GE2025 Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu yaahirishwa hadi Agosti 13,2025

GE2025 Kesi ya Uhaini ya Tundu Lissu yaahirishwa hadi Agosti 13,2025

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Tundu Lissu anajua sana kulinda haki zake na kuweka grounds mahakamani zitakazo linda watu wengine kwa miaka 50 ijayo.

Thank You Hon TAL for your courage
Naamini Mungu ameacha haya yampate Lissu kwa ajili ya kuweka somo kwa miaka ijayo kama ulivyoandika.

Naamini Tanzania ya kesho itakuwa salama kutokana na haya mapito ya leo.

Mungu Baba wa Mbinguni azidi kumbariki sana Tundu A.M. Lissu kwa shule anayoitoa.
 
Wakikuambia tuko nyuma yako, geuka nyuma uangalie kama kweli wapo
 
Naamini Mungu ameacha haya yampate Lissu kwa ajili ya kuweka somo kwa miaka ijayo kama ulivyoandika.

Naamini Tanzania ya kesho itakuwa salama kutokana na haya mapito ya leo.

Mungu Baba wa Mbinguni azidi kumbariki sana Tundu A.M. Lissu kwa shule anayoitoa.
Yeah haya maumivu lazima Mungu atulipie
 
Aliyewaambia Tunduma mkiniletea wapinzani maji msahau maana sitoleta sitaki kuchanganyiwa betri na magunzi alikuwa nani?

Mnafikiri tumesahau aliyesema wapinzani wanachelewesha maendeleo , katengeneza bunge kibogoyo ni kijani tupu leo deni ni trilioni 107 bi Mwenda akisemwa tu naye anakutimua.


View: https://youtu.be/xjJ1nLDvm9k?si=1Ur0Aq9WWySiKA52

Kwa miaka 20 iliopita ni kiongozo gani wa nchi alifanya kazi nzuri na inayoelezeka nje na ndani ya nchi hii?
 
Kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Tundu Lissu baada ya kuahirishwa Julai 15, 2025 inatarajiwa kuendelea tena leo, ambapo bado inasubiriwa hatua ya Ofisi ya Mwendesha mashtaka (DPP) kufanya uamuzi wa kufikisha kesi hiyo Mahakama Kuu ambayo ina hadhi ya kisheria.

Mara ya mwisho Kesi ilipotajwa upande wa Jamhuri ulisema kuwa una nia ya kupeleka kesi hiyo Mahakama Kuu, lakini walieleza kuwa tayari kuna ombi la kuficha mashahidi walikuwa wamelifikisha Mahakamani hivyo waliomba ahirisho ili kwanza liweze kujibiwa.

Hata hivyo Tundu Lissu alipinga hoja ya ahirisho akiomba Mahakama kutumia mamlaka yake kufuta shauri hilo kutokana na Jamhuri kuomba ahirisho mara kwa mara.

Hata hivyo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Franko Kiswaga baada ya kusikiliza hoja za upande wa Jamhuri na upande wa Lissu, alifikia uamuzi wa kutoa ahirisho kama ilivyoombwa na Jamhuri.

Hata hivyo alitoa maelekezo kwa Jamhuri kwa kuwataka washughulikie maombi hayo haraka iwezekanavyo ili yasiwe kikwazo cha ucheleweshwaji wa shauri hilo.

Ikumbukwe Tundu Lissu alikamatwa April 9, 2025 akiwa kwenye mkutano wa Chadema huko Mbinga, na kufikishwa Mahakamani Dar es Salaam siku iliyofuata, 10 Aprili 2025. Hivyo, tangu alipofikishwa mahakamani, hadi leo Julai 30, 2025, zimepita siku takribani 112.


Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) taifa, Tundu Lissu, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo mahakama hiyo inatarajia kuendelea kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili.
Askari Magereza walioficha nyuso zao wakiwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.

Ukumbi wa Mahakama umekwisha jaa asubuhi hii, wananchi, wanachama na viongozi wa CHADEMA wakiwa tayari kufuatia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama Taifa, Tundu Lissu.

Wananchi, Wanachama na viongozi wa Chadema wakiwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya uhaini inayomkabali Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Tundu Lissu.

Makamu Mwenyekiti wa Chama John Heche akiwasili Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia mwenendo wa kesi ya Uhaini inayomkabili Tundu Lissu.

Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga, kwa niaba ya upande wa Jamhuri katika kesi ya uhaini inayomkabili Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, ameomba mahakama kuahirisha kwa mara nyingine usikilizwaji wa kesi hiyo.

Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu, akizungumza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, amepinga ombi la upande wa Jamhuri la kutaka kuahirisha tena kesi ya uhaini inayomkabili. Kesi hiyo inaendelea huku ikiwa ni siku ya 112 tangu akamatwe na kuwekwa gerezani.

"Mhe. Hakimu naomba nianze kwa kusema kwamba maombi haya yasiyoisha ya ahirisho, namba moja ni ushahidi mwingine kama kuna ushahidi zaidi unaohitajika wa matumizi mabaya ya Judiciary Process, Abuse of Court Process, huu ni ushahidi mwingine tena, hilo ni la kwanza na la pili ni kwamba haya yanatokea kwa sababu mahakama yako imeruhusu kuendeshwa na mawakili wa serikali"

"Mhe. Hakimu Mahakama yako imeshindwa kuona na kuhakikisha kuwa amri zake zinatekelezwa. Jaji Mkuu Mstaafu Samatta CJ alisema Majaji dhaifu ni chanzo cha ukiukwaji wa Haki za watu"

"Mhe. Hakimu, kama kweli unataka kuonesha Mahakama kuwa haiendeshwi na mawakili wa serikali, basi wakatalie ahirisho lao once and for all"

"Ni ajabu Mheshimiwa Hakimu hapa ni Mshtakiwa anaedai apelekwe mahakama kuu akashtakiwe, Kama Mahakama itaona ana hatia anyongwe. Twendeni tukapambane, si mnataka? Si mmefungua kesi ya uhaini? Pelekeni taarifa mahakama kuu."

"Mimi siombi huruma ya Mahakama, Mimi nataka HAKI, Pelekeni taarifa Mahakama Kuu kama Sheria inavyotaka, tukapambane huko".

"Huyu mtu mmoja ambaye yuko kwenye gereza lenye ulinzi wa juu, amewekwa na watu waliohukumiwa kufa, ana ulinzi mkali, nawezaje kutishia mahakama yako?"

Wakili wa Serikali Mahakamani

"Mhe. kwenye kuiheshimu Mahakama tuna lugha za staha hata kama umewiwa namna gani, haya mengine unaweza zungumzia nje lakini kwenye proceedings kuna lugha za staha ambazo zinaifanya Mahakama au tuonyeshe heshima kwa Mahakama."

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Franco Kiswaga alivyoahirisha Kesi ya Uhaini ya Lissu mpaka tarehe 13 Agosti 2025.


Serikali si jambo la kuchezea sanaaa.
 
Samia na genge lake wanamuogopa sana Lissu hadi wametumia Polisi na Mahakama kumuweka kizuizini kwani wanajua kwenye uchaguzi ulio huru na wa haki Lissu anamshinda Samia saa nne asubuhi tu tena kwa margin kubwa sana.
Hakuna hilo

Tundu lissu kafanya haya kwa makusudi ili watu wanje wampe support na fedha.
Na hayo yote anofanya mahakamani ni kwa sababu hizo . Jumuiya za nje zimpe support yeye na chama chake.

Serikali imeingia kwenye mtego wake.
 
Hakuna hilo

Tundu lissu kafanya haya kwa makusudi ili watu wanje wampe support na fedha.
Na hayo yote anofanya mahakamani ni kwa sababu hizo . Jumuiya za nje zimpe support yeye na chama chake.

Serikali imeingia kwenye mtego wake.
Wote wenye akili timamu wanajua hii kesi ya mchongo ni agizo la Samia ili apate ahueni kuelekea uchaguzi mkuu, kama kuna kesi kwa nini wasipeleke High Court ili ianze kusikilizwa? tumia hata hiyo akili kiduchu uliyobakishiwa.
 
Kwa miaka 60 sasa serikali ni ya chama gani kuanzia rais hadi mawaziri?
Hoja hujibiwa kwa hoja sasa wewe unaleta uswahili ila sababu mie n mtu mzima nimelijua jibu lako hvyo ndio uelewe yule jamaa alikuwa anaijenga Tanzania na alikuwa tayari kuifuta CCM na kutengeneza chama kingine chenye muundo mzuri wa kuwaleta pamoja watanzania
 
Hoja hujibiwa kwa hoja sasa wewe unaleta uswahili ila sababu mie n mtu mzima nimelijua jibu lako hvyo ndio
Wapi umejibu?

Umekanusha wapi kauli yako ya kusema aliunganisha watu bila ubaguzi wakati video akiwa Tunduma inajieleza akiwapa watu vitisho?
uelewe yule jamaa alikuwa anaijenga Tanzania na alikuwa tayari kuifuta CCM na kutengeneza chama kingine chenye
Wapi aliwahi kusema angeifuta CCM weka ushahidi.
muundo mzuri wa kuwaleta pamoja watanzania
Mfumo upi huo?

Wa kusema mkimchagua mpinzani siwaletei maji hapa?
 
Wapi umejibu?

Umekanusha wapi kauli yako ya kusema aliunganisha watu bila ubaguzi wakati video akiwa Tunduma inajieleza akiwapa watu vitisho?

Wapi aliwahi kusema angeifuta CCM weka ushahidi.

Mfumo upi huo?

Wa kusema mkimchagua mpinzani siwaletei maji hapa?
Hyo video ni effects za Kuona Kila anachofanya CHADEMA wanasema anacopy hoja zetu kama sio hoja Yao basi wanapinga sio sawa ndio akaona huo ni ujinga ndio sababu ya kuona upinzani hauna maana

Kuoneshana kuwa alikuwa tayari kufanya kazi na upinzani na kufuta CCM na kuleta chama kipya ni pale alipoamua kuleta mtu kutoka chama chochote na Kuona anamawazo chanta anampa wizara, au udc hata nafasi nyeti ndani ya CCM.

Kwa lugha nyingine mie Nina kadi ya CHADEMA kuhusu Magufuli aisee usimseme vibaya yule Mzee kafanya mengi na makubwa kwenye taifa hili
 
Samia na genge lake wanamuogopa sana Lissu hadi wametumia Polisi na Mahakama kumuweka kizuizini kwani wanajua kwenye uchaguzi ulio huru na wa haki Lissu anamshinda Samia saa nne asubuhi tu tena kwa margin kubwa sana.
REFORMS are inevitable.✍️📌
 
Back
Top Bottom