Kesi za mauaji zinavyowasumbua mahabusu na wafungwa wengi

Kesi za mauaji zinavyowasumbua mahabusu na wafungwa wengi

Tatizo kubwa polisi wetu hawana uwezo wa kupeleleza kitaalamu….wanatumia mbinu ya kupiga watu na kutesa ili wakubali na kutokana na watu kuchoka na mateso wanakubali…..Mimi naamini na kuna wafungwa na na mahabusu ambao wamebambikiwa tu kesi...

Kitengo cha upelelezi kiboreshwe na watu wapewe mafunzo hata nje ya nchi…
Kiundwe taasis/kitengo maalumu cha upelelezi kushughulika kesi kubwa kubwa maana polisi wamelemewa.
 
Tuhuma za makosa yote zinapaswa kuwa na dhamana, ni sheria za hovyo kupoka haki ya dhamana kwa kosa lolote.
 
Hahaha



Wasaidizi wake wamelala binafsi namshukuru hayati Magufuli alienda butimba kujionea hali na waliosingiziwa walitolewa kwa chifu hangaya sijui kama atakumbuka kwenda gereza lolote
Kinachotakiwa ni katiba mpya itakayoweka haki ya dhamana kwa makosa yote sio huu mtindo wa kusubiri hisani na fadhila za mtu mmoja.
 
Kesi za mauaji murder case ni serious sana hata kwenye nchi maskini z nazoendelea zenye weak judiciary system.
Hili sio tatizo la mahakama tu ni suala la polisi wanaokamata watu bila upelelezi na ushahidi wa kujitosheleza unaoweza kupelekwa na kusikilizwa mahakamani.
 
Tatizo kubwa polisi wetu hawana uwezo wa kupeleleza kitaalamu….wanatumia mbinu ya kupiga watu na kutesa ili wakubali na kutokana na watu kuchoka na mateso wanakubali…..Mimi naamini na kuna wafungwa na na mahabusu ambao wamebambikiwa tu kesi...

Kitengo cha upelelezi kiboreshwe na watu wapewe mafunzo hata nje ya nchi…
Kitengo cha upelelezi kitolewe police kisiwe idera ya police kiwe chini ya mwendesha mashtaka WA serikali itasaidia snaa wakiajiri Kwa mkupuo watu 30000 waanze kukisuka polepole kuliko kuachia polisi
 
Polisi hawana akili. Hata ukikiri kosa mwenyewe bado watasema uchunguzi bado.
Nakumbuka Kuna dogo alikwapua milioni hamsini kazini. Wahasibu walipopelekwa polisi dogo alijitolea akasema ni yeye ndio aliyeiba lkn polisi bado hawakumuamini kwamba ni yeye.
Wanangangania wanafanya uchunguzi.
Mapolisi wakubwa ni kina Kingai na Swila hao wadogo wanaopewa maelekezo na kina Swila unategemea vichwani mwao Kuna ubongo wa namna gani?
 
Jaji Mkuu anataarifa hii? Kwamba kesi zinacheleweshwa? Kuna sababu gani ya kumshikilia mtu kwa kesi ya mauaji kwa miaka 15 kama upelelezi umeshindikana bunge litunge sheria ya jaji kuwaachia Mahabusu waliokaa miaka 5 Mahabusu wakisubiri upelelezi ukamilike.
Jaji mkuu Yuko kwenye huo mfumo kitambo ndio maana sasa ni bosi. Anajua kila kitu, ndio hivyo tena hana nia ya kutafuta suluhisho.
 
Back
Top Bottom