BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 525
- 1,257
Mashauri ya ndoa na talaka 1,358 yamefunguliwa katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Temeke (IJC), Dar es Salaam katika kipindi cha kuanzia Novemba 2021 hadi Julai, 2022.
Idadi hiyo ni sawa na mashauri 220 yanayofunguliwa kila mwezi kituoni hapo, hali inayoonyesha kuyumba kwa taasisi nyeti ya ndoa, hasa mkoani Dar es Salaam.
Mashauri hayo ni miongoni mwa mashauri 4,267 yaliyofunguliwa katika kipindi hicho, kati ya hayo 2,911 yakihusu mirathi.
Hata hivyo, kituo hicho kimefanikiwa kunusuru ndoa 29 kati ya 80, ambazo wanandoa walifikishana hapo kwa ajili ya kuzivunja.
Naibu Msajili wa IJC, Mary Moyo amesema mashauri yanayoongoza kufunguliwa katika kituo hicho ni ya mirathi ambayo ni 2,911, sawa na asilimia 62 ya mashauri yote, ikifuatiwa na mashauri 1,358 ya ndoa na talaka sawa na asilimia 38.
Kwa upande wa mashauri ya ndoa yaliyofunguliwa katika kipindi hicho, Moyo alisema mashauri yanayoongoza ni ya talaka, wanandoa kuomba kutengana, mgawanyo wa mali baada ya ndoa kuvunjika, matunzo ya watoto na sehemu wanakotakiwa kuishi watoto baada ya wazazi wao kutengana.
Alisema kati ya mashauri 1,358 ya ndoa, mashauri 1,127 ndiyo yaliyosikilizwa na kutolewa maamuzi, huku mashauri 231 yakiwa bado hayajatolewa uamuzi.
“Takwimu hizi ni tangu kituo hiki kilipoanza kutoa huduma Novemba, 2021 hadi Julai 19, 2022 na wanaokuja kupata huduma katika kituo hiki wengi ni wanawake ambao wamekuwa wakifungua kesi za ndoa, talaka, malezi ya watoto na upande wa wajane wamekuwa wakifungua kesi za mirathi,” alisema Moyo.
Kuhusu mirathi, Moyo alisema tayari wasimamizi wa mirathi 2,376, sawa na asilimia 82 wameshateuliwa na mahakama hiyo kukusanya mali na madeni katika kipindi hicho.
Alieleza sababu kubwa ya kituo hicho kupokea kesi nyingi kwa kipindi kifupi ni kutokana na kituo hicho kuhudumia mkoa mzima wa Dar es Salaam.
Tofauti na mahakama nyingine, kituo hicho kina ngazi tano za mahakama kwa pamoja, yaani Mahakama ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, jambo ambalo limerahisisha watu kupata huduma kwa urahisi.
Chanzo: Mwananchi