Kesi za mauaji zinavyowasumbua mahabusu na wafungwa wengi

Kesi za mauaji zinavyowasumbua mahabusu na wafungwa wengi

bongo nyoso, bongo balaa

Damu ya mtu haikuachi hivihivi na huko gerezani ndio shiiida
 
Jaji Mkuu anataarifa hii? Kwamba kesi zinacheleweshwa? Kuna sababu gani ya kumshikilia mtu kwa kesi ya mauaji kwa miaka 15 kama upelelezi umeshindikana bunge litunge sheria ya jaji kuwaachia Mahabusu waliokaa miaka 5 Mahabusu wakisubiri upelelezi ukamilike.
Jaji mkuu kageuka msemaji wa ccm
 
Nakumbuka kipindi nilipokuwa mahabusu na hatimaye mfugwa nilikutana na mahabusu wengi waliokuwa wanasubiri hatima ya kesi zao. Wengi wamekuwa kama vichaa au kuchoka kimwili kwa muda mrefu wanaosubiri hukumu yao.

Nilikutana na mzee aliyekaa mahabusu toka 2008 anasubiri hukumu ya kumuua mkewe hakika huyu mzee anasikitisha sana haswa usiku huwa anapiga kelele nyingi kama kuota au hali ya kuweweseka.

Kwa hali ilivyo kesi za mauaji iwe uliua au umesingiziwa kwa uzoefu nilioupata pale wengi wanaoshtakiwa kesi hizi zimekuwa ngumu sana kwao na kuwaathiri kimwili na kisaikolojia. Wengi wamepigwa sana na askari kipindi cha upelelezi miguu kuvunjwa mikono kuvunjwa wengi wanachechemea na majeraha makubwa mwilini na kutengwa na ndugu zao hakika wanakua kwenye kipindi kigumu sana .

Ombi langu kubwa ni kwa askari kukamilisha upelelezi mapema na wapate haki zao mapema, wengi wanafia ndani bila kuhukumiwa

Mahakama ziangalie pale na division ya kuhukumu kesi za mauaji tu zimekuwa nyingi na wengi wanaishia rumande miaka 10-15 bila kupata hukumu.

Tatizo kubwa polisi wetu hawana uwezo wa kupeleleza kitaalamu….wanatumia mbinu ya kupiga watu na kutesa ili wakubali na kutokana na watu kuchoka na mateso wanakubali…..Mimi naamini na kuna wafungwa na na mahabusu ambao wamebambikiwa tu kesi...

Kitengo cha upelelezi kiboreshwe na watu wapewe mafunzo hata nje ya nchi…
 
Kama kesi ya kusingiziwa M/Mungu awaongoze wapate haki zao haraka kama mtu aliua kweli kwa maksudi afege tu naye huko huko mahabusu
 
Inasikitisha sana...

Jela siyo kuzuri kabisa, unaingia wewe, unatoka mtu mwingine kabisa mwenye roho tofauti kabisa...
 
Tatizo kubwa polisi wetu hawana uwezo wa kupeleleza kitaalamu….wanatumia mbinu ya kupiga watu na kutesa ili wakubali na kutokana na watu kuchoka na mateso wanakubali…..Mimi naamini na kuna wafungwa na na mahabusu ambao wamebambikiwa tu kesi...

Kitengo cha upelelezi kiboreshwe na watu wapewe mafunzo hata nje ya nchi…
Tatizo usilolijua ni kwamba 98% ya watuhumiwa wanaohojiwa kwa nguvu na kukiri, ni wahusika wa matukio.

Hauwezi kukiri bila ya kuonesha vielelezo ukahesabika umekiri na ukaaminika.

Mtu anayehesabika amekiri na kutoa ushirikiano ni yule anayekiri na kuonesha vidhibiti.
 
Unatetea ujinga
 
Hii ishu inauniza sana,hasa sie maskini,na mdogo wangu huu mwaka wa nne yupo mahabusu kwa kesi ya kusingizwa,kisa alikutwa amekaa kwenye gari na mshikaji wake kumbe mshikaji ni jambazi alikua anatafutwa,hivo wakakamatwa wote na akihusishwa natukio.
Kufika polisi akawa anaoneshwa video za cctv camera za msela mwingine afu polisi wakawa wanamforce akubali kuwa ni yeye , dah dogo akagoma.askari mmoja akamwambia yule wa kwny camera kweli sio yeye ila anatakiwa ajiongeze la sivyo watamuhusisha na tukio jingine ambalo lilikua mpaka na mauaji.sorry nashindwa kuendelea zaidi,naumia sana mdogoangu mpaka sahv anateseka bure kisa tu tulishindwa kutoa million 3.
 
Nakumbuka kipindi nilipokuwa mahabusu na hatimaye mfugwa nilikutana na mahabusu wengi waliokuwa wanasubiri hatima ya kesi zao. Wengi wamekuwa kama vichaa au kuchoka kimwili kwa muda mrefu wanaosubiri hukumu yao.

Nilikutana na mzee aliyekaa mahabusu toka 2008 anasubiri hukumu ya kumuua mkewe hakika huyu mzee anasikitisha sana haswa usiku huwa anapiga kelele nyingi kama kuota au hali ya kuweweseka.

Kwa hali ilivyo kesi za mauaji iwe uliua au umesingiziwa kwa uzoefu nilioupata pale wengi wanaoshtakiwa kesi hizi zimekuwa ngumu sana kwao na kuwaathiri kimwili na kisaikolojia. Wengi wamepigwa sana na askari kipindi cha upelelezi miguu kuvunjwa mikono kuvunjwa wengi wanachechemea na majeraha makubwa mwilini na kutengwa na ndugu zao hakika wanakua kwenye kipindi kigumu sana .

Ombi langu kubwa ni kwa askari kukamilisha upelelezi mapema na wapate haki zao mapema, wengi wanafia ndani bila kuhukumiwa

Mahakama ziangalie pale na division ya kuhukumu kesi za mauaji tu zimekuwa nyingi na wengi wanaishia rumande miaka 10-15 bila kupata hukumu.
Huyu kamuua mama yake mzazi. Askari magereza wata enjoy sana.

7F815EF1-8107-4DAF-AFFC-8D8BCD85A7D8.jpeg
 
Unatetea ujinga
Ipo ivii?
Kmf: umekamatwa kwa tuhuma za mauwaji kisha ukabanwa na kukiri kuwa umeua, je watakuamini umeuwa bila kwenda kuonesha silaha na vielelezo vingine ulivyoitumia kuua ili kuthibitisha?

Na je katika upelelezi ukikiri hata kipenda roho bila ya kulazimishwa kwamba ni wewe uliyehusika na tukio fulani, waweza kuishia hapo na wakaamini kuwa wewe ndiye muhusika bila kuonesha support evedences?

Hiyo ndiyo maana yangu.
 
Kesi hizi zinachelewa sababu ya kutumia mida mwingi kuendesha kesi za akina Mbowe
Wrong point mbowe ni mtu wa kawaida kama wengine.

Sio kila mtu anamuabudu kama wewe!
Wabongo tuna stress! Katika maelezo yake hapo juu, ni wapi huyo jamaa amesema anamwabudu Mbowe! Au amesema huyo Mbowe ni mtu wa hadhi ya juu sana!!
 
Back
Top Bottom