Roving Journalist
JF Roving Journalist
- Apr 18, 2017
- 5,352
- 15,876
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franco Kiswaga, anatarajiwa kutoa uamuzi wa hoja zilizowasilishwa na pande mbili katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Tundu Lissu.
Kabla ya uamuzi huo, upande wa Jamhuri utatakiwa kutoa maelezo kuhusu hatua walizofikia kulingana na rai iliyotolewa na mahakama kuwata kufanya hivyo.
Uamuzi huo unasomwa baada ya upande wa Lissu kupinga ombi la Jamhuri la kuahirisha mara kwa mara shauri hilo bila kuchukua uamuzi wa kulipeleka Mahakama Kuu, endapo wana nia ya kuendelea nalo.
Lissu alipinga ombi hilo akidai kuwa kuna uzembe wa upande wa mawakili wa Jamhuri, ambao unasababisha shauri hilo kutofikishwa Mahakama Kuu, huku akiomba mahakama ikatae ombi la kuahirisha.
Hata hivyo, upande wa Jamhuri ulidai kuwa ulikuwa ukisubiri uamuzi wa ombi lao waliloliwasilisha Mahakama Kuu, wakiiomba iridhie ushahidi wa siri. Walieleza kuwa mahakama imezuiliwa kutoa uamuzi kwa kuwa ombi hilo lipo katika mahakama ya juu yake.
Wakili wa Serikali Mkuu, Nassor Katuga, aliongeza kuwa maelezo ya mashahidi yanapaswa kuambatana na taarifa za mashtaka, jambo lililochelewesha mchakato huo kutokana na mashahidi hao kuwa sehemu ya ombi la ulinzi.
Hakimu Kiswaga, baada ya kusikiliza pande zote, alisema atatoa uamuzi leo, Agosti 13, 2025, na kwamba kutokana na aina ya hoja zilizowasilishwa, alihitaji muda zaidi kufanya utafiti wa kisheria ili kuandaa uamuzi.
Hata hivyo, hakimu alielekeza upande wa Jamhuri kuhakikisha wanachukua hatua madhubuti ili Mahakama Kuu itoe uamuzi kuhusu maombi ya kulinda mashahidi. Alibainisha kuwa kabla ya kuanza kusoma uamuzi, atataka kwanza apewe maelezo kuhusu hatua walizofikia.
Ikumbukwe kuwa Mahakama Kuu – Masijala ya Dar es Salaam, Agosti 4, 2025, ilikubali ombi la upande wa Jamhuri la kuficha majina na taarifa nyingine za mashahidi wa upande wa mashtaka katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga
"Upande wa Jamhuri umeshapeleka taarifa Mahakama Kuu, kwa maana ya kufaili taarifa, kwa mujibu wa kifungu cha 262(6), na taarifa hiyo imepokelewa na kusajiliwa kwa namba Criminal Session 19605/2025 ambayo ni shauri la Jamhuri dhidi ya Tundu Antipas Lissu."
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Antiphas Tundu Lissu.
"Mheshimiwa naomba maelekezo ya Mahakama yako, taarifa iliyopelekwa Mahakama Kuu kama imeshaletwa kwenye Mahakama hii, maana yake ikishapelekwa Mahakama Kuu inatakiwa iletwe kwenye mahakama hii ni Msajili wa Mahakama Kuu....Mahakama yako mheshimiwa itupe maelekezo kama 'file' limekuja kutoka mahakama kuu tuendelee mimi niko tayari."
"Sasa ile hofu yangu ya Star Chamber Court, inatima sasa, tunaingizwa katika utaratibu ambao kesi zitafanyika gizani kesi ya uhaini ambayo adhabu yake ni kifo kwa maombi yao inatakiwa ifanyike gizani."
Wakili wa Serikali Mkuu, Nassoro Katuga, ametaka kesi ya Tundu Lissu isiendelee kuonyeshwa moja kwa moja kupitia Vyombo vya Habari.
"Mahakama Kuu, kwa busara zake na kutaka kuona kwamba hawa mashahidi raia hawapati vitisho vyovyote kabla na baada ya kutoa ushahidi, ikasema wakati wa usikilizaji wa kesi mahakamani hatakuwa na chapisho la nyaraka yoyote au ushahidi mwingine wowote utakaopelekea utambuzi wa mashahidi ambao ni raia, vinginevyo kuwe na ruhusa ya Mahakama Kuu."
"Mhe. Msingi wa kuyasema haya ni kwamba shauri hili linaendeshwa na kurushwa moja kwa moja dunia nzima, kwa maana tayari tukiyasoma kwa njia hii ya kurusha moja kwa moja itakuwa tumekinzana na maamuzi ya Mahakama Kuu ya kwamba tusi-publish nyaraka au ushahidi mwingine wowote ambao unapelekea utambuzi wa shahidi huyu."
"Ombi letu sisi pamoja na nia njema ya Mahakama ya kuonyesha moja kwa moja mwendo wa Shauri hili tunaiomba Mahakama yako tukufu iweze kufuata maagizo kwenye rulling hii na Mahakama Kuu kwa kuzuia publication ya ushahidi wa namna hii"
===
Kesi ya Uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu iliyokuwa ikiendelea leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam, imeahirishwa hadi Agosti 18, 2025.
Hakimu Mkazi Franco Kiswaga amesema, kesi hiyo itaendelea hatua inayofuata (committal) na si tena kuandaa maamuzi.