Kesi za ndoa na talaka 1,358 zafunguliwa ndani ya miezi 8 Dar es Salaam

Kesi za ndoa na talaka 1,358 zafunguliwa ndani ya miezi 8 Dar es Salaam

Aisee!? Shida wengi wanaingia kwenye hizo ndoa wakiwa wahajakomaa kiakili wanazania wataishi daima kama walivyo kuwa wanaishi maisha ya uchumba
 
Watu wanaoana bila tafiti. Zipo tabia haziendani, zipo herufi za majina haziendani, zipo number za majina haziendani, ipo miungu, mizimu haiendani. Roho zinashambuliwa wengi hawajui kinga za kiroho, kusafisha Roho zilizochafuka. Vyote hivi uleta misuguano kwenye mahusiano na kupelekea watu kutengana.
Ndoa ni mawimbi kwann uogope mawimbi
 
Ngoja nisikilize tena wimbo wa stamina aliyechapiwa mke na mchezaji wa Simba mpaka ndoa ikavunjika.
Alafu madem wanato-mb-wg bwelele na wachezaj mpira na wasanii
Wanawapa k kiubwete kabisa

Ova
 
Watu wanaoana bila tafiti. Zipo tabia haziendani, zipo herufi za majina haziendani, zipo number za majina haziendani, ipo miungu, mizimu haiendani. Roho zinashambuliwa wengi hawajui kinga za kiroho, kusafisha Roho zilizochafuka. Vyote hivi uleta misuguano kwenye mahusiano na kupelekea watu kutengana.
Ndoa ni mawimbi kwann uogope mawimbi
sasa sio wote wana elimu ya numerology/astrology mkuu
 
Mashauri ya ndoa na talaka 1,358 yamefunguliwa katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Temeke (IJC), Dar es Salaam katika kipindi cha kuanzia Novemba 2021 hadi Julai, 2022.

Idadi hiyo ni sawa na mashauri 220 yanayofunguliwa kila mwezi kituoni hapo, hali inayoonyesha kuyumba kwa taasisi nyeti ya ndoa, hasa mkoani Dar es Salaam.

Mashauri hayo ni miongoni mwa mashauri 4,267 yaliyofunguliwa katika kipindi hicho, kati ya hayo 2,911 yakihusu mirathi.

Hata hivyo, kituo hicho kimefanikiwa kunusuru ndoa 29 kati ya 80, ambazo wanandoa walifikishana hapo kwa ajili ya kuzivunja.

Naibu Msajili wa IJC, Mary Moyo amesema mashauri yanayoongoza kufunguliwa katika kituo hicho ni ya mirathi ambayo ni 2,911, sawa na asilimia 62 ya mashauri yote, ikifuatiwa na mashauri 1,358 ya ndoa na talaka sawa na asilimia 38.

Kwa upande wa mashauri ya ndoa yaliyofunguliwa katika kipindi hicho, Moyo alisema mashauri yanayoongoza ni ya talaka, wanandoa kuomba kutengana, mgawanyo wa mali baada ya ndoa kuvunjika, matunzo ya watoto na sehemu wanakotakiwa kuishi watoto baada ya wazazi wao kutengana.

Alisema kati ya mashauri 1,358 ya ndoa, mashauri 1,127 ndiyo yaliyosikilizwa na kutolewa maamuzi, huku mashauri 231 yakiwa bado hayajatolewa uamuzi.

“Takwimu hizi ni tangu kituo hiki kilipoanza kutoa huduma Novemba, 2021 hadi Julai 19, 2022 na wanaokuja kupata huduma katika kituo hiki wengi ni wanawake ambao wamekuwa wakifungua kesi za ndoa, talaka, malezi ya watoto na upande wa wajane wamekuwa wakifungua kesi za mirathi,” alisema Moyo.

Kuhusu mirathi, Moyo alisema tayari wasimamizi wa mirathi 2,376, sawa na asilimia 82 wameshateuliwa na mahakama hiyo kukusanya mali na madeni katika kipindi hicho.

Alieleza sababu kubwa ya kituo hicho kupokea kesi nyingi kwa kipindi kifupi ni kutokana na kituo hicho kuhudumia mkoa mzima wa Dar es Salaam.

Tofauti na mahakama nyingine, kituo hicho kina ngazi tano za mahakama kwa pamoja, yaani Mahakama ya Mwanzo, Mahakama ya Wilaya, Mahakama ya Hakimu Mkazi, Mahakama Kuu na Mahakama ya Rufani, jambo ambalo limerahisisha watu kupata huduma kwa urahisi.


Chanzo: Mwananchi
Kuanzia kuchagua mchumba,kuposa hadi ndoa,izi hatua zote ni muhimu sana kumshirikisha Mungu,unaomba Mungu akupatie mchumba omba mungu,umepata mchumba omba mungu pia,unaenda posa omba mungu na hata wakati wa kukaribia ndoa omba Mungu,na katika izo nyakati zote omba Mungu akubainishie mke aliye mwema kwako,ndani ya maisha yako na wakati wa uzao wako
 
Back
Top Bottom