GE2025 Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu yaahirishwa hadi Agosti 13,2025

GE2025 Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu yaahirishwa hadi Agosti 13,2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Unending case adjournments what is the remedy in Tanzania law

In Tanzanian law, the remedy for unending case adjournments, particularly in criminal cases, is for the court to dismiss the charge and discharge the accused. This action is taken when delays are deemed excessive and prejudicial to the accused, especially when caused by the prosecution's lack of diligence or deliberate attempts to delay the proceedings
 
Unending case adjournments what is the remedy in Tanzania law

In Tanzanian law, the remedy for unending case adjournments, particularly in criminal cases, is for the court to dismiss the charge and discharge the accused. This action is taken when delays are deemed excessive and prejudicial to the accused, especially when caused by the prosecution's lack of diligence or deliberate attempts to delay the proceedings
Kesi hii ilitakiwa iishe ndani ya Mwezi mmoja tu. Maana hakuna cha kusililiza
 
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu baada ya kuahirishwa Julai 15, 2025 inatarajiwa kuendelea tena leo, ambapo bado inasubiriwa hatua ya Ofisi ya Mwendesha mashtaka (DPP) kufanya uamuzi wa kufikisha kesi hiyo Mahakama Kuu ambayo ina hadhi ya kisheria.

Mara ya mwisho Kesi ilipotajwa upande wa Jamhuri ulisema kuwa una nia ya kupeleka kesi hiyo Mahakama Kuu, lakini walieleza kuwa tayari kuna ombi la kuficha mashahidi walikuwa wamelifikisha Mahakamani hivyo waliomba ahirisho ili kwanza liweze kujibiwa.

Hata hivyo Tundu Lissu alipinga hoja ya ahirisho akiomba Mahakama kutumia mamlaka yake kufuta shauri hilo kutokana na Jamhuri kuomba ahirisho mara kwa mara.

Hata hivyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franko Kiswaga baada ya kusikiliza hoja za upande wa Jamhuri na upande wa Lissu, alifikia uamuzi wa kutoa ahirisho kama ilivyoombwa na Jamhuri.

Hata hivyo alitoa maelekezo kwa Jamhuri kwa kuwataka washughulikie maombi hayo haraka iwezekanavyo ili yasiwe kikwazo cha ucheleweshwaji wa shauri hilo.

Ikumbukwe Tundu Lissu alikamatwa April 9, 2025 akiwa kwenye mkutano wa Chadema huko Mbinga, na kufikishwa Mahakamani Dar es Salaam siku iliyofuata, 10 Aprili 2025. Hivyo, tangu alipofikishwa mahakamani, hadi leo Julai 30, 2025, zimepita siku takribani 112.


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Lissu, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo mahakama hiyo inatarajia kuendelea kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili.
Askari Magereza walioficha nyuso zao wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Ukumbi wa Mahakama umekwisha jaa asubuhi hii, wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA wakiwa tayari kufuatia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Lissu.

Wananchi, Wanachama na viongozi wa Chadema wakiwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabali Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu.

Makamu Mwenyekiti wa Chama John Heche akiwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, kwa niaba ya upande wa Jamhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameomba mahakama kuahirisha kwa mara nyingine usikilizwaji wa kesi hiyo.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, amepinga ombi la upande wa Jamhuri la kutaka kuahirisha tena kesi ya uhaini inayomkabili. Kesi hiyo inaendelea huku ikiwa ni siku ya 112 tangu akamatwe na kuwekwa gerezani.

"Mhe. Hakimu naomba nianze kwa kusema kwamba maombi haya yasiyoisha ya ahirisho, namba moja ni ushahidi mwingine kama kuna ushahidi zaidi unaohitajika wa matumizi mabaya ya Judiciary Process, Abuse of Court Process, huu ni ushahidi mwingine tena, hilo ni la kwanza na la pili ni kwamba haya yanatokea kwa sababu mahakama yako imeruhusu kuendeshwa na mawakili wa serikali"

"Mhe. Hakimu Mahakama yako imeshindwa kuona na kuhakikisha kuwa amri zake zinatekelezwa. Jaji Mkuu Mstaafu Samatta CJ alisema Majaji dhaifu ni chanzo cha ukiukwaji wa Haki za watu"

"Mhe. Hakimu, kama kweli unataka kuonesha Mahakama kuwa haiendeshwi na mawakili wa serikali, basi wakatalie ahirisho lao once and for all"

"Ni ajabu Mhe kwamba Mshitakiwa ndiye anayedai apelekwa mahakama kuu ashitakiwe kama mahakama itaona ana hatia anyongwe, mshitakiwa ndiye anayesema twendeni huko."


Tundu Lissu anajua sana kulinda haki zake na kuweka grounds mahakamani zitakazo linda watu wengine kwa miaka 50 ijayo.

Thank You Hon TAL for your courage
 
Kuna jambo kubwa sana la kujifunza kupitia kesi hii ya kihistoria.

Mchakato wa Haki Jinai wa Tanzania (Criminal Justice System) kutumiwa vibaya huku waTanzania tukikubali iwe hivyo.

1753863721036.png

Mbinga Ruvuma Tanzania
1753863975050.jpeg
 
Back
Top Bottom