GE2025 Kesi ya Uhaini ya Lissu yaahirishwa tena Mahakama ya Kisutu, hadi Julai 30, 2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Wakuu!

Mwenyekiti CHADEMA Taifa Tundu Lissu kufikishwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kwa ajili kesi ya Uhaini inayomhusu.

Kumbuka kwamba kwenye kesi hii Tundu Lissu anajitetea mwenyewe.

Je, leo mwamba anaachiwa au atarudishwa tena 'kukamilisha na kumalizia kabisa kabisa kabisaaaa upelelezi?'

Wacha tuone kitakachojiri!

Kesi ya uhaini inayomkabili Lissu kutajwa tena leo Julai 15, uamuzi wa DPP kungojewa

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Antiphas Lissu inaendelea leo Julai 15, 2025 ikiwa ni siku 14 tokea iliposikilizwa mara ya mwisho, ambapo unangojewa uamuzi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutokana na jalada ambalo ilielezwa kuwa lipo mezani kwake.

Ikumbukwe kuahirishwa kwa kesi hiyo inayotajwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi KIsutu, kulifikiwa baada ya Mahakama hiyo kukubali maombi ya upande wa Jamhuri ulioeleza kuwa mpaka tarehe hiyo Julai 1, 2025, bado DPP alikuwa ajafanya uamuzi wa jalada la kesi ambalo lipo mezani kwake.

Awali, kabla ya kutolewa uamuzi huo na mahakama, Tundu Lissu wakati akijitetea aliiomba Mahakama kuagiza upande wa Jamhuri kulipeleka shauri lake Mahakama Kuu ya Tanzania haraka kama wamekamilisha ushahidi au Mwendesha Mashtaka aonyeshe nia ya kutoendelea na shauri lake, hivyo amuachie huru (nolle prosequi). Ikumbukwe Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu inafungwa mikono kisheria kusikiliza kesi hiyo.

===

Ulinzi umeimarishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam

Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika na Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Nyasa,
Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Sharifa Suleiman tayari wamefika hapa Kisutu kufuatilia kesi ya uhaini inayomhusu Mwenyekiti wa chama chao Tundu Lissu.

Tayari Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche afika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ili kufuatilia kesi ya uhaini inayomhusu Mwenyekiti wa chama chao Tundu Lissu.

WEKA LINK SASA
 
Kulikuwa na haja ya kuyasema haya mkuu wangu? mbona ni mjadala wa kawaida sana. Ingawa anayejadiliwa siyo mtu wa kawaida.
Mkuu kuna watu defensive mechanism Yao ni kutukana ili unyamaze maana ukiwa muungwana huwezi kujibizana nae kwa matusi kama hayo
 
Wakuu!

Mwenyekiti CHADEMA Taifa Tundu Lissu kufikishwa katika Mahakamani ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo kwa ajili kesi ya Uhaini inayomhusu.

Kumbuka kwamba kwenye kesi hii Tundu Lissu anajitetea mwenyewe.

Je, leo mwamba anaachiwa au atarudishwa tena 'kukamilisha na kumalizia kabisa kabisa kabisaaaa upelelezi?'

Wacha tuone kitakachojiri!

Kesi ya uhaini inayomkabili Lissu kutajwa tena leo Julai 15, uamuzi wa DPP kungojewa

Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Tundu Antiphas Lissu inaendelea leo Julai 15, 2025 ikiwa ni siku 14 tokea iliposikilizwa mara ya mwisho, ambapo unangojewa uamuzi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) kutokana na jalada ambalo ilielezwa kuwa lipo mezani kwake.

Ikumbukwe kuahirishwa kwa kesi hiyo inayotajwa kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi KIsutu, kulifikiwa baada ya Mahakama hiyo kukubali maombi ya upande wa Jamhuri ulioeleza kuwa mpaka tarehe hiyo Julai 1, 2025, bado DPP alikuwa ajafanya uamuzi wa jalada la kesi ambalo lipo mezani kwake.

Awali, kabla ya kutolewa uamuzi huo na mahakama, Tundu Lissu wakati akijitetea aliiomba Mahakama kuagiza upande wa Jamhuri kulipeleka shauri lake Mahakama Kuu ya Tanzania haraka kama wamekamilisha ushahidi au Mwendesha Mashtaka aonyeshe nia ya kutoendelea na shauri lake, hivyo amuachie huru (nolle prosequi). Ikumbukwe Mahakama Hakimu Mkazi Kisutu inafungwa mikono kisheria kusikiliza kesi hiyo.

===

Ulinzi umeimarishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam

Kaimu Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika Mwenyekiti wa chama hicho Kanda ya Nyasa, Joseph Mbilinyi (SUGU),Mwenyekiti wa Bawacha Taifa, Sharifa Suleiman tayari wamefika hapa Kisutu kufuatilia kesi ya uhaini inayomhusu Mwenyekiti wa chama chao Tundu Lissu.

Tayari Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Bara, John Heche awasili katika ukumbi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Lissu.

Acha ushabiki ndezi, hiyo kesi inahusiana vp na GE. Watu kwl mnaumwa.
 
In fact,
kwasabb ya uropokaji, ubishi na maneno mengi yasioyohusiana na kesi mahususi,

muungwana ataeleza madai mengine kabisa na kupoteza muda wa mahakama na kisha atarudishwa korokoroni kama kawaida hadi wakati mwingine 🐒
Wewe tangu upewe rushwa ya baiskeli feki na ccm unajiona umeyapatia maisha sana.
 
Attachments

  • FB_IMG_1752520128500.jpg
    FB_IMG_1752520128500.jpg
    526.6 KB · Views: 26
Back
Top Bottom