Kesi za mauaji zinavyowasumbua mahabusu na wafungwa wengi

Kiundwe taasis/kitengo maalumu cha upelelezi kushughulika kesi kubwa kubwa maana polisi wamelemewa.
 
Waambieni hiyo mitoto inayotaka kuua wazazi wao.
 
Tuhuma za makosa yote zinapaswa kuwa na dhamana, ni sheria za hovyo kupoka haki ya dhamana kwa kosa lolote.
 
Hahaha



Wasaidizi wake wamelala binafsi namshukuru hayati Magufuli alienda butimba kujionea hali na waliosingiziwa walitolewa kwa chifu hangaya sijui kama atakumbuka kwenda gereza lolote
Kinachotakiwa ni katiba mpya itakayoweka haki ya dhamana kwa makosa yote sio huu mtindo wa kusubiri hisani na fadhila za mtu mmoja.
 
Kesi za mauaji murder case ni serious sana hata kwenye nchi maskini z nazoendelea zenye weak judiciary system.
Hili sio tatizo la mahakama tu ni suala la polisi wanaokamata watu bila upelelezi na ushahidi wa kujitosheleza unaoweza kupelekwa na kusikilizwa mahakamani.
 
Kitaalamu inaitwa death row
Death row ni watu waliohukumiwa kifo wanaosubiri hukumu yao kutekelezwa, mleta uzi anazubgumzia watuhumiwa walio mahabusu.
 
Kitengo cha upelelezi kitolewe police kisiwe idera ya police kiwe chini ya mwendesha mashtaka WA serikali itasaidia snaa wakiajiri Kwa mkupuo watu 30000 waanze kukisuka polepole kuliko kuachia polisi
 
Polisi hawana akili. Hata ukikiri kosa mwenyewe bado watasema uchunguzi bado.
Nakumbuka Kuna dogo alikwapua milioni hamsini kazini. Wahasibu walipopelekwa polisi dogo alijitolea akasema ni yeye ndio aliyeiba lkn polisi bado hawakumuamini kwamba ni yeye.
Wanangangania wanafanya uchunguzi.
Mapolisi wakubwa ni kina Kingai na Swila hao wadogo wanaopewa maelekezo na kina Swila unategemea vichwani mwao Kuna ubongo wa namna gani?
 
Jaji mkuu Yuko kwenye huo mfumo kitambo ndio maana sasa ni bosi. Anajua kila kitu, ndio hivyo tena hana nia ya kutafuta suluhisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…