GE2025 Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu yaahirishwa hadi Agosti 13,2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu baada ya kuahirishwa Julai 15, 2025 inatarajiwa kuendelea tena leo, ambapo bado inasubiriwa hatua ya Ofisi ya Mwendesha mashtaka (DPP) kufanya uamuzi wa kufikisha kesi hiyo Mahakama Kuu ambayo ina hadhi ya kisheria.

Mara ya mwisho Kesi ilipotajwa upande wa Jamhuri ulisema kuwa una nia ya kupeleka kesi hiyo Mahakama Kuu, lakini walieleza kuwa tayari kuna ombi la kuficha mashahidi walikuwa wamelifikisha Mahakamani hivyo waliomba ahirisho ili kwanza liweze kujibiwa.

Hata hivyo Tundu Lissu alipinga hoja ya ahirisho akiomba Mahakama kutumia mamlaka yake kufuta shauri hilo kutokana na Jamhuri kuomba ahirisho mara kwa mara.

Hata hivyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franko Kiswaga baada ya kusikiliza hoja za upande wa Jamhuri na upande wa Lissu, alifikia uamuzi wa kutoa ahirisho kama ilivyoombwa na Jamhuri.

Hata hivyo alitoa maelekezo kwa Jamhuri kwa kuwataka washughulikie maombi hayo haraka iwezekanavyo ili yasiwe kikwazo cha ucheleweshwaji wa shauri hilo.

Ikumbukwe Tundu Lissu alikamatwa April 9, 2025 akiwa kwenye mkutano wa Chadema huko Mbinga, na kufikishwa Mahakamani Dar es Salaam siku iliyofuata, 10 Aprili 2025. Hivyo, tangu alipofikishwa mahakamani, hadi leo Julai 30, 2025, zimepita siku takribani 112.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Lissu, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo mahakama hiyo inatarajia kuendelea kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili.
Your browser is not able to display this video.

​
Askari Magereza walioficha nyuso zao wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Your browser is not able to display this video.
Ukumbi wa Mahakama umekwisha jaa asubuhi hii, wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA wakiwa tayari kufuatia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Lissu.

Your browser is not able to display this video.
Wananchi, Wanachama na viongozi wa Chadema wakiwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabali Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu.

Your browser is not able to display this video.


Your browser is not able to display this video.
Makamu Mwenyekiti wa Chama John Heche akiwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu.

Your browser is not able to display this video.
Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, kwa niaba ya upande wa Jamhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameomba mahakama kuahirisha kwa mara nyingine usikilizwaji wa kesi hiyo.

Your browser is not able to display this video.
Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, amepinga ombi la upande wa Jamhuri la kutaka kuahirisha tena kesi ya uhaini inayomkabili. Kesi hiyo inaendelea huku ikiwa ni siku ya 112 tangu akamatwe na kuwekwa gerezani.

Your browser is not able to display this video.
"Mhe. Hakimu naomba nianze kwa kusema kwamba maombi haya yasiyoisha ya ahirisho, namba moja ni ushahidi mwingine kama kuna ushahidi zaidi unaohitajika wa matumizi mabaya ya Judiciary Process, Abuse of Court Process, huu ni ushahidi mwingine tena, hilo ni la kwanza na la pili ni kwamba haya yanatokea kwa sababu mahakama yako imeruhusu kuendeshwa na mawakili wa serikali"

"Mhe. Hakimu Mahakama yako imeshindwa kuona na kuhakikisha kuwa amri zake zinatekelezwa. Jaji Mkuu Mstaafu Samatta CJ alisema Majaji dhaifu ni chanzo cha ukiukwaji wa Haki za watu"

"Mhe. Hakimu, kama kweli unataka kuonesha Mahakama kuwa haiendeshwi na mawakili wa serikali, basi wakatalie ahirisho lao once and for all"

"Ni ajabu Mheshimiwa Hakimu hapa ni Mshtakiwa anaedai apelekwe mahakama kuu akashtakiwe, Kama Mahakama itaona ana hatia anyongwe. Twendeni tukapambane, si mnataka? Si mmefungua kesi ya uhaini? Pelekeni taarifa mahakama kuu."

"Mimi siombi huruma ya Mahakama, Mimi nataka HAKI, Pelekeni taarifa Mahakama Kuu kama Sheria inavyotaka, tukapambane huko".

"Huyu mtu mmoja ambaye yuko kwenye gereza lenye ulinzi wa juu, amewekwa na watu waliohukumiwa kufa, ana ulinzi mkali, nawezaje kutishia mahakama yako?"

Your browser is not able to display this video.
Wakili wa Serikali Mahakamani

"Mhe. kwenye kuiheshimu Mahakama tuna lugha za staha hata kama umewiwa namna gani, haya mengine unaweza zungumzia nje lakini kwenye proceedings kuna lugha za staha ambazo zinaifanya Mahakama au tuonyeshe heshima kwa Mahakama."

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Franco Kiswaga alivyoahirisha Kesi ya Uhaini ya Lissu mpaka tarehe 13 Agosti 2025.

Your browser is not able to display this video.
 
Samia na genge lake wanamuogopa sana Lissu hadi wametumia Polisi na Mahakama kumuweka kizuizini kwani wanajua kwenye uchaguzi ulio huru na wa haki Lissu anamshinda Samia saa nne asubuhi tu tena kwa margin kubwa sana.
 
Tuko busy na uchaguzi wa wabunge ccm,lema yupo canada,heche kesi imeshamchosha,tonetone imekata,wanachadema wapo busy na CCM,kwani kesi ya lisu ni Leo?
 
Free Tundu Lissu.
No reform No election
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…