Notorious thug
JF-Expert Member
- Dec 29, 2021
- 2,817
- 10,667
Nakumbuka kipindi nilipokuwa mahabusu na hatimaye mfugwa nilikutana na mahabusu wengi waliokuwa wanasubiri hatima ya kesi zao. Wengi wamekuwa kama vichaa au kuchoka kimwili kwa muda mrefu wanaosubiri hukumu yao.
Nilikutana na mzee aliyekaa mahabusu toka 2008 anasubiri hukumu ya kumuua mkewe hakika huyu mzee anasikitisha sana haswa usiku huwa anapiga kelele nyingi kama kuota au hali ya kuweweseka.
Kwa hali ilivyo kesi za mauaji iwe uliua au umesingiziwa kwa uzoefu nilioupata pale wengi wanaoshtakiwa kesi hizi zimekuwa ngumu sana kwao na kuwaathiri kimwili na kisaikolojia. Wengi wamepigwa sana na askari kipindi cha upelelezi miguu kuvunjwa mikono kuvunjwa wengi wanachechemea na majeraha makubwa mwilini na kutengwa na ndugu zao hakika wanakua kwenye kipindi kigumu sana.
Ombi langu kubwa ni kwa askari kukamilisha upelelezi mapema na wapate haki zao mapema, wengi wanafia ndani bila kuhukumiwa
Mahakama ziangalie pale na division ya kuhukumu kesi za mauaji tu zimekuwa nyingi na wengi wanaishia rumande miaka 10-15 bila kupata hukumu.