Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu baada ya kuahirishwa Julai 15, 2025 inatarajiwa kuendelea tena leo, ambapo bado inasubiriwa hatua ya Ofisi ya Mwendesha mashtaka (DPP) kufanya uamuzi wa kufikisha kesi hiyo Mahakama Kuu ambayo ina hadhi ya kisheria.
Mara ya mwisho Kesi ilipotajwa upande wa Jamhuri ulisema kuwa una nia ya kupeleka kesi hiyo Mahakama Kuu, lakini walieleza kuwa tayari kuna ombi la kuficha mashahidi walikuwa wamelifikisha Mahakamani hivyo waliomba ahirisho ili kwanza liweze kujibiwa.
Hata hivyo Tundu Lissu alipinga hoja ya ahirisho akiomba Mahakama kutumia mamlaka yake kufuta shauri hilo kutokana na Jamhuri kuomba ahirisho mara kwa mara.
Hata hivyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franko Kiswaga baada ya kusikiliza hoja za upande wa Jamhuri na upande wa Lissu, alifikia uamuzi wa kutoa ahirisho kama ilivyoombwa na Jamhuri.
Hata hivyo alitoa maelekezo kwa Jamhuri kwa kuwataka washughulikie maombi hayo haraka iwezekanavyo ili yasiwe kikwazo cha ucheleweshwaji wa shauri hilo.
Ikumbukwe Tundu Lissu alikamatwa April 9, 2025 akiwa kwenye mkutano wa Chadema huko Mbinga, na kufikishwa Mahakamani Dar es Salaam siku iliyofuata, 10 Aprili 2025. Hivyo, tangu alipofikishwa mahakamani, hadi leo Julai 30, 2025, zimepita siku takribani 112.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Lissu, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo mahakama hiyo inatarajia kuendelea kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili.
Askari Magereza walioficha nyuso zao wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Ukumbi wa Mahakama umekwisha jaa asubuhi hii, wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA wakiwa tayari kufuatia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Lissu.
Wananchi, Wanachama na viongozi wa Chadema wakiwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabali Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu.
dalili nzuri tutashinda