapo kwa mujibu wa Jaji Othman Chande, huko Mbeya waliuawa watu 80.
Songea walitoka mashahidi wawili, PW5 na PW7, na kwa mujibu wa Tume ya Jaji Othman Chande, Songea pia waliuawa watu, lakini idadi yake hawakuitaja.
Waheshimiwa Majaji, PW16, ACP Amini Mahamba, mbele ya Mahakama hii alisema yeye alikuwa katika timu ya upelelezi ya matukio ya mauaji ya Oktoba 29.
Nikamuuliza, hawa waliosema watafanya fujo, na fujo zikatokea, watu wakauwawa namna hii, mmewachukulia hatua yoyote? Jibu lake lilikuwa: Hapana.
Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa wahalifu wa namna hii una uzito kiasi gani kisheria?
Huu ndiyo ushahidi wa Serikali dhidi yangu.
Ushahidi wa mashahidi waliokiri uhalifu, wakakamatwa, wakakiri, wakaachiwa, wakarudi katika maeneo yao kufanya uhalifu na watu wakauwawa, ni ushahidi wa namna gani?
Ushahidi wa namna hii, kwa kusema kwa pole, ni totally unsafe and totally unreliable.
Waheshimiwa Majaji, shitaka dhidi yangu linasema kwamba nilitengeneza nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Na nikathibitisha (manifest) nia hiyo kwa kutamka yale maneno maarufu.
Sasa, Waheshimiwa Majaji, kuhusiana na shitaka hili na kwa mujibu wa maamuzi ya kisheria ambayo tumeyazungumza sana mbele yenu ya Grey, Makungu na Ghandi.
Kuhusu utiifu kwa Serikali, hilo halina mjadala.
Lakini zinasemaje kuhusu nia ya kutenda kosa la uhaini?
Kwenye hoja hii, Waheshimiwa Majaji, mashahidi waliotoa ushahidi kuthibitisha ni PW1 George Byagemu, PW2 Inspector John Kahaya, PW16 ACP Amini Mahamba na PW17, mwandishi wa habari.
Waheshimiwa Majaji, kwa ridhaa yenu, naomba nipatiwe vielelezo D1, D15 na D16.
Waheshimiwa Majaji, kielelezo D1 ni maelezo ya onyo ya PW2 John Kahaya.
Jaji Ndunguru: Twende taratibu.
Lissu: Nimesema nipatiwe kielelezo D1, maelezo ya John Kahaya, na D15, maelezo ya Amini Mahamba, na maelezo ya shahidi wa 17.
Jaji Ndunguru: Umeshapewa?
Lissu: Sinapewa bado.
Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka mnalolote?
Mawakili wa Serikali: Apewe, Mheshimiwa.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, PW1 ni shahidi pekee ambaye maelezo yake hayakuwasilishwa Mahakamani.
Waheshimiwa Majaji, PW1 katika ushahidi wake alisema mimi nimetengeneza nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kuhamisha, kusimamisha uchaguzi, na kwamba Serikali ndiyo inasimamia uchaguzi, kwa hiyo akaona nia katika inayodaiwa kuwa kauli niliyoitoa.
Waheshimiwa Majaji, shahidi mwingine aliyeona nia hiyo ni PW16 Amini Mahamba.
Waheshimiwa Majaji, kwenye kielelezo D15, maelezo yake ya onyo Polisi alisema maneno yafuatayo:
βKuonyesha kwamba nilikuwa na nia ya kutenda hilo kosa la uhaini.β
βMimi pamoja na timu nzima ya upelelezi tuliitizama na kusikikiza video hiyo, ndiyo tulipobaini kuna makosa ya jinai, kosa la kwanza ni uhaini na kuchapisha na kusambaza taarifa za uongo.β
Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga: Samahani, Waheshimiwa Majaji, kielelezo hiki kimepokelewa kwa mujibu wa kifungu 163 cha Sheria ya Ushahidi kuanza kurejea na kutumia kama content yake itakuwa ina contradict, kwa sababu kilitumika kwa mazingira maalumu.
Sasa anakirejea kwa misingi ipi na sisi tunakitumia dhidi yake?
Kama anachokifanya ni sahihi kwa uelewa wake wa sheria, itakula pande zote mbili.
Mimi nilidhani anacontradict tu kielelezo.
Sasa yeye anakisoma baada ya kuwa kimepokelewa. Je, kwa misingi ipi?
Sisi tunataka kukitumia kielelezo hiki dhidi yake.
Tunaomba Mahakama itoe mwongozo.
Waheshimiwa, ni hayo tu.
(Anakaa chini.)
Anasimama tena Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga:
Waheshimiwa, ni kwamba ilikuwa ni kwa ajili ya ku-contradict.
Lissu: Nianze kwa wao kusema itakuwa furaha. Mimi nitakuwa more happy wakikitumia.
Wanasema watakitumia pia dhidi yangu, sasa mimi nasema Mahakama itoe ruhusa wao wakitumie dhidi yangu.
Waheshimiwa Majaji, kielelezo kilitengenezwa kwa ajili ya kesi hii.
Hawakutaka kisomwe ili nisiweze kumuhoji shahidi wao, ila Mahakama ilishakipokea na kielelezo kipo kwa ajili ya ushahidi.
Kama kielelezo kipo kwa ajili ya kesi, nitakitumia kwa ajili ya kesi.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Huyo Jamaa Ubongo wake ni 1000TNi wach1che wenye memory capacity kunwa kama huyu mwamba
Jamaa ana kumbukumbu kana kwamba hata ukiwa na Nondo unasoma wewe utakosea ila yeye atapata,π€£Huyu mtu ni kama ana kamemory card kichwan sio kwa kukumbuka yote hayo. Mungu atasimama na wewe lissu na wote waliokufanyia huo uhuni wajue kwamba barabara ya kwenda mbinguni haipiti kwao.
Umemwona? Kazi sana! wao ndio wafungwa wa muda wote hawana furaha kabisaafande anatamani kucheka ila ndo haiwezekani
Mkata viuno wa lumumba buku7fc lissu sio mhaini mhaini NI samuya na genge lake walifanya mapinduzi Kisha wakajiapisha na waliuwa watanganyika wasiokua na idadiaah,
kibaraka kaja kumalizia hotuba zake za kuaga ndugu, jamaa na marafiki kabla ya kuhukumiwa kifungo jela na kunyongwa hadi kufa, right?π
Huyo jamaa kama mimi sema amenizidi attention yake hata kwenye mazingira kama hayo mimi nisingetoboa, lakini kwa kumbukumbu nipo vizuri hasa za maongezi kati yangu na mtu huwa sisahau kilarahisiHuyo Jamaa Ubongo wake ni 1000T
Jamaa ana kumbukumbu kana kwamba hata ukiwa na Nondo unasoma wewe utakosea ila yeye atapata,π€£
ok.πUtaelewa tuπππ
Wewe unafanya nini kwenye uzi huu?huna haja ya kubabaika na porojo gentleman π
ok.π